Chatu huyo anaaminika amekuwa akirandaranda kwenye mitaa ya mjini Portsmouth. |
Nyoka aina ya chatu anazagaa katikati ya jiji baada ya kuwa ametupwa kwenye uzio wa miti iliyooteshwa pale dereva taksi alipokataa kuruhusu nyoka huyo kuingizwa kwenye gari lake.
Inafahamika mwanaume mmoja alikuwa na nyoka huyo aliyemviringa kwenye shingo yake wakati akipanda kwenye taksi hiyo, lakini dereva huyo alisema hawezi kuruhusu nyoka huko kuingizwa ndani.
Abiria huyo ndipo akamtupia nyoka huyo kwenye uzio wa miti iliyooteshwa na sasa polisi na askari wa zimamoto wanamsaka nyoka huyo kwenye maeneo ya Hants, mjini Portsmouth.
Kutofahamika alipo nyoka huyo kumeibua hofu katika jiji hilo huku ikitokea siku mbili tu baada ya watoto wawili kuuawa na chatu nchini Canada.
Connor, mwenye miaka sita, na Noah Barthe, mwenye miaka minne, walikuwa wamelala kwenye ghorofa ambako rafiki yao alikuwa akiishi juu ya duka la wanyama wa kufugwa.
Chatu huyo mwenye urefu wa futi 14 alitoroka kutoka kwenye duka hilo na kuwanyonga wavulana hao hadi kufa.
Msemaji wa Hampshire Constabulary alisema: "Polisi walikwenda eneo hilo mjini Portsmouth kufuatia taarifa za kutoweka kwa chatu mmoja.
"Inaaminika nyoka huyo pengine yuko kwenye uzio wa miti iliyopandwa eneo la jirani.
"Askari wa Zimamoto na vikosi vya uoakoaji pia walikwenda eneo la tukio.
"Kamera maalumu pia zilitumika kujaribu kumsaka nyoka huyo."
Elizabeth Oakshott anaishi kwenye mtaa huo huko Milton, Portsmouth, ambako nyoka huyo alionekana kwa mara ya mwisho Alhamisi.
Bibi huyo mwenye miaka 75 alisema: "Jirani yangu ana mbwa watatu na wamekuwa wakienda kwenye kichaka hicho maeneo ya upande wa bustani hiyo, lakini pale mtu anapotoka kwenda kutazama, hawaoni chochote.
"Polisi walikwenda kwenye uzio huo wakiwa na fimbo na kuvuta baadhi ya matawi."
Steve McGovern, ambaye hufanya kazi katika Kundi la Upimaji Ardhi, ambalo hutunza viwanja kuzunguka eneo la jirani la mabweni ya wanafunzi, alisema mtu mmoja inafahamika kuwa alimtupa nyoka huyo
Alisema: "Tuliambiwa mwanaume mmoja ambaye alichukuliwa na taksi moja na alikuwa na nyoka ambaye alimzungusha shingoni mwake.
Dereva taksi huyo alisema: "Haiwezekani kupanda na nyoka wako kwenye gari langu" hivyo akamtupia kwenye uzio huo ili aweze kupanda kwenye taksi hiyo.
"Kisha akamchukua mwanaume huyo na kumpeleka alikokuwa akienda."
Nyoka huyo ni jamii ya Boidae, ambayo kwa ajili hupatikana huko Kaskazini, Katikati na Kusini mwa Amerika.
Kwa kawaida hula aina mbalimbali za mamalia wenye ukubwa wa kuanzia wadogo hadi ukubwa wa wastani na ndege na anaweza kufikia urefu wa takribani futi 14.
No comments:
Post a Comment