![]() |
| Freeman Mbowe. |
Alisema hivi karibuni kumekuwa na kauli za baadhi ya mawaziri na wabunge za kufikiria kujitoa katika jumuiya hiyo, alisema ana imani sasa matatizo yaliyojitokeza katika EAC yatakwisha kwani jumuiya hiyo ni muhimu kwa uchumi, kijamii na kiutamaduni.
“Kuuvunja ni hasara kubwa kuliko kuujenga, Rais aweke juhudi zaidi, asisite kutumia hata asasi za ndani na nje ya nchi kuimarisha jumuiya na uamuzi wa nchi,” alisema Mbowe na kuongeza; “Lakini katika kujenga, hatua ni muhimu kuchukuliwa na kuzingatia”.
Alisema ni kweli tupo taratibu kwa kuwa tunaenda kwa hatua lakini inapaswa pia kwenda kwa haraka na kupendekeza isichukuliwe miaka 30 kwani wengine wanakereka kutokana na namna mambo yanavyokwenda.
Mbowe alisema tabia ya vyombo vya habari kushabikia Jumuiya ivunjike si njema kwani Tanzania ikigombana na Kenya ama Uganda, tutabaki na majirani gani, alisema Rais hapaswi kulalamika bali kupata muda wa kujadili na wenzake ili kujua kulikoni.Akizungumzia kuhusu ajira, alisema lazima kukubali changamoto na kutafakari ni kwa nini tatizo lipo ili kulitafutia ufumbuzi.
Naye Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR-Mageuzi), alimpongeza Rais kwa hotuba nzuri na kwamba imeondoa madukuduku ya wananchi kuhusu Jumuiya hiyo.
Alisema hatua za marais watatu wa Kenya, Uganda na Rwanda si vya kiungwana na kwamba malalamiko ya Rais Kikwete juu ya viongozi hao ni sahihi.
Pongezi nyingine zimetoka kwa Katibu Mkuu wa NCCR-Mageuzi, Sam Ruhuza, akisema hotuba ya Rais Kikwete imejaa matumaini kwa watanzania juu ya hatima ya muungano wa jumuiya ya Afrika Mashariki.
"Mawaziri wake waliongea kwa kukata tamaa kwamba tunasubiri talaka tuu tofauti na hotuba ya Rais ambayo ilitoa mwanga tena kwa watanzania imeonesha Rais alivyo na msimamo," alisema Ruhuza.

No comments:
Post a Comment