MWILI WA BIBI HARUSI WAKUTWA UKINING'INIA NYUMBANI KWAKE...

KUSHOTO: Simone akiwa na mumewe, Mohammed Jabakhanji siku ya harusi yao. KULIA: Simone Jabakhanji
Bi harusi ambaye alitania kuhusu mume wake mpya 'alimvunja miguu yake' amekutwa amekufa nyumbani kwao baada ya kugundua alikuwa mgumba.

Simone Jabakhanji, mwenye miaka 27, kutoka Leyland huko Lancashire amekuwa akigombana na mumewe mfanyabiashara, Mohammed, miaka 29, baada ya kuwa amepewa taarifa za kupagawisha na madaktari, jopo linalochunguza kifo chake limeelezwa.
 Siku kadhaa kuelekea kifo chake mwanamke huyo alimweleza mama yake nchini Uingereza kwamba alikuwa akitishwa na mumewe na alihitaji kumpatia 'sehemu tulivu.'
Lakini alikutwa akining'inia nyumbani kwao katika mji mkuu wa Banjul katika nchi hiyo ya Afrika Magharibi, Agosti 13, 2011.
Mwaka mmoja kabla Simone alifunga ndoa na Mohammed Jabakhanji katika sherehe iliyofanyika kwenye ufukwe mmoja wa nchini Gambia iliyohudhuriwa na familia yake akiwamo kaka yake, Paul Lally na mama Janice Lally.
Wawili hao walikutana wakati wa mapumziko ya familia na ingawa familia ya Simone mwanzoni ilikuwa na makazi, mwanamke huyo akahamia Gambia kuwa na mumewe mtarajiwa mwaka 2009 na kufunga ndoa mwaka uliofuata katika Siku ya Wapendanao mwaka 2010.
Katika uchunguzi wa awali wa kifo chake Mohammed alikamatwa na Polisi wa Gambia kwa mauaji ya mwanamke huyo lakini baadaye akaachiwa.
Katika mashitaka mjini Preston, Ofisa wa Uchunguzi wa Vifo, Simon Jones alisema hakukuwa na ushirikiano kutoka kwa mamlaka za Gambia katika uchunguzi wao na kwamba haiwezekani kusema moja kwa moja kwamba kifo chake ni cha kujiua.
Alisema kumekuwa na maombi ya kujirudia kupitia Interpol, Wizara ya Mambo ya Nje na Balozi wa Gambia, lakini ni taarifa chache tu zilizoweza kupatikana.
Pia aliongeza kwamba hakuna uchunguzi uliofanyika nchini Gambia na mwili wa Simone ulitiwa dawa ili usioze kabla ya kurejeshwa nchini Uingereza, kukiwa na uwezekanao kabisa wa kuondoa alama za uzima zinazozingira kifo chake.
Jones alisema: "Kumekuwa na taarifa kidogo mno kuhusu mambo yaliyozunguka, aligungulika akiwa kaning'inia nyumbani kwake. Hakuna ishara zozote za jinsi Simone alivyofika pale.
"Pale kifo kama hiki kinapotokea katika nchi hii hupata taarifa za polisi, picha za eneo la tukio.
"Wakati tunaposhughulikia vifo vinavyotokea nje ya Uingereza na Wales kwa ujuma tunazitegemea mamlaka husika katika nchi hiyo kutupatia taarifa.
"Kama Ofisa Uchunguzi wa Vifo sina nguvu ya kutaka mashahidi ambao wanaishi nje ya nchi kuja kwenye kesi."

No comments: