WAOMBOLEZA KIFO CHA MAMBA MKUBWA ZAIDI DUNIANI...

Wananchi wakipiga picha mbele ya mwili wa mamba mkubwa zaidi duniani.
Mji mzima ulikuwa katika maombolezo jana baada ya Lolong, mamba mkubwa kabisa duniani kufa katika Ziwa lake la kujengwa kutokana na kuumwa ghafla.
Mamba huyo majichumvi mwenye urefu wa futi 21 na uzito wa tani moja, ambaye alikamatwa miezi chini ya 18 iliyopita na timu ya wanaume majasiri kusini mwa Philippines, alikutwa akiwa amelala chali katika eneo lake kwenye hifadhi ya biashara ya utalii.
Lolong, anaaminika kuwa na zaidi ya miaka 50, aliana kuumwa baada ya kumeza mfuko wa plastiki takribani wiki tatu zilizopita. Baada ya hapo akabaki akiharisha mfululizo, limeripoti gazeti la The Philippine Star.
Lolong, amepewa jina hilo na mwindaji maarufu wa Philippines, amekuwa akilaumiwa kwa vifo vya vya wavuvi kadhaa kabla ya kukamatwa kiaina kwenye ziwa lenye matope karibu na mji wa Bunawan (wenye wakazi 35,000), maili 515 kusini mashariki mwa Manila.
Wanaume 30 walitumia wiki tatu kujaribu kumkamata mnyama huyo mkubwa kabla mwishowe kufanikiwa Septemba 2011 kwa kutumia mzoga wa nguruwe kama chambo na kutupa nyaya juu kuzunguka mwili wake.
Ilibidi litumike trekta kumvuta hadi kwenye trela - lakini hapo kabla umati mkubwa wa watu ulimzingira kwa ajili ya kupiga picha na mamba huyo aliyevunja rekodi.
Tangu hapo, Lolong amekuwa kivutio nyota kwenye hifanyi ya kitalii na madiwani wa mji wametangaza kwamba mji wao mdogo hatimaye umepata nafasi kwenye ramani ya dunia.
Lakini jana, wengi wa wakazi wa mji huo walikuwa wakilia baada ya kugundua kwamba Lolong amekufa ndani ya mwaka na nusu tangu kuhamishiwa kwenye makazi yake mapya.
"Hatufahamu kilichomtokea," alisema Meya Edwin Elorde aliyeshitushwa mno na kifo hicho, ambaye aliripotiwa kumshika mnyama huyo kabla hajafa.
"Nimetokea kumpenda mamba yule. Ameleta umaarufu na hazina kwenye mji wetu na, katika njia ndogo, kuelekea Philippines."
Elorde alisema kwamba baada ya kukamatwa kwa mamba huyo - ambaye alitawala vichwa vha habari kwenye vyombo mbalimbali vya habari duniani - hifadhi maalumu ya utalii wa kibiashara ilitengenezwa kumhifadhi.
Wakazi wa nchi hiyo na watalii wa nje wamefanya safari maalumu kwenye jamii hiyo inayofikika kwa shida kushuhudia kiumbe huyo wa ajabu.
"Tulikuwa tumepanga kujenga barabara maalumu kuelekea kwenye hifadhi hiyo sababu tumekuwa tukipata watalii wengi, lakini sasa sina hakika kama tutaendelea na mipango hiyo," alisema Meya huyo.
"Pengine  mipango itaendelea kama tutaweza kukamata mammba zaidi - kuna wengine wengi kuzunguka eneo hilo - lakini siwezi kusema kama wanaweza kufikia ukubwa kama wa Lolong.
Uchunguzi ulitarajiwa kufanyika jana kujua sababu za kifo chake.

No comments: