MWANAMKE ABAMBWA AKISAFIRISHA COCAINE KWENYE MIMBA BANDIA...

KUSHOTO: Mwanamke huyo na mimba yake bandia baada ya kukamatwa. KULIA: Uwanja wa ndege wa Bogota.
Mwanamke mmoja wa Toronto ambaye alijifanya mjamzito kujaribu kusafirisha kilo mbili za dawa za kulevya aina ya cocaine amekamatwa jana kwenye Uwanja wa ndege wa Bogota na polisi wa Colombia.

Kanali Esteban Arias amesema Tabitha Leah Ritchie mwenye miaka 28 alisimamishwa wakati akijaribu kupanda ndege ya Air Canada mjini Bogota baada ya mkaguzi mmoja kubaini kwamba tumbo lake lilikuwa na ubaridi usio wa kawaida na gumu.
Amesema polisi waligundua tumbo bandia lililotengenezwa kwa ulimbo wa mpira na kufungwa kwenye mwili wake kwa gundi na kukuta kilo mbili za cocaine.
Polisi wamesema Ritchie aliwasili nchini Colombia mnamo Agosti 6 na alijitambulisha kama mfanyakazi wa kujitolea.
Ubalozi wa Canada haukujibu maombi ya kutoa taarifa zaidi.
Maofisa wa Colombia wamesema watu 874 kutoka mataifa mbalimbali ya nje wanashikiliwa kwenye mahabusu za nchini humo, wengi wao kwa mashitaka ya dawa za kulevya.

No comments: