MWALIMU ALIYEMWAGIWA TINDIKALI ZANZIBAR ARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALINI...

Kirstie Trup (kushoto) ameruhusiwa kutoka hospitalini hapo (pichani).
Mmoja wa wasichana waliomwagiwa tindikali katika kisiwa cha Zanzibar ameruhusiwa kutoka hospitalini juzi usiku.

Kirstie Trup, mwenye miaka 18, ambaye alimwagiwa tindikali hiyo sambamba na rafiki yake Katie Gee, pia miaka 18, katika shambulio la kutisha wiki iliyopita, atarejea kwenye Hospitali wa Chelsea and Wesminster Alhamisi wiki hii kufanyiwa upandikiziwaji ngozi, mama yake Rochelle alisema.
Katie, ambaye alisemekana kuungua kwa asilimia 80 ya mkono wake wa kulia na asilimia 50 ya kiwiliwili chake, amebaki hospitalini hapo ambako alitarajiwa kufanyiwa upasuaji.
Mama Trup, mwenye miaka 49, alisema: "Ninathibitisha kwamba Kirstie ameruhusiwa kwa muda hadi Alhamisi atakaporejea kwa ajili ya kupandikiziwa ngozi. Hatutazungumzia chochote kuhusiana na Katie."
Mama wa Katie, Nicky Gee alikataa kuzungumzia kuhusu matibabu ya binti yake kwa kile alichoelezea kama ni 'wakati nyeti mno'.
Hospitali hiyo imekataa kuzungumzia kuhusiana na hali za wasichana hao jana.
Ndugu wa familia za wasichana hao wameendelea kusimama kando ya vitanda kwenye hospitali hiyo, ambako hali za waathirika hao zimeelezekwa kwamba 'zimeimarika'.
Polisi mjini Zanzibar imewakamata watuhumiwa wawili na kuwahoji wengine sita ambao inaamini wana 'taarifa muhimu'.
Mhubiri mwenye msimamo mkali Shekhe Ponda Issa Ponda anafahamika kuwa yuko chini ya ulinzi mkali wa askari wenye silaha hospitalini baada ya kuwa amejeruhiwa wakati akijaribu kuwatoroka polisi.
Anasemekana kuwa alipigwa risasi begani wakati akijaribu kutoroka mjini Morogoro, maili 200 kutoka Dar es Salaam.
Imedaiwa kwamba Shekhe Ponda alijisalimisha mwenye kwa polisi baada ya kujeruhiwa kufuatia shambulio hilo dhidi ya walimu hao wa kujitolea.
Anadaiwa kuwa na uhusiano na kundi la Uamsho, kundi la Waislamu wenye msimamo mkali ambalo polisi inahisi linaweza kuwa limehusika katika shambulio hilo.
Mashambulio ya tindikali yamekuwa sifa ya kundi hilo ambalo linataka Zanziba iwe nchi huru kutoka Tanzania na sheria ya Sharia itumike kisiwani humo.
Kiongozi huyo wa juu alitembelea Zanzibar katika wiki ya mashambulio dhidi ya wasichana hao wa Uingereza na alionekana akihamasisha wafuasi wake kupinga dhidi 'ukoloni' kutoka kwa Wakristo na kuwataka vijana wa Kiislamu kufanya vurugu.
Katie na Kirstie walisafirishwa kutoka Tanzania kwa kutumia ndege maalumu ya wagonjwa na haraka wakapelekwa kwenye taasisi maalumu kwa ajili ya kushughulikia vidonda vya moto Ijumaa iliyopita.

No comments: