![]() |
| Mabasi na malori yakipimwa uzito kwenye mizani ya Kibaha, Pwani. |
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ameruhusu mabasi na malori, kuendelea kusafirisha abiria na mizigo kwa kufuata utaratibu wa awali kwa mwezi mmoja, wakati Serikali ikisubiri ushauri kutoka kwa timu itakayoundwa kwa kuhusisha pande zinazovutana.
Pinda alisema hayo jana baada ya kupata maelezo ya baadhi ya mawaziri na wawakilishi wa wamiliki wa malori na mabasi, kuhusu mvutano uliojitokeza na kusababisha wamiliki wa vyombo hivyo vya usafirishaji kugoma.
Amesisitiza kuwa ni lazima pande mbili hizo zifanye utafiti wa kina kuhusu mambo yanayolalamikiwa na kutoa uamuzi wa kudumu.
Katika kufanikisha utafiti huo, Serikali itatoa timu ya wataalamu itakayofanya kazi pamoja na wawakilishi wa wasafirishaji hao, ili kuja na uamuzi weye tija na wa kudumu.
"Kwa hili suala, kuwashirikisha wadau ni jambo la msingi na busara kwa sababu uchumi wa nchi unategemea sekta hii kwa kuwa asilimia 90 ya bidhaa zote ikiwemo chakula, zinasafirishwa kwa malori huku asilimia 64 ya mizigo hiyo ikienda nchi jirani.
"Hivyo hawa ni wadau wakubwa wa usafirishaji, inatupasa tuzungumze nao ili jambo hili tulimalize vizuri…kumekuwepo mrundikano wa shehena huko bandarini kutokana na meli kutoshusha mizigo ndio maana tumeona tulitazame kwa mapana suala hili," alisema Pinda.
Mwaka 2006, Wizara ya Ujenzi ilitoa barua kuruhusu magari hayo kuzidisha mizigo juu ya kiwango cha mwisho cha uzito uliowekwa kisheria kisheria wa tani 56, lakini si zaidi ya asilimia tano.
Kutokana na barua hiyo, malori hayo yaliruhusiwa kuendelea na safari baada ya kupita mizani na kukutwa na uzito uliozidi tani 56, lakini si zaidi ya asilimia tano ya uzito huo wa kisheria.
Hata hivyo Wizara hiyo ya Ujenzi ikatoa barua nyingine mwaka huu, kwamba kuanzia Oktoba mosi, malori hayo yatii sheria inayotaka yasizidishe mzigo zaidi ya kiwango kilichowekwa kisheria cha tani 56.
Pinda alisema baada ya barua hiyo, Chama cha Wamiliki wa Malori (Tatoa) na Chama Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), waliomba wapewe muda kwa sababu kuna mizigo wanayosafirisha ambayo walishaingia mikataba kabla ya tangazo la Wizara ya Ujenzi, hivyo kubadilisha taratibu ghafla kungevuruga biashara yao.
Hata hivyo Pinda alihadharisha kuwa uamuzi huo wa kuruhusu utaratibu wa awali, usitoe fursa kwa wasafirishaji kuzidisha uzito. "Bado utaratibu wa kupima utaendelea ili watakaozidisha uzito wachukuliwe hatua."
"Ni lazima kama nchi tujali barabara zetu na kuzilinda hivyo naagiza kuwa malori na mabasi yatakayozidisha uzito nje ya utaratibu huu wa asilimia tano, wachukuliwe hatua kali," alisema Pinda.
Pinda pia ameamuru malori yote yaliyosafiri kuanzia jana yaanze kupima uzito katika mizani ya Mikese, Morogoro na Chalinze mkoani Pwani, ili kuepusha msongamano utakaokuwepo kutokana na tangazo hilo la Serikali litakalosababisha wasafirishaji kuanza safari ambazo walikuwa wamezisitisha.
"Natambua kwa uamuzi huu kutakuwa na msongamano mkubwa wa malori, ili kuepusha hali hiyo nashauri malori yakapime Mikese na yanayoenda njia ya Tanga, yapime mzani wa kwanza baada ya Kibaha. Hii itasaidia kuepusha msongamano wa magari kutoka Dar es Salaam hadi Kibaha," alisema.
Kuhusu uundaji wa timu hiyo ya wataalamu, Pinda alisema ameagiza Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Uchukuzi, Wizara ya Viwanda na Biashara na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, kuunda timu ya wataalamu watakaokutana na wawakilishi wachache wa Tatoa na Taboa, ili kupitia kanuni hizo kwa lengo la kupata muafaka.
"Ninatoa mwezi mmoja kwa wizara husika na wadau hao kukamilisha kazi hiyo, katika kipindi hicho cha mpito, utaratibu uliokuwepo awali kabla ya tangazo la Oktoba mosi, utaendelea kutumika," alisema Pinda.
Alisema katika kikao cha Serikali na wawakilishi wa Tatoa na Taboa, wadau hao wa sekta ya usafirishaji walilalamika tatizo la tafsiri sahihi ya sheria husika katika vituo vya mizani hasa baada ya Wizara ya Ujenzi kufuta barua ya Waziri wa Ujenzi ya mwaka 2006, na kuanza kulipishwa faini kwa uzito ambao awali ulipita bila kulipiwa.
Pinda alikiri kuwa kuna changamoto za upimaji wa magari katika mizani, ikiwemo ya vitendo vya rushwa vinavyofanywa na watumishi wa Wakala wa Barabara (Tan roads), kwa kushirikiana na wasafirishaji waharibifu kupitisha magari yenye uzito unaozidi viwango vinavyoruhusiwa.
"Wasafirishaji wameingia makubaliano yasiyo rasmi na baadhi ya watumishi wa mizani ili magari yao yapite kwenye mizani katika muda ambao watumishi hao watakuwa zamu, ili wayapitishe magari hayo yakiwa yamezidisha uzito bila kutozwa faini inayotakiwa," alisema Pinda.
Aliongeza kuwa ili kukabiliana na tatizo hilo la rushwa, Wizara ya Ujenzi imefukuza watumishi 400 wa kwenye mizani na imeajiri watumishi wenye shahada ambao wamekula kiapo cha kutopokea rushwa.
Wakati huo huo, Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA CCC), limelaani mgomo wa mabasi yaendayo mikoani kwa kuwa ulikiuka haki za msingi za watumiaji wa huduma za usafiri wa barabara .
Baraza hilo limedai kuwa haki iliyokiukwa ni haki ya kupewa taarifa na haki ya usalama wa abiria.
Aidha baraza hilo limetoa rai kwa abiria wote walioathiriwa na mgomo au vurugu hizo, kuwasilisha madai yao kwenye kampuni walizokuwa wasafiri nazo na lipatiwe nakala kwa ajili ya kudai fidia kwa usumbufu walioupata, ambao kimsingi haukuwa na sababu.
Akizungumza jana na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Baraza hilo, Ayoob Omari, alisema walipokea taarifa ya mgomo huo kwa masikitiko makubwa na kushuhudia mateso kwa abiria hususani wanawake na watoto waliokuwa wanasafiri siku hiyo katika Kituo cha Mabasi Ubungo.
Katika taarifa ya Omari iliyosomwa kwa niaba yake na Katibu Mtendaji wa baraza hilo, Oscar Kikoyo, ilieleza kuwa kugoma kutoa huduma ni kuwakomoa abiria masikini ambao sio sehemu ya mgogoro wa wenye mabasi dhidi ya sheria husika wakati usafiri wa mabasi ndio tegemeo lao.
“Baraza linachukua fursa hii kuwakumbusha wamiliki wa mabasi kuwa abiria akishakata tiketi anakuwa ameingia mkataba na kampuni yako. Kitendo cha kugoma kwa sababu ambazo hazina uhusiano wa moja kwa moja na abiria, hakina uhalali wowote wa kukatisha mkataba wako na abiria,” alisema.
Pia alitoa mwito kwa watumiaji wa usafiri wa nchi kavu na majini ambao wanatarajia kusafiri mwishoni mwa mwaka kuanza kukata tiketi mapema, ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza kama ilivyo kawaida ya mwisho wa mwaka.
Alisema mwaka huu wataadhimisha siku ya kumbukumbu ya waathirika wa ajali ulimwenguni kote Novemba 17 ambapo kaulimbiu ya mwaka huu ni “Usalama wa barabara kwa watu wote.”

No comments:
Post a Comment