Friday, June 14, 2013

PAPA FRANCIS AKIRI KUWAPO VITENDO VYA USHOGA NDANI YA VATICAN...

Papa Francis akiwasili katika mkutano huo.
Papa Francis amekiri uwepo wa 'vitendo vya ushoga' ndani ya utawala wa siri wa Vatican kwa mara ya kwanza.
Akizungumza mbele ya hadhara na Wakatoliki wa Amerika ya Kusini, Baba Mtakatifu huyo kutoka Argentina alisema kwamba kulikuwa na 'mtandao wa rushwa' ndani ya Curia ya Roma - bodi inayosimamia Kanisa Katoliki.
Pia alikiri uwepo wa tetesi za muda mrefu kuhusu 'ushoga' ndani ya Curia hiyo, na kugusia kwamba lazima atachukua hatua kuhusiana na suala hilo.
Akizungumza kwa kutumia lugha yake ya asili ya Kihispaniola Alhamisi iliyopita, Papa huyo mwenye miaka 76 aliueleza CLAR (the Latin American and Caribbean Confederation of Religious Men and Women): "Kwenye Curia, hakika kuna baadhi ya watakatifu, lakini pia kuna mtandao wa rushwa.
"Kunazungumziwa uwepo wa 'vitendo vya ushoga' na ni kweli, vipo," alisema, katika ripoti iliyowekwa kwenye tovuti moja ya Chile. "Tutaangalia tunachoweza kufanya."
Papa huyo kutokamArgentina anadhamiria kuunda upya Curia hiyo ya Roma - utawala wa Kanisa Katoliki unaoshutumiwa vikali - nguzo kuu ya upapa wake, lakini alisema itakuwa 'vigumu'.
"Siwezi kufanya mabadiliko mwenyewe," alisema, akafafanua 'hakuwa amejipanga vizuri.'
Kwa sababu hiyo, jukumu hilo litashughulikiwa na kamisheni ya makardinali wanane kutoka duniani kote ambao Papa Francis aliwachagua mwezi Aprili kumsaidia kusimamia Kanisa Katoliki.
Wamepanga kukutana kwa mara ya kwanza mwezi Oktoba.
Wakati Papa aliyepita, Benedict XVI, alipotangaza uamuzi wake wa kustaafu, wengi walihisi kazi tetesi za uwepo wa vitendo vya ushoga katika roho ya Curia.

No comments: