![]() |
| Abiria akipanda kwenye treni ya TAZARA. |
Treni inayofanya safari zake kati ya Pugu Mwakanga na Tazara, nusura ipate ajali baada ya kuparamia mawe yaliyokuwa yamepangwa relini.
Hali hiyo ilifanya abiria waliokuwa wanasafiri na treni hiyo kupata kiwewe kutokana na kishindo kikubwa kilichotokea baada ya treni kuparamia ‘mlima’ huo wa mawe.
Tukio hilo lililotokea wiki iliyopita saa 1:00 usiku wakati treni hiyo ilipokuwa inafanya safari yake ya pili kuelekea Pugu Mwakanga.
Tukio hilo limefanya uongozi wa Tazara, kuwatangazia abiria juu ya tukio hilo la hatari kuwa vitendo hivyo vya hujuma vikiendelea, vinaweza kufanya treni hiyo kusitisha safari zake.
“Ndugu abiria siku ya Alhamisi katikati ya kituo cha Majoe na Songosongo, abiria waliokuwa wanasafiri na sisi walipatwa na wasiwasi baada ya kusikia kishindo kikubwa.
Kishindo kile kilitokana na treni yetu kuvamia mawe yaliyokuwa yametegwa katikati ya reli, kitendo kile ni cha hatari kwani zisingekuwa juhudi za dereva treni ingeweza kuacha njia.
“Tukio kama lile linaweza kufanya treni kuacha njia na abiria wote kupoteza maisha, tunaomba abiria wetu kuwa walinzi wa njia ya reli,” alisikika mtangazaji akiwatangazia abiria waliosafiri na treni.
Mtangazaji huyo alizidi kueleza kuwa suala hilo, limetokana na watu wasiojulikana kutega mawe kwenye reli na akaeleza kuwa tayari wameshavijulisha vyombo vya Dola kufuatilia suala hilo.
Pia, aliwataka abiria kuripoti suala hilo katika ofisi za mitaa zinazopakana na reli ili kuwaelimisha wananchi wao hatari ya kuchezea reli.
Kamanda wa Polisi wa Tazara Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Rashid Seif alithibitisha kuwepo kwa tukio hilo.
Seif alisema matukio ya namna hiyo ni hatari kwa treni. Alisema ameshauriana na uongozi wa Tazara wataenda kufanya kikao na wakazi wa maeneo hayo ili suala hilo lisijitokeze tena.
“Ni kweli tukio hilo lipo japo wasaidizi wangu wanadai eti hayo mawe yalitegwa na watoto, lakini kwangu mimi nalichukulia kama ni tukio la uhalifu.
Maana wahusika hawajakamatwa hivyo hatujui kama ni watoto au ni watu wazima. Na kama ni watoto hatujui kama walitumwa au ni utundu wao, sisi ni lazima tuchukue hatua za kuzuia,” alisema.
Alisema hatua ya kuzuia ni kwenda eneo ambako kitendo hicho kilifanyika, kufanya kikao na wenyeji wa maeneo hayo ili wawe walinzi wa reli ili yasije kutokea madhara makubwa.

No comments:
Post a Comment