Baadhi ya waandamanaji kwenye ghasia hizo zilizokatisha uhai wa watu 19. |
Vurugu zilizoambatana na ghasia zimeua watu 19 kaskazini mwa India baada ya makundi ya Wahindu na Waislamu kushambuliana kwa bunduki na visu kutuliza makelele ya matusi mtaani.
Ghasia hizo zilianza kwa mauaji ya wanakijiji watatu ambao walijitokea kumlinda msichana mmoja aliyekuwa akisumbuliwa huko Kawal, Jimbo la Uttar Pradesh wiki iliyopita.
Hasira ilifoka katika eneo tangu tukio hilo, lakini vurugu zinabadilika na kuwa za kutisha Jumapili pale mwandishi mmoja, mpigapicha mmoja wa polisi na wanakijiji kadhaa walipokufa kutokana na vurugu hizo.
Zaidi ya watu ishiri wamekufa kutokana na majeraha yao yaliyotokana na mapigano ya Jumamosi katika wilaya ya Muzaffarnagar, baada ya vurugu kusambaa kwenye vijiji kadhaa vya jirani.
Serikali imeingilia kati kwa kupeleka mamia ya askari kuzima vurugu hizo na kufanya msako wa silaha katika eneo hilo, wakati hali ya hatari ikiwa imeweka huko Uttar Ptadesh, eneo la makazi ya watu milioni 200.
"Amri ya kutotembea usiku imewekwa kwenye maeneo matatu yaliyoathiriwa zaidi na ghasia hizo ya Muzaffarnagar," alisema mkuu wa mambo ya ndani ya jimbo hilo, R.M. Srivastava.
Ghasia zililipuka Jumamosi mchana baada ya maelfu ya wakulima wa Kihindu kufanya mkutano kwenye kijiji cha Kawal kudai haki katika mauaji ya Agosti 27 ya wanaume watatu ambao waliongea pale mwanamke mmoja alipokuwa akisumbuliwa kwa maneno.
Waziri mdogo wa afya jimboni humo, Mohammad Azam Khan, alisema wahudhuriaji hao walikuwa wakihutubia kutaka Waislamu wauwawe kujibu mapigo ya vifo vya wanakijiji hao watatu.
Wakulima hao walishambuliwa wakati wakirejea nyumbani baada ya mkutano huo, ofisa wa juu wa polisi Arun Kumar alisema, akiongeza kwamba washambuliaji hao wanaonesha kuwa walipanga shambulio lao kutokana na kuwa na silaha za 'bunduki kubwa na vitu vyenye ncha kali.'
Milio ya bunduki iliripotiwa kutoka sehemu mbalimbali za kijiji hicho. Ndani ya masaa kadhaa mapigano yakaibuka kwenye vijiji vya jirani, alisema Kumar.
Mtangazaji wa kituo cha habari cha IBN 7, Rajesh Verma alipigwa risasi kifuani wakati akiripoti maandamano ya jumuiya mjini Abupura, na kufariki katika eneo hilo la tukio.
Uttar Pradesh lilikuwa kitovu cha mapigano mabaya zaidi ya jumuiya nchini India Desemba mwaka 1992, baada ya kundi la Hindu kuharibu kabisa msikiti wa Babri uliojengwa karne ya 16 mjini Ayodhya.
Serikali imeonya kwamba India inashuhudia ongezeko la ghasia za jumuiya, huku matukio 451 yakiwa tayari yameripotiwa mwaka huu, kulinganisha na 410 kwa mwaka mzima wa 2012.
Kwa mwezi Agosti pekee ghasia za jumuiya zimeua watu wawili na kujeruhi 22 katika kijiji kimoja huko jimbo la Bihar, mashariki mwa Uttar Pradesh, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya India.
No comments:
Post a Comment