![]() |
| Wanandoa hao, Ryan Barry (kushoto) na Ashley Cyr. |
Ryan Barry, miaka 30, na Ashley Cyr, miaka 26, wote wakazi wa Quincy, walikamatwa Ijumaa. Hawakupatikana na hatia na waliamriwa kushikiliwa kwa dhamana ya Dola za Marekani 200,000 taslimu.
Binti huyo wa wanandoa hao, Mya Barry, alifariki Septemba 2011, wakati familia hiyo ikiishi mjini Marshfield, mwendo wa nusu saa kwa gari kusini-mashariki mwa Quincy.
Polisi walifika baada ya kupigiwa simu na kukuta mtoto huyo akiwa kwenye sakafu sebuleni na bibi yake wakimpima CPR, Ofisi ya Mwanasheria wa Mahakama ya Wilaya ya Plymouth, Tim Cruz ilisema.
Mtoto Mya alikimbizwa kituo cha afya cha South Shore, ambako alitangazwa kufariki dunia muda mfupi baadaye.
Polisi walisema walikuta gramu 3 za heroin na sindano ndani ya chanja katika chumba chake wanachochangia na Barry, Cyr, mtoto huyo na dada zake wawili, wenye umri wa miaka mitatu na minne.
Mwendesha mashitaka Frank Middleton alisema Barry aliwaeleza polisi kwamba Cyr hakuwa makini na matumizi yake ya dawa za kulevya na kwamba alikuwa ameonekana akiwa ametelekeza heroin kwenye kitabu cha Dk. Seuss na kisha kutelekeza kitabu hicho sakafuni ambako watoto hao wangeweza kuzichukua.
Middleton alisema mahakamani kwamba Barry aliwaeleza polisi kwamba majira ya Saa 1:30 Septemba 23, 2011, alimwandalia mtoto huyo chupa yake ya mwisho kwa kuchanganya vifuniko viwili vya heroin na vifuniko viwili vya maji.
Alisema kwamba wakati Barry alipohoji jinsi heroin hiyo ilivyoingia kwenye chupa hiyo alisema pengine kuna mtu ameoshea bomba chafu la sindano kwenye chupa hiyo yenye maji aliyotumia kuandaa mchanganyiko huo.
Uchunguzi umebaini kwamba mchanganyiko wa mtoto huyo kwenye chupa ulijumuisha heroin. Uchunguzi umebaini kwamba mtoto huyo alifariki kutokana na dawa ya kutia usingizi.
Baraza Kuu la Mahakama lilirejesha mashitaka rasmi ya kuua bila kukusudia dhidi ya Barry na Cyr Alhamisi. Cyr pia alishitakiwa kwa shitaka moja ya uzembe uliomweka hatarini mtoto.
Middleton alisema mahakamani kwamba mtoto Mya alizaliwa akiwa ameathirika kwa heroin sababu mama yake alikuwa ametumia dawa hizo za kulevya kila siku tangu aliposhika mimba ya mtoto huyo.
Mwanasheria wa Barry, Liam Scully, alisema kwamba haikufahamika aliyeweka heroin katika chupa ya mtoto huyo na kwamba Barry amekana kufanya makosa yeyote.
"Alipagawa kutokana na kifo hicho cha binti yake na anakubaliana kwamba janga hilo ni funzo kubwa kwake," alisema Scully.
Mwanasheria wa Scully hakupokea simu zilizomtaka kuzungumzia suala hilo Ijumaa.
Barry na Cyr wanatarajiwa kurejea mahakamani Novemba 8 kwa usikilizwaji wa suala hilo.
Imeripotiwa kwamba Barry amekuwa na majanga mengi yanayohusiana na sheria kwa miaka kadhaa sasa. Mwaka 2006, alipatikana na hatia ya kumbaka msichana mdogo wa chini ya umri wa miaka 16 wakati wa sherehe ya kutumia dawa za kulevya na kunywa pombe.
Alihukumiwa kifungo cha miaka miwili na nusu jela, lakini akatumikia miezi 15 na akawekwa chini ya uangalizi kwa miaka mitatu.
Aprili mwaka huu, mwanaume huyo mwenye miaka 30 pia alipatikana na hatia ya kumiliki heroin.

No comments:
Post a Comment