Friday, June 14, 2013

SISTA WA MUDA MREFU ZAIDI DUNIANI AFARIKI AKIWA NA MIAKA 105...

Sista Teresita Barajue.
Mwanamke anayeaminika kuwa sista aliyefanya kazi hiyo kwa muda mrefu zaidi duniani ambaye alitumia miaka 86 akiishi kwenye jumba la masista amefariki dunia nchini Hispania akiwa na umri wa miaka 105.
Sista Teresita Barajuen alifariki juzi usiku kwa mujibu wa Sista Maria Romero, mkuu wa jumba la Shirika la Masista wa Buenafuente lililoko nje ya jiji la Madrid.
Aliingia katika jumba hilo la masista wakati alipokuwa na miaka 19, kwa mujibu wa mkuu huyo.
Sista Teresita alikiri kwenye mahojiano kwamba kama ilivyo kwa wanawake wengi vijana wakati huo, hakuwahi kufikiria kuwa sista lakini aliingia kwenye jumba hilo sababu ya shinikizo kutoka kwa familia yake.
Mwaka 2011 alitoka kwenye jumba hilo kwa mara ya kwanza katika miaka 40 kwenda kuonana na Baba Mtakatifu ambaye sasa amestaafu, Benedict XVI wakati wa ziara yake ya kipapa mjini Madrid.
Aliingia kwenye jumba hilo siku sawa na tarehe yake ya kuzaliwa.

No comments: