Simu ya iPhone 5. |
Mwanamke nchini China amedai amechubuka mboni ya jicho lake baada ya simu yake ya iPhone 5 kulipuka.
Mtumiaji huyo wa simu, aliyetajwa kwa jina la ubini la Li kutoka Dalian, alisema alidhani kwamba iPhone yake ilikuwa imepata moto baada ya kuongea kwa dakika 40.
Alisema kwamba pale alipojaribu kukata simu katika kioo cha simu hiyo haikufanya kazi na kisha ikalipuka kwenye kona ya mkono wa kulia, kupasua kioo na kurusha vipande vya simu hiyo machoni mwake.
Li alisema kwamba alinunua simu hiyo Septemba mwaka jana na kuacha kuitumia baada ya tukio hilo, akiiacha simu hiyo ikiwa na ufa mdogo kwenye kona ya mkono wa kulia, imeripotiwa.
Mwezi uliopita ilidaiwa kwamba mhudumu wa kike kwenye ndege aliuawa kwa mshituko wa umeme wakati alipokuwa akipokea simu katika iPhone 5 yake wakati akiichaji.
Taarifa za kifo hicho cha Ma Ailun, mwenye miaka 23, zilipostiwa kwenye mtandao wa intaneti na dada yake, na kuibua shutuma dhidi ya Apple miongoni mwa mamilioni ya watumiaji wa iPhone nchini humo.
"Nataka kumuonya kila mmoja asipige simu wakati simu hiyo akiwa anaichaji," aliandika dada yake.
Ma, ambaye alikuwa akitarajia kufunga ndoa Agosti mwaka huu, alisemekana kununua iPhone 5 yake Desemba, mwaka jana kutoka duka rasmi katika mji anaoishi katika jimbo la Xinjiang.
Kaka yake alilieleza gazeti moja la Hong Kong simu hiyo ilikabidhiwa kwa mamlaka za China kwa uchunguzi.
Kulikuwa pia na ilani za kiusalama kuhusu kuwapo kwa mamilioni ya simu feki za bei nafuu na chaja sokoni. Bidhaa za Apple huuzwa haraka nchini China, mahitaji hayo husababisha viwanda kuzalisha bidhaa feki za iPhone, iPads na iPods.
Mwaka 2011, maduka 22 feki ya Apple yalifichuliwa kwenye mji mmoja wa China, Kunming, pekee.
Apple imeahidi kuchunguza kifo hicho - pigo kwa kampuni hiyo inayokwenda na teknolojia kwenye soko lake hilo la pili kwa ukubwa baada ya Marekani.
Ilikataa kuzungumza kama ilikuwa ikichunguza kesi hiyo pekee au ilikuwa ikifanya kwa kulenga bidhaa hiyo kuirejesha kiwandani.
Hofu ya usalama ni tukio la karibuni kabisa kuikumba sifa ya kampuni hiyo nchini China.
Aprili mwaka huu, Apple iliwaomba radhi watumiaji wa China na kubadilisha sera za waranti ya iPhone, kufuatia shutuma za huduma zake baada ya mauzo.
Miaka miwili iliyopita hali katika baadhi ya viwanda vya kutengeneza bidhaa za Apple ilishutumiwa kwa mlolongo wa matukio ya wafanyakazi kujiua.
Kaka wa Ma, Yuelin, alilieleza Apple Daily kwamba familia inaamini dada huyo alikufa kutokana na mshituko wa umeme wakati akipokea simu na kwamba simu hiyo na vifaa vyake vilikabidhiwa kwa mamlaka za China.
No comments:
Post a Comment