Mahali lilipotokea tukio hilo. |
Binti wa India mwenye umri wa miaka sita ambaye alifungiwa kwenye chumba na kubakwa analazimishwa kuolewa na mvulana wa miaka minane ambaye ni mtoto wa mwanaume anayedaiwa kufanya ubakaji huo.
Muathirika huyo, ambaye anaishi kwenye kijiji cha Keshavpura, huko Rajasrhan, alishambuliwa na mwanaume huyo mwenye miaka 40 takribani wiki mbili zilizopita, ilidaiwa.
Badala ya kwenda polisi, familia yake walishitaki kwa wazee wa baraza ambao walifanya mkutano kuamua kinachotakiwa kufanywa kwa mtuhumiwa huyo wa ubakaji.
Kwa namna ya kustaajabisha, baadaye waliwaeleza wazai wa msichana huyo kwamba binti yao lazima aolewe na mtoto wa kiume wa mbakaji huyo.
Wakati huohuo, binti huyo anaaminika kuwa alibakwa tena na mwanaume huyo Jumatano ya juzi, kwa mujibu wa kituo kimoja cha televisheni.
Familia ya muathirika huyo imekataa kutekeleza uamuzi wa wazee hao.
Kesi hiyo ni ya hivi karibuni kabisa katika mlolongo wa mashambulio ya ubakaji dhidi ya wanawake na washichana wadogo nchini India, likiwamo shambulio baya kwa msichana wa miaka 23 mwanafunzi wa udaktari mjini Delhi mwishoni mwa mwaka jana na kubakwa kwa mwandishi wa habari mjini Mumbai mwezi uliopita.
Katika kesi hiyo ya hivi karibuni mjini Keshacpura, ambako ni umbali wa takribani maili 150 kutoka jiji hilo la Jaipur, polisi walihusishwa tu baada ya wanaharakati wa kijamii kumpeleka muathirika na wazazi wake katika Kituo cha Polisi cha Mahaveer Nagar mjini Kota kufungua mashitaka.
Mwanaume huyo alikamatwa na uchunguzi umeanza kuhusiana na madai hayo shidi ya wazee wa baraza.
Msemaji wa polisi alisema: "Alimfungia kwenye chumba na kumbaka binti huyo. Badala ya kufungua mashitaka polisi, wazee walioko kwenye jamii ya binti huyo waliitisha mkutano wa baraza la wazee (panchayat)."
Rajasthan ni moja ya majimbo yanayoshikilia ukale nchini India na, licha ya juhudi za wanakampeni, ndoa za utotoni bado zimeshamiri.
Shambulio hilo limekuja katikati ya maandamano ya nchi nzima kushinikiza mamlaka za India kupitisha sheria kali kwa uhalifu dhidi ya wanawake na wasichana.
Desemba mwaka jana, mwanafunzi wa udaktari mwenye miaka 23 alibakwa na kundi la wanaume na kuuawa wakati akisafiri kwenye basi mjini Delhi.
Kesi hiyo imeibua shutuma kali kutoka kwa wananchi baada ya mmoja wa washambuliaji wake mwenye umri mdogo kuhukumiwa kifungo cha miaka mitatu tu jela ikiwa ni adhabu kwa uhalifu huo.
Wiki iliyopita, baba wa muathirika huyo alizungumzia hukumu hiyo, akisema: "Ni kosa kuzaliwa msichana katika nchi hii."
Mwandishi mwenye umri wa miaka 22 pia alikuwa muathirika wa kubakwa na kundi la wanaume watano kwenye eneo la Shakti Mills mjini Mumbai mwezi uliopita.
Mwanamke huyo, ambaye alikuwa akizindikizwa na mwenzake wa kiume ambaye alipigwa na wabakaji hao, alidaiwa kubakwa wakati akiwa eneo hilo kutekeleza majukumu yake ya kikazi mnamo Agosti 22, mwaka huu.
No comments:
Post a Comment