Friday, February 1, 2013

BOTI YENYE ABIRIA YAZAMA BAHARINI NUNGWI...

Watu  32 wamenusurika kufa maji baada ya boti ya   Sun rise iliyokuwa ikitoka Pangani Tanga, kwenda Nungwi Unguja, kuzama katika mkondo wa Nungwi baada ya kuzidiwa na mawimbi makali.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Kamishna Msaidizi, Ahmada Abdalla Khamis, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kunusurika kwa watu hao baada ya kuokolewa na boti zilizotoka Nungwi.
Alisema boti hiyo ilikuwa katika safari zake za kawaida kutoka Tanga kwenda Unguja na ilipofika katika eneo la mkondo wa Nungwi, ilikumbwa na kasi ya mawimbi na kuzama.
“Ni kweli tumepata taarifa ya kuzama kwa boti ikiwa na watu 32 na uchunguzi zaidi kujua chanzo cha ajali hiyo kwa sasa, unafanywa na Polisi,” alisema Kamanda.
Nahodha wa boti hiyo, Abdala Saleh alisema boti
hiyo ilipata ajali baada ya kupigwa na mawimbi ya bahari katika mkondo wa Nungwi ambao ni maarufu kwa kuwepo kwa maji yanayovutana.
Saleh alisema juhudi za kujaribu kuepukana na ajali hiyo zilishindikana, ambapo anashukuru msaada wa boti zilizotoka Nungwi pamoja na wavuvi waliokuwepo katika
maeneo ya jirani ambao walisaidia.
Kutokana na ajali hiyo, watu watatu wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Kaskazini Kivunge wakipata matibabu zaidi baada ya kunywa maji mengi.
Watu 22 walipata matibabu katika Hospitali ya Kivunge na kuruhusiwa kurudi nyumbani. ha kwa jina la Ali Juma.
Hivi karibuni Mamlaka ya Usalama wa Baharini Zanzibar na Mamlaka ya Hali ya Hewa, zilitoa tahadhari kuhusu kuwepo kwa upepo mkali ambapo wavuvi pamoja na wamiliki wa vyombo vya baharini, walitakiwa  kuchukuwa tahadhari.

No comments: