![]() |
Dk John Sentamu. |
Askofu wa York ameamuru uchunguzi binafsi kuhusiana na madai dhidi ya aliyekuwa Paroko wa Kanisa Kuu la Dayosisi.
Dk John Sentamu alisema Kanisa hilo la England linachukulia madai ya udhalilishaji watoto 'kwa uzito wa hali ya juu'.
Taarifa yake imekuja baada ya mtangulizi wake, Lord Hope wa Thornes, kukataa mapendekezo aliyofunikia madai dhidi ya Robert Waddington, Paroko wa zamani wa Kanisa Kuu la Dayosisi Manchester, ambaye alifariki kwa saratani miaka mitano iliyopita.
Lord Hope, ambaye alikuwa Askofu wa York kati ya mwaka 1995 na 2005, alitaarifiwa mara mbili kuhusu madai shisi ya Waddington, ambaye alisemekana kuwa alimdhalilisha mtumikiaji Eli Ward mjini Manchester katika miaka ya 1980 na mwanafunzi wa kiume nchini Australia.
Eli Ward alisema kwanza alichukuliwa peke yake na Paroko huyo wa Manchester, Padri Robert Waddington, katika umri wa miaka 11 na kisha baadaye kuwa mwenzi wake wa karibu kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano.
Madai hayo yalitolewa hadharani na Ward kwa mara ya kwanza wiki hii na kupelekea mapendekezo ya kufunika wajibu wa Kanisa hilo kufuatia madai yaliyowasilishwa kwa maaskofu mwaka 2003.
Lakini Askofu huyo wa zamani wa York, Lord Hope wa Thornes, ambaye wakati huo alikuwa akisimamia Dayosisi ya Manchester, alisema hakuwaeleza polisi na huduma za jamii sababu sheria za Kanisa wakati huo hazikuagiza hivyo na sababu Paroko huyo alikuwa akikaribia kufa kwa saratani.
Ward, ambaye sasa ana miaka 40, alisema alikuwa akilala kwenye kitanda cha Paroko huyo wakati alipokuwa na miaka 13 na hadi katikati ya miaka kumi na kitu alikuwa akitumia takribani kila wikiendi na usiku katika nyumba ya padri huyo. Alikwenda naye mapumzikoni huko Cornwall, Lake District, Paris na Kusini mwa Ufaransa.
Ushalilishaji huo ulianza pale Waddington alipoanza mchakato wa mambo ya kikubwa mwaka 1984 na kukoma baada ya hisia kuwa zimeibuka katika Dayosisi ya Manchester mwaka 1989, Ward alieleza. Mwaka 2004, Paroko Waddington, ambaye wakati huo alikuwa amestaafu, alikuwa amevuliwa madaraka kuongoza huduma za Kanisa na Lord Hope lakini hakuna taarifa zilizofikishwa polisi au huduma za jamii. Paroko huyo alifariki mwaka 2007.
Juzi Lord Hope alisema katika taarifa: "Katika kipindi chote kama askofu kila mara nilishikilia kwenye kushika sheria halali za Kanisa la England kuhusiana na kinga."
Alisema Sera ya Kanisa hilo la England ya mwaka 1999 juu ya Ulinzi wa Watoto, ambayo ilikuwa ikitumika wakati huo lakini ambayo ilikuwa ikiangaliwa upya, ilieleza kwamba hakuna matakwa ya moja kwa moja kisheria kwa Kanisa kupeleka madai yahusuyo watu wazima polisi au huduma za jamii.
Lakini alisema sera hiyo inaeleza ni muhimu kutilia uzito endapo watoto wanaweza kuwa bado kwenye hatari kutoka kwa mtuhumiwa huyo wa udhalilishaji na, kama hivyo, kutaarifu suala hilo kwa polisi au huduma za jamii.
1 comment:
No recommendations are made, each agency has a unique road network.
Arianna is a remarkable person and she will continue to be punctuated by episodes of severe financial volatility
that would erode government's ability to repay debt. We provide best rates in the market. 5% increase from Russia and Eastern Europe.
Feel free to visit my blog paphos Car rental review
Post a Comment