DOKTA APOKEA KIPIGO KIKALI, KISA? KAWEKA POZI KAMA MUISLAMU...

KUSHOTO: Waislamu wakiwa katika sala. KULIA: Dk Masood Ahmad.
Daktari wa Uingereza mwenye umri wa miaka 72 amefungwa jela nchini Pakistani kwa 'kuweka pozi kama Muislamu' baada ya wanaume wawili waliojifanya kuwa wagonjwa kumrekodi akisoma Kurani.
Masood Ahmad, mfuasi wa jumuiya ya Ahmadiyya, alikamatwa mjini Lahore mwezi uliopita baada ya wanaume wawili kumkaba shingoni' na kumpiga.
Ahmadi alitumikia sehemu kubwa na maisha yake akifanya kazi kama daktari mjini London, lakini alirejea Pakistani mwaka 1982 na kufungua duka la dawa.
Kwa mujibu wa sheria ya Pakistani, wafuasi wa Ahmadiyya sio Waislamu na wanaweza kufungwa jela miaka mitatu kwa 'kuweka pozi kama Waislamu' au 'kufisadi hisia za Waislamu'.
Kaka wa Ahmad amesema wanaume wawili waliokaa kama wagonjwa walimuuliza maswali kuhusu imani yake na kutumia simu za mikononi kumrekodi kwa siri akisoma aya kutoka kwenye Korani.
"Alimwambia "wewe ni kama baba yangu, tafadhali nisaidie maswali kadhaa", Nasir Ahmad alisema.
"Pale kaka yangu alipojibu, walianza kumpiga na kumkokota nje huku wakiwa wamemkaba shingoni."
Masood Ahmad alishindwa mashauri ya dhamana mara tatu, lakini ameendelea kukaa rumande.
Shauri moja lilisikilizwa huku kundi la watu likiimba vibwagizo vya kuipinga Ahmadiyya na mwanasheria wake alidaiwa kuhofia mno kuweza kuhudhuria mashauri mengine mawili.
Mtoto wake wa kiume, mmoja kati ya saba walioko nchini Uingereza na Australia, alisema familia hiyo inashuku mtu mmoja alikuwa akijaribu kupora zahanati ya baba yake.
"Najisikia hasira mno sababu siwezi kufanya lolote kutoka hapa," alisema Abbas Ahmad mwenye miaka 39, dereva taksi mjini Glasgow. Inaudhi kujua kwamba watu walikuwa wakipanga njama dhidi ya mtu unayempenda."
Mmoja wa washitaki wake, mwalimu wa kidini Muhammad Ihsan, amesema Ahmad amewahubiria kinyume cha sheria.
Jumuiya ya Ahmadiyya imekabiliwa na mashitaka ya kidini kwa miongo kadhaa sasa. Mwaka jana, kesi 20 dhidi ya wafuasi wa Ahmadiyya waliodaiwa 'kuweka pozi kama Waislamu', licha ya kundi hilo kudai Uislamu ni imani yao.
Kesi moja ilishuhudia mfanyakazi wa benki akikamatwa kwa kuvalia pete yenye aya za Kurani na nyingine familia nzima ilishitakiwa kwa kuandika salamu ya Kiislamu kwenye mwaliko wa harusi.
Wafuasi wachadini walipanga mara mbili kukamatwa kwa mji mzima wa wafuasi wa Ahmadiyya, watu 60,000, kwa kufanya sherehe za kidini. Wakazi walikuwa wakigawa chakula, kutoa peremende na kuonesha vitambaa vya mapambo mbalimbali, walisema washitaki hao.
"Hatutakuwa na tatizo nao kama hawatatumia jina Uislamu na alama za Kiislamu," alisema Tahir Ashrafi, mkuu wa Baraza lenye nguvu la wachadini la Ulema.
"Tunapingana na mauaji ya wasio na hatia. Kama mashambulizi hayakubaliki au kuruhusiwa, lakini kama wanavunja sheria, tunayo haki ya kuwashitaki kwa polisi," alisema.
Kuna takribani nusu milioni ya wafuasi wa Ahmadiyya nchini Pakistani, viongozi wao wanasema. Wengi wao wanajisikia salama huko Rabwa, mji walionunua wakati Pakistani ilipoundwa mwaka 1947.

No comments: