Tuesday, July 2, 2013

SAA ZA MWISHO ZA RAIS OBAMA DAR ES SALAAM KABLA YA KUONDOKA...

Rais Barack Obama akifurahia ngoma kutoka kwa moja vikundi vya utamaduni vilivyokuwa vikitumbuiza kwenye Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam muda mfupi uliopita kabla ya kurejea mjini Washington. Kushoto ni mwenyeji wake, Rais Jakaya Kikwete.
Rais Barack Obama akionesha uwezo wake wa kuchezea mpira maalum wakati alipotembelea mitambo ya kuzalisha umeme iliyoko Ubungo, Dar es Salaam leo asubuhi.
Rais Barack Obama akisalimiana leo asubuhi na walionusurika pamoja na ndugu wa marehemu waliokufa kwenye mlipuko wa bomu katika Ubalozi wa Marekani mjini Dar es Salaam.
Rais wa 43 wa Marekani, George W. Bush (kushoto) na Rais wa 44 wa nchi hiyo, Barack Obama wakiinamisha vichwa vyao mapema leo, kuwakumbuka watu 11 waliofariki kutokana na shambulio la bomu kwenye Ubalozi wa Marekani mwaka 1998.

No comments: