![]() |
| Papa Benedict XVI. |
Imebainika kwamba licha ya kustaafu kwa Papa, Kiongozi huyo bado ataendelea kupokea kitita kinono kwa maisha yake yote.
Wakati Papa Benedict XVI akijiuzulu juzi, mafao yake ya kustaafu - ambayo ni ya kwanza kuandaliwa na Vatican tangu miaka 600 iliyopita – bila shaka yatakuwa mazuri kama anayopata raia mzee wa Marekani, hasa kwa kuzingatia kuwa ni mapato ya uhakika na marupurupu mazuri.
Papa huyo mstaafu atakuwa akipata pensheni ya euro 2,500 (Sh milioni 5.3) kwa mwezi, kwa mujibu wa gazeti la Italia, La Stampa. Hiyo ni sawa na malipo ya pensheni anayostahili kulipwa Mmarekani atakayestaafu mwaka huu.
Ni watu wachache ambao watastahili kupata kiwango hicho cha malipo. Kwa wanaoanza watatakiwa kusubiri hadi umri wa miaka 70 ya kustaafu. Watatakiwa pia kutumia muda wao mwingi wa maisha yao ya kikazi kupata mafao hayo ambayo yatakatwa kodi, ambayo ni sawa na dola 113,700 za Marekani mwaka huu.
Papa huyo mstaafu hatakuwa na sababu ya kuhofia maisha. Kanisa Katoliki litagharimia matumizi yake, atapewa nyumba nzuri ndani ya Vatican na kumlipia chakula na wahudumu wa ndani, kwa mujibu wa gazeti la Telegraph.
Huduma kama hiyo haiwezi kutolewa kwa mzee wa kimarekani isipokuwa tu kama atakuwa anaishi katika makazi ya wasio na uwezo.
Juzi usiku Papa Benedict XVI alijiuzulu rasmi akisema sasa “atakuwa hujaji” anayeanza safari yake ya mwisho duniani.
Papa huyo mwenye umri wa miaka 85, jana aliruka kwa helikopta kutoka Vatican hadi kwenye kasri la Gandolfo, karibu na Roma ambako atapumzika.
Baraza la Makadinali, likiongozwa na Kadinali Tarcisio Bertone, ndilo sasa linaongoza Wakatoliki bilioni 1.2 duniani hadi papa mpya atakapopatikana. Papa Benedict alishatangaza utiifu wake wa dhati kwa papa mpya bila kujali anatoka nchi gani.
Kwa kawaida, mapapa huondoka Vatican wakiwa kwenye majeneza na – baada ya kipindi cha mombolezo- hupumzishwa katika makaburi ndani ya Kanisa la Mtakatifu Peter, huku kengele kuu ndani ya Kanisa hilo la kwanza la kikristo zikirindima. Lakini haikuwa hivyo kwa Papa Benedict XVI.
Utawala wake wa karibu miaka minane ya upapa, umemalizika si kwa kifo, lakini kwa kujiuzulu kwa aina yake. Kengele zilipigwa kwa muda mfupi wakati Papa huyo mstaafu akiwa na mkongojo wake mweusi – akiondoka Vatican kwa mara ya mwisho akitumia helikopta nyeupe ya Jeshi la Italia.
Iliruka angani jioni hiyo yenye ubaridi ikitoka katika kiwanja chake maalumu kilichoko kwenye kona ya bustani za Vatican. Baada ya kuzunguka kama mara mbili angani mwa Jiji la Vatican, marubani waliielekeza iliko kasri ya Gandolfo kwenye vilima vya Alban.
Baada ya safari hiyo ya dakika 15 ilitua na Benedict kushuka na kulakiwa na umati wa watu wa eneo hilo waliomshangilia na kumwombea huku naye akiwatakia usiku mwema na kuingia ndani.
Ilipotimia saa 2 usiku saa za Italia, milango ya makazi yake ilifungwa. Walinzi wa kiswisi waliokuwa wakimlinda wakawa wamemaliza kazi na kuondoka. “Nafasi ya kazi ya upapa” sasa ikawa imetangazwa rasmi kuwa wazi.

No comments:
Post a Comment