![]() |
| Jeneza sahihi likiwa limewekwa tayari kwa mazishi. |
Bahati wakati msafara ulipowasili mfanyakazi mmoja wa Southampton Crematorium (Kampuni ya huduma ya uchomaji maiti) alikagua kibao chenye jina la marehemu na kubaini haukuwa mwili wa mzee mwenye umri wa miaka 77.
Mashuhuda walisema tukio hilo liliwaacha waombolezaji wakiingia kwa utulivu kwenye kanisa dogo huku wakingojea jeneza hilo sahihi.
Wakurugenzi wa msiba Nigel Guilder Ltd kutoka Chandler's Ford, Hampshire, haraka walijipanga na kwenda kuchukua jeneza sahihi baada ya kosa kugundulika.
Waliondoka na kurejea muda mfupi baadaye wakiwa wamebadili jeneza hilo na kuleta lililo sahihi.
Wakati hili likitokea familia hiyo ilitakiwa kusubiri ndani ya kanisa hilo dogo wakati mabadiliko hayo yakifanyika.
Marafiki na jamaa walikusanyika kwenye kanisa dogo la East la Southampton Crematorium kutoa heshima zao za mwisho.
Mpendwa wao alikuwa amefariki akiwa na umri wa miaka 77 kufuatia kuugua kwa muda mrefu.
Haikuweza kufahamika mara moja endapo familia ya mtu ambaye jina lake lilikuwa kwenye jeneza la kwanza walitaarifiwa nini kilichotokea.
Nigel Guilder Ltd na familia hiyo wamekataa kuzungumzia mkasa huo.
Mkurugenzi mwingine wa msiba alisema: "Hili ni jambo la kutisha kutokea kwa familia yoyote.
"Kuna taratibu za kutosha kufanyika kuhakikisha hili haliwezi kutokea."

No comments:
Post a Comment