Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC), Jacques Rogge akionesha jina la jiji la Tokyo, usiku wa kuamkia leo lililochaguliwa kuandaa Michezo ya mwaka 2020. |
Tokyo itaanda Michezo ya Olimpiki 2020 baadaya kura zilizopigwa na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki usiku wa kuamkia leo.
Wanachama wa ujumbe wa Japan walikumbatiana na kutokwa machozi ya furaha wakati Rais wa OIC, Jacques Rogge akitangaza kwamba mji mkuu huo wa Japan umeuangusha mji wa Istanbul kuandaa michezo hiyo.
Itakuwa mara ya pili kwa Tokyo kuandaa michezo hiyo ya Olimpiki, baada ya kuwa imeandaa Michezo hiyo mwaka 1964.
Jiji hilo limezishinda hofu za hatari za mionzi kutoka kwenye mlipuko wa nyuklia wa Fukushima na kuweza kuibuka kidedea kuandaa Olimpiki hizo za 32.
Istanbul imeshindwa kuandaa Michezo hiyo kwa mara ya tano. Hilo lilikuwa jaribio la pili mfululizo kwa Tokyo kuomba kuwa mwenyeji.
Ujumbe kutoka majiji yote matatu yalijinadi mbele ya kamati hiyo mapema jana kabla ya Tokyo kushinda kura za mwisho 60 kwa 36.
Katika kujinadi kwao kwa mara ya mwisho, Tokyo
Zabuni ya Tokyo ilikuwa yenye mvuto, lakini Istanbul ikacharuka, kwa namna ya kushangaza ikafungana na Madrid katika mzunguko wa kwanza wa kura.
Tokyo linakuwa jiji la tano kuandaa Olimpiki za Majira ya Joto kwa mara ya pili.
No comments:
Post a Comment