Friday, March 1, 2013

KINARA WA WIZI MKUBWA WA TRENI KATIKA HISTORIA YA UINGEREZA AFARIKI DUNIA...

KUSHOTO: Treni hilo muda mfupi baada ya kutokea wizi huo. KULIA: Bruce Reymolds alivyokuwa siku chache kabla ya kifo chake.
Bruce Reynolds, kinara ambaye aliratibu Wizi Mkubwa wa Treni mwaka 1963, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 81.
Baada ya kuendesha mpango wenye thamani ya Pauni za Uingereza Milioni 2.6, ambao ulikuwa wizi mkubwa kwa wakati huo katika historia ya Uingereza, Reynolds alitumia miaka mitano mafichoni kabla ya kufungwa kwa miaka tisa.
Polisi mmoja ambaye anachunguza uhalifu huo alisema kwamba kifo cha Reynolds miezi kadhaa mbele baada ya sherehe yake ya kutimiza miaka 50 'ilihitimisha zama zake.'
Kifo hicho kilitangazwa na mtoto wa kiume wa Reynolds, Nick, ambaye ni mmoja wa wanamuziki wanaounda bendi ya Alabama Three.
Mhalifu huyo mkongwe aliandika kitabu cha kumbukumbu, The Autobiography of a Thief (Wasifu wa Mwizi), ambacho kilijipambanua kama moja ya vitabu vilivyokuwa vikielimisha mno uhalifu halisia kuwahi kuchapishwa.
Wizi Mkubwa wa Treni ulifanyika katika masaa ya mapema ya Agosti 8, 1963 katika daraja la reli mjini Buckinghamshire.
Reynolds na wenzake 16 walipanga mpango huo ambapo wangevamia treni ya Royal Mail iliyokuwa ikisafirisha Pauni za Uingereza milioni 2.6 - sawa na zaidi ya Pauni za Uingereza milioni 40 kwa sasa.
Walishambulia wafanyakazi waliokuwamo ndani na kutokomea na pesa hizo, huku wakikata nyaya za simu zilizokuwa jirani ili waathirika wasiweze kupiga simu kuomba msaada.
Jack Mills, dereva wa treni hilo, alitupwa nje kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kuachwa akisumbuliwa na maumivu makali ya kichwa kwa maisha yake yote yaliyobaki.
Reynolds alikimbia nchini humo katika jaribio la kukwepa mkono wa sheria, na kuishi nchini Mexico na kisha Canada akitumia jina la uongo pamoja na familia yake.
Lakini aliporejea Uingereza alikamatwa na kufunguliwa mashitaka, kisha kuhukumiwa kifungo cha miaka 25 jela kwa ushiriki wake katika wizi huo.
Mpangaji huyo wa uhalifu aliachiwa mwaka 1978 na kwa kiasi kikubwa alijificha asionekane hadharani.
Reynolds alisambaza kitabu chake cha kumbukumbu mwaka 1995, akielezea jinsi alivyoachana na ndoto zake za kuwa mwandishi wa habari na kuhamia kwenye uhalifu.
Katika miaka yake ya baadaye aliishi huko Croydon, Surrey, na kusumbuliwa na kuzorota kwa afya yake kabla ya kifo chake.
Nick Reynolds alisema: "Nathibitisha kwamba amefariki na alikufa akiwa usingizini.
"Hakuwa mzima kwa siku chache na nilikuwa nikimuuguza."
Eddie Richardson, rafiki wa siku nyingi wa Reynolds ambaye alitumikia kifungo hicho pamoja naye gerezani, alisema alikuwa na huzuni kusikia kifo chake na kumwelezea kama 'mshirika mzuri'.
Richardson, ambaye alijitambulisha mwenyewe kama 'bosi wa genge la kusini mwa London', alisema: "Alikuwa sahihi wakati wote. Alikuwa ni mtu wake pekee. Alifanya vitu vyake mwenyewe. Kuna muungano mmoja umeachwa kwa sasa."
Akiwa ametumikia miaka 25 jela mwenyewe, Richardson amemkumbuka Reynolds kuwa rafiki mwema kwake katika kipindi chote gerezani.
"Alikuwa mtu mzuri mno," alisema. "Alikuwa mshirika safi, mtu mwenye uzoefu, alikuwa na machache ya kusema. "Ninahuzuni kusikia taarifa hizo, na hakika ni aibu."

No comments: