TJ Jackson hatoweza tena kuhudumia kama mzazi mbadala wa
watoto watatu wa Michael Jackson bila kupata fidia kiasi fulani, hivyo
Wasimamizi wa mali za Michael Jackson wanamtaka Jaji kumpatia TJ kiasi fulani
cha pesa kuwezesha 'jahazi hilo' kuendelea na safari.
Wasimamizi hao wamefungua madai hayo -- ambayo yanasema TJ
amekuwa akijitolea mno kwa Paris, Prince na Blanket tangu kifo cha Michael
Jackson. TJ -- ambaye sasa ni mlezi wa watoto hao akishirikiana na Katherine
Jackson -- anatumia masaa 40 kwa wiki akiwatunza watoto hao watatu.
Wasimamizi hao wanasema imekuwa vigumu mno kwa TJ -- ambaye
ameoa na kufanikiwa kupata watoto wake watatu. Ingawa amekuwa mlezi mshirika
tangu Julai, hajawahi kulipwa hata senti moja kutokana na huduma yake hiyo.
Wasimamizi hao wanamtaka jaji kuwaruhusu wamlipe
TJ Dola za Marekani 9,000 kwa mwezi (zaidi ya Shilingi milioni 14.6 za
Tanzania), kuanzia Julai mwaka jana. Waliongeza, kwa namna mwelekeo ulivyo
sasa, TJ hatoweza kuendelea, hivyo fidia ni muhimu sana.
No comments:
Post a Comment