![]() |
| Ng'ombe wakiwa malishoni. |
Kukabidhiwa hati mfugaji na mkulima huyo kumetokana na kuhamasika na kuamua kuuza baadhi ya mifugo yake, ili ajenge makazi bora baada ya kuishi kwenye nyumba ya tembe mpaka sasa.
Sasa mfugaji huyo mwenye watoto wa kiume 30 na wa kike 22 amebakiwa na ng'ombe 600, kondoo na mbuzi 200, shamba la ekari 300 na amekopa trekta ili kumsaidia katika shughuli za kilimo.
Alisema trekta hilo lenye thamani ya Sh milioni 32, ameshalilipia Sh milioni 11 na pia amejenga nyumba ya kulala wageni Bahi Mjini na amechangia fedha ujenzi wa Shule ya Msingi Kidete.
Alisema changamoto kubwa inayomkabili ni uhaba wa maji lakini anafanya juhudi kuhakikisha anatafuta wataalamu wa kuchimba kisima.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Betty Mkwasa alisema sasa amejizatiti kuhakikisha anafikia wafugaji wengi ili wapate elimu na kuuza mifugo ili kuwa na makazi bora.
Alisema katika wilaya yake kuna wafugaji wenye ng'ombe wengi wanaoishi maisha duni wakati wanaweza kupunguza mifugo yao kwa kuiuza na kupata fedha za ujenzi wa makazi bora na kupeleka watoto wao shule.
Katika mpango huo wa kuhamasisha wafugaji kuwa na makazi bora wamefanikiwa kwani nyumba yake ya wageni imetoa ajira kwa wananchi wengine.
Mkwasa alisema walimpa mfugaji huyo ramani kutokana na kuwa ni mkulima na mfugaji mkubwa anayeishi kwenye nyumba duni.
Alisema Kamite pia alihamasishwa kuingia katika kilimo bora na cha kisasa na kumudu kununua trekta hilo.
Akimkabidhi ramani hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk Rehema Nchimbi alisema ni vizuri kama wafugaji watabadilika na kuuza baadhi ya mifugo na kuweza kuwa na maisha bora.
Alisema wafugaji wengine wanatakiwa kuiga mfano huo ili kufurahia utajiri wao wa mifugo kwa kuishi kwenye makazi mazuri na kuachana na tabia ya kumiliki mifugo mingi huku wakiendelea kuishi masikini.

No comments:
Post a Comment