KIKONGWE WA ETHIOPIA MWENYE MIAKA 160 ATISHIA REKODI YA DUNIA...

Dhaqabo Ebba.
Watu wengi hawafahamu kuhusu uvamizi wa Italia nchini Ethiopia mwaka 1895, lakini mwanaume mmoja hafahamu tu kuhusu mapambano hayo - anadai kuwa aliishi kipindi chote hicho.

Mkulima mstaafu Dhaqabo Ebba, kutoka Ethiopia, anasema amefikisha umri wa miaka 160, ambayo inaweza kumfanya kuwa mwenye umri mkubwa zaidi duniani ambaye bado anaishi.
Anadai kuwa na kumbukumbu kamili za uvamizi wa Italia nchini kwake katika karne ya 19 - hatahivyo, hakuna cheti cha kuzaliwa kuthibitisha umri wake.
Katika taarifakwenye kituo cha televisheni cha Oromiya, alitoa taarifa nyingi za kina kuhusu historia ya eneo lake ambazo zilimshawishi mwandishi Mohammed Ademo kwamba Ebba lazima atakuwa na umri wa takribani miaka 160.
Hii itamfanya amzidi kwa miaka 46 anayeshikilia rekodi hiyo ya mtu mzee zaidi.
"Wakati Italia ilipoivamia Ethiopia nilikuwa na wake wawili, na mtoto wangu wa kiume alikuwa mkubwa vya kutosha kuchunga mifugo", alisema Ebba.
Kisha alikumbukia safari yake ya siku nane akisafiri kwa farasi kurejea Addis Ababa akiwa mtoto - safari ambayo leo huchukua masaa machache tu.
Wakati Ebba akikua katika jamii isiyoandikwa, hakukuwa na matumizi ya karatasi na mashahidi walio hai kuthibitisha umri wake.
Hatahivyo, kama madai yake yanaweza kuthibitishwa kitabibu, atampiku Misao Okawa mwenye miaka 115, ambaye kwa sasa anatambulika na Guinness World Records kama mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani ambaye bado anaishi.
Pia atampita mwanamke wa Ufaransa Jeanne Calment kama mtu mwenye umri mkubwa zaidi kuwahi kutokea duniani.
Calment alifariki mwaka 1997 akiwa na umri wa miaka 122.

No comments: