PAKA ATAFUNA NA KULA MWILI WA MMILIKI WAKE ALIYEFIA JIKONI...

Mwili huo uligunduliwa kwenye nyumba hiyo iliyoko kwenye mtaa huu (kulia).
Mwili wa mpenda wanyama umetafunwa na kuliwa na paka wake mwenyewe baada ya kuwa amefariki nyumbani kwake akiwa peke yake, mahakama ilielezwa.

Kiwiwili kilichonyofolewa viungo cha Janet Veal, mwenye miaka 56, kiligunduliwa kwenye sakafu ya jikoni ya nyumba yake iliyojitenga huko Ringwood, mjini Hampshire, Aprili 4.
Majirani walitoa taarifa za kutomuona mwanamke huyo kwa kipindi kirefu na kugundua kwamba sanduku lake la barua lilikuwa limejaa kupita kiasi, Mahakama ya Afisa Mchunguzi wa Vifo Southampton ilielezwa.
Polisi walilazimika kutumia ngazi kuingia kwenye jengo hilo la ghorofa moja, ambalo liko mwishoni mwa njia ya shamba yenye urefu wa yadi 100, kupitia dirisha lililokuwa wazi ghorofani.
Ndani walikuta 'tukio la kuhuzunisha'. Kulikuwa na idadi kubwa ya wanyama waliokufa - wakiwamo paka na mbwa - jikoni na sebuleni, lakini wengine walinusurika.
Inaaminika wanyama hao wenye njaa walianza kumla mmiliki wao baada ya kuwa wameachwa bila chakula kwa miezi kadhaa.
Ofisa wa polisi Dave Ivey alisema nyumba hiyo haikuonekana ikifunguliwa madirisha kwa wiki kadhaa na hakuweza kuona sakafu kutokana na uchafu huo uliokuwa umetapakaa.
Mahakama ilielezwa kwamba Janet alikuwa ni mtu anayeishi pekee na alikuwa ametelekezwa na mumewe.
Akirekodi kifo hicho kilichotokana na sababu za kawaida, Afisa Mchunguzi wa Vifo, Keith Wiseman alisema: "Wanyama hawa wamekuwa, ofisa huyo alifikiri, waliwekwa kwenye vyumba hivi viwili ghorofa ya chini kwa kipindi cha wiki nyingi, ambacho kiliongezeka na kufikia miezi kadhaa."
Aliongeza: "Hiki pia ulikuwa uzoefu wa kuhuzunisha sababu ilikuwa wazi kwamba sehemu kadhaa za mwili wa Janet hazikuwapo na kufanya, ofisa huyo kupata picha, kwamba vilikuwa vimetafunwa na kuliwa na wanyama hao.
Wiseman alihitimishwa Janet alikuwa ameliwa na paka wake baada ya kuwa amefariki huku mwili wake ukiwa umelala jikoni mwake kwa wiki kadhaa.
Alikuwa akisumbuliwa na matatizo kadhaa ya kifua siku za nyuma, ilielezwa.
Wiseman alisema: "Kilichotokea hasa kumfanya Janet kushindwa kujisaidia mwenyewe au kupata msaada hakijafahamika."

No comments: