Mlevi mmoja alikuwa akinywa bia kwa fujo kwenye baa moja iliyoko ghorofani. Wakati akitaka kwenda msalani akapita dirishani badala ya mlangoni na kudondoka nje na kupoteza fahamu. Wakati wapitanjia wakiulizana kilichotokea, ghafla yule mlevi akainuka na kujibu: "Yani hapa ndio kwanza nafika sijui chochote!" Duh...
Thursday, February 28, 2013
WASOMI 200 WAJITOLEA KUAJIRIWA NA JKT...
Baadhi ya askari wa JKT wakiwa kwenye gwaride. |
Wasomi 200 waliojitolea kujiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) mwaka jana, ujasiri wao umezaa matunda mema.
Hali hiyo imetokana na kutambuliwa na Rais Jakaya Kikwete ambaye ameutaka uongozi wa Jeshi hilo kuwaajiri ili wasipotee na utaalamu wao baada ya kumaliza mkataba wa mafunzo.
Akizungumza katika makao makuu ya JKT, Dar es Salaam jana alipofanya ziara ya kikazi, Rais aliyeweka rekodi ya kuwa Rais wa kwanza kutembelea eneo hilo akiwa madarakani alisema, kujitolea kwa wasomi wenye Shahada na shahada za uzamili kushiriki mafunzo ya JKT ni heri, hivyo wasiachwe wakapotea.
“Matarajio yetu katika Operesheni Sensa yetu ya mwaka 2012 yalikuwa kupata watu wasio na elimu na walio na elimu ya kati, lakini cha kufurahisha ni kwamba hata wenye Shahada na Shahada za Uzamili nao walijitokeza kwa wingi na kumaliza vizuri mafunzo ya awali ya kijeshi kwa miezi sita. Hao 200 si haba.
“Nimekuwa nikipata ujumbe wao kwamba wamemaliza mafunzo ya awali na mwingine niliupata jana (juzi) wanauliza: ‘Sasa tumemaliza mtatuacha tu?’ Nimewajibu kwamba mimi si mwajiri, lakini kwa sababu mwajiri yupo hapa mkutanoni, ninawaletea suala hili, fanyeni utaratibu muwaajiri kulingana na fani zao watawafaa, hivyo msiache wakarejea nyumbani na kuwapoteza,” Rais alisema.
Akisisitiza hoja hiyo, alisema si lazima wote waajiriwe JKT bali hata kwenye maeneo mengine ya Jeshi nchini.
“Cha msingi JKT iangalie ni idadi gani inahitaji na wengine mwajiri ataangalia mahali pa kuwapangia kazi kulingana na uwezo wao wa kiutendaji na elimu. Mafunzo mengine yanaweza kufuata wakiwa ndani ya ajira,” Rais alisema.
Alifafanua, kuwa mkataba wa miaka miwili waliouingia na JKT kimafunzo, usiachwe ukaisha kwani kuwapata baada ya hapo inaweza kuwa kazi itakayoilazimu JKT kuwatafuta wengine kwa kuwalazimisha ili wajiunge na Jeshi hilo.
Wakati huo huo, Rais Kikwete aliwahakikishia Watanzania kuwa JKT itaanza rasmi Machi 4, ikiwa na lengo la kutimiza majukumu yaliyokuwa yakitimizwa na lililokuwapo kabla ya kufutwa mwaka 1994.
Hata hivyo, tofauti na matarajio, Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Raphael Muhuga alimweleza Rais kuwa uwezo wa kifedha uliopo ni mdogo kuhudumia watu wachache katika kambi zote nchini.
Kwa mujibu wa Muhuga, kinyume na ilivyokuwa katika JKT ya awali kwamba wahitimu wote wa kidato cha sita wanajiunga na JKT kwa lazima, kati ya 41, 000 waliomaliza kidato hicho mwaka huu, ni 5,000 tu ndio watajiunga kwa lazima huku 5,000 wengine wakitoka katika kundi la hiyari la vijana na wabunge 47 watakaokuwa kambini kwa wiki tatu.
“Hali ya majengo yetu si nzuri na uwezo wa kuhudumia watu wengi hatuna kwa sasa, kutokana na hilo, idadi ya wanaopaswa kuingia JKT kwa hiyari na kwa kujitolea inatuzidi uwezo,” alisema na kuongeza kuwa wamelazimika kutumia vigezo vilivyotolewa na Wizara ya Elimu ili kuchagua wahitimu wa kidato cha sita watakaojiunga.
Baada ya kuelezwa kuhusu uzalishaji mdogo wa mbegu na mahindi, Rais alitoa mwito kwa viongozi wa JKT waingie ubia na raia au wawekezaji wenye utaalamu wa uzalishaji katika maeneo wasiyo na utaalamu nayo.
“Wapo raia wenye uwezo na utaalamu wa kilimo na ufugaji, watafuteni mwingie ubia ili mfanye uzalishaji wenye tija. Kuna maeneo hayahitaji kuendeshwa kijeshi bali kwa kuzingatia utaalamu, sasa itakuwa vizuri kama mtashirikisha wataalamu wawasaidie kuyaendesha kwa faida, mkitafuta wababaishaji mtaishia kushitakiana mahakamani na msipoangalia, mtajikuta mnashindwa,” aliasa.
Katika hatua nyingine Rais alielezwa kuwa shirika hilo limefanikiwa kukusanya Sh bilioni 16 kati ya Sh bilioni 58 linazodai kutoka kwa wateja waliokopeshwa matrekta, lakini Rais alitoa angalizo kwamba Serikali haitakuwa tayari kuona inapoteza fedha hizo, kwa kuwa haikulidhamini shirika hilo kwa lengo la kutoa msaada au ubani kama inavyofanya kwenye misiba.
“Ni lazima madeni yote yakusanywe, kwa sababu muda utafika wakati mkopeshaji kutoka India atatakiwa kulipwa Sh bilioni 40 zake, zilizobaki kwa wateja ni Sh bilioni 42, ambazo hatuko tayari kuzilipa kupitia jasho la walipa kodi. Waliochukua matrekta wakumbushwe ili walipe,” Rais alisema.
Kuhusu madeni ya mbegu bora ya Sh milioni 420 ambayo JKT inadai kampuni tatu akiwamo Wakala wa Mbegu wa Taifa, Rais alisema ‘atamvaa’ wakala huyo wa Serikali ili alipe na kwamba kampuni mbili binafsi; Tropical Seeds na Highlands Seeds, watapaswa kufuatiliwa na waliowakopesha.
Rais Kikwete aliitaka JKT ihakikishe uwepo wake katika uwanja unaotumiwa kwa mapigano Tarime kati ya Waanchari na Warenchoka unakuwa chachu ya amani na si uzalishaji pekee.
“Wale watu wakishachokozana huko wanabebana hadi kwenye uwanja ule na kuanzisha mapigano, wala hawagombei eneo hilo sasa ninyi mmepewa mlitumie kwa uzalishaji na ujenzi, hakikisheni uwepo wenu unamaliza mapigano hayo,” alisema.

PAPA AAGA RASMI WAKATOLIKI, MRITHI WAKE MWEZI UJAO...
![]() |
Papa Benedict XVI. |
Kiongozi Mkuu wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Benedict XVI ameaga rasmi na kukiri hadharani, kwamba alikabiliwa na ‘dhoruba kali’ wakati wa miaka yake minane ya uongozi wa Kanisa Katoliki, lakini akasema alikuwa akiongozwa na Mungu na kuhisi uwepo wake kila siku.
Papa huyo mwenye umri wa miaka 85, anastaafu rasmi leo – akiwa ni Papa wa kwanza kuachia madaraka tangu Papa Gregory XII aliyefanya hivyo mwaka 1415.
Maelfu ya mahujaji jana walikusanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Peter, Vatican kumsikiliza Papa. Mrithi wake atachaguliwa katika mkutano wa makadinali mwezi ujao.
Papa Benedict aliuambia umati uliokusanyika katika makazi yake, kwamba kwake upapa ulikuwa “mzigo mzito” lakini aliukubali kwa sababu alikuwa na uhakika kwamba Mungu atamwongoza.
Kuna wakati alihisi “kama Mtakatifu Peter na mitume wake katika Ziwa la Galilaya”, alisema, akirejea hadithi ya Biblia pale wanafunzi walipokuwa wakikabiliana na mawimbi mazito na Yesu Kristo akawatokea.
Kanisa hilo limegubikwa na kashfa za udhalilishaji wa kijinsia ukifanywa na baadhi ya mapadri na kuvuja kwa nyaraka za siri zikionesha kuwapo rushwa na mizozo ndani ya Vatican.
Hakujawahi kutokea Papa kuomba mabilioni ya Wakatoliki duniani kote wamwombee “na wafanye hivyo pia kwa Papa mpya”, kama Benedict XVI alivyofanya jijini Vatican jana.
Hakika jana Papa Benedict alionekana kusawajika – dhaifu, hata alipokuwa akitoa sala yake ya ufunguzi, huku akiwa amezungukwa na walinzi wa kiswisi ambao wataondolewa karibu naye leo jioni wakati atakapokuwa anauvua rasmi upapa.
Lakini uamuzi wake wa kujiuzulu unaacha nyuma changamoto kubwa za kipapa juu ya udhalilishaji wa kijinsia na kashfa za kifedha, ingawa wafuasi wake wanadai alifanya mengi kukabiliana nayo huku akikiri kuwapo kazi kubwa inayotakiwa kufanywa.
Papa aliwashukuru waumini wake kwa kuheshimu uamuzi wake wa kujiuzulu na kusema anafanya hivyo kwa ajili ya mema ya Kanisa.
“Nilichukua hatua hii (kujiuzulu) nikijua kabisa uzito wake na kwamba haikuwa kawaida, lakini kwa roho safi,” alisema katika hotuba yake.
Kutokana na tangazo lake hilo la kushitua, hivi sasa Kanisa limerekebisha sheria zake ili kuruhusu kuanza mchakato wa kupata mrithi wake.
Baraza la siri la makadinali linalomchagua Papa linaloanza vikao vyake katikati ya mwezi ujao, litakuwa limebakiza muda mfupi wa kupata Papa mpya atakayesimikwa katika kipindi hiki maalumu kuliko vingine katika kalenda ya kikatoliki, Wiki Takatifu, kuelekea Pasaka, ambayo inaanza Machi 24.
Habari zinasema leo Papa atasafiri kwa helikopta kwenda katika makazi yake ya wakati wa kiangazi ya kasri la Gandolfo umbali wa kilometa 24 Kusini Mashariki mwa Roma. Ataacha rasmi upapa saa 2 usiku.
“Kwa upande mmoja, nilihisi kwamba kwa kuwa uamuzi wake wa kuacha madaraka tayari umeshafahamika, Papa Benedict amefarijika,” alisema Mkuu wa Mkutano wa Maaskofu wa Ujerumani, Askofu Mkuu Robert Zollitsch.
“Lakini pia hivi sasa anahisi huruma ya watu kwake na hivyo atakuwa mwenye huzuni na hamu ya kurudi nyumbani.”
Jana alitarajiwa kutumia muda wake wa mwisho katika makazi yake ya Vatican akiagana na makadinali ambao wamekuwa wasaidizi wake wa karibu katika kipindi chote cha miaka minane ya upapa.
Nyaraka zake binafsi zitafungwa na itakapotimia saa 2 usiku leo, walinzi wake wa kiswisi watakaokuwa katika makazi yake ya Gandolfo wataondolewa na nafasi zao kuchukuliwa na polisi wa Vatican.
Hiyo ndiyo itakuwa ishara ya mwisho rasmi wa upapa wake na mwanzo wa kipindi cha mpito cha kumpata mrithi wake.
Kuanzia Machi 4, makadinali watakutana kujadili matatizo yanayolikabili Kanisa na kupanga tarehe ya kuanza uchaguzi wa siri, au Baraza la kumchagua Papa, ili kumpata mrithi wa Papa Benedict wa XVI.
Mrithi huyo atachaguliwa na makadinali 115 (wenye umri wa chini ya miaka 80) kwa njia ya sanduku la kura katika Kanisa dogo la Sistine, Vatican.
Zaidi ya theluthi mbili za kura ndizo zinahitajika kumchagua papa. Makadinali 67 waliteuliwa na Benedict XVI na waliosalia waliteuliwa na aliyemtangulia, Papa Yohanne Paul II.
Karibu nusu ya makadinali hao (60) wanatoka Ulaya – 21 ni Wataliano - na wengi walishafanya kazi katika chombo cha utawala cha Kanisa – Curia, jijini Vatican.

BOBBY BROWN AHUKUMIWA KIFUNGO JELA KWA ULEVI...
Bobby Brown amehukumiwa kifungo cha siku 55 jela kufuatia kukamatwa kwake hivi karibu akiendesha gari huku akiwa amelewa, imefahamika.
Bobby alikamatwa Oktoba mwaka jana baada ya polisi kumsimamisha mwimbaji huyo kutokana na uendeshaji wa hatari, na kunuka harufu ya pombe ndani ya gari yake.
Bobby alishitakiwa kwa makosa ya kuendesha huku akiwa amelewa na kutumia leseni iliyofungiwa wakati wa tukio hilo. (Leseni ya Bobby imefungiwa kufuatia makosa kama hayo siku za nyuma mwaka 2012. Bobby pia alishawahi kuhusika na kosa kama hilo mwaka 1996.)
Bobby hakutakiwa kujibu chochote jana. Alihukumiwa kifungo hicho jena pamoja na kuwekwa chini ya uangalizi maalumu kwa miaka minne. Pia ameamriwa kumaliza mpango wake wa miezi 18 wa tiba dhidi ya pombe. Hii ni mara ya tatu kwa Bobby kukamatwa kwa kuendesha gari huku akiwa amelewa.
Bobby ataanza kutumikia kifungo hicho ifikapo Machi 20, mwaka huu - na ameamriwa kuhudhuria mikutano ya 3 AA kwa wiki hadi wakati huo.

WALIOTEKA BINTI KIBAHA KUPANDISHWA KIZIMBANI...
Polisi mkoani Pwani imesema imekamilisha uchunguzi dhidi ya vijana watatu wanaotuhumiwa kumteka na kumbaka binti wa miaka 16 huku wakimfungia ndani bila ridhaa yake kwa miezi minne.
Pamoja na hayo, wanaharakati na wanasheria wametoa maoni yao kuhusu tukio hilo, ambapo pamoja na kulaani wahusika, pia wametaka taratibu za kisheria zifanyike haraka ili watuhumiwa wakibainika kuhusika wachukuliwe hatua kali.
Akizungumza na mwandishi jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Ulrich Matei, alisema kwa mujibu wa utaratibu wa sasa, polisi wanapokuwa na kesi lazima waiwasilishe kwanza Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ndipo ipangiwe tarehe ya kufikishwa mahakamani.
“Sisi tuko tayari, tumeshapeleka jalada kwa wanasheria, tunachosubiri ni tarehe ambayo watuhumiwa hawa watapandishwa kizimbani,” alisema Matei.
Alisema uchunguzi wa awali wa Polisi umebaini kuwa watuhumiwa hao; Faida Kazigwa, Isaka Kazigwa na Jovian Oswald wanatakiwa kujibu mashitaka ya kuteka na kubaka.
Mwanasheria wa kujitegemea, Rosalie Makalle alilielezea tukio hilo kama la kuteka na kubaka, ingawa aliahidi kufuatilia kwanza mkasa huo ili kutathmini sheria inasemaje.
Mkurugenzi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Valeria Msoka, alisema kitendo alichofanyiwa binti huyo ni unyama na kutaka vyombo vya sheria kuharakisha kesi hiyo na hukumu itolewe mapema.
“Unajua vitendo hivi vinakithiri sana siku hizi kwa kuwa kesi za aina hii zinapofika kwenye vyombo vya sheria huchukua muda mrefu hadi kupatiwa ufumbuzi, hivyo ni vema katika hili muda ukazingatiwa na iwapo wahusika watabainika kuwa na makosa wapewe adhabu kali ili iwe fundisho,” alisisitiza.
Vijana hao wanadaiwa kuwa Novemba 11 mwaka jana walimteka na kumweka kwenye mazingira magumu mwanafunzi wa kidato cha kwanza wa sekondari Pangani mkoani Pwani na kumbaka na kisha kumtoa mimba kwa kumkorogea majani ya chai na kumnywesha.
Hata hivyo, alifanikiwa kuepuka mateso hayo, pale vijana hao siku moja waliposahau kufunga mlango na yeye kupata upenyo na kutoroka na kuingia porini akiepuka kukutana na vijana hao lakini njiani akasaidiwa na mchoma mkaa kuwasiliana na babu yake na kurejea nyumbani.
Kabla ya hapo, binti huyo alikuwa akichungwa na mmoja wa vijana hao aliyekuwa na kisu, hivyo kumtia hofu na kushindwa kupiga kelele hata watu wakiwamo polisi, walipofika katika kibanda alimokuwa amefichwa kwa muda wote huo.
Babu wa binti huyo, Daudi Zakayo, alisema mjukuu wake alipotea Novemba 3 na walifanya juhudi zote za kumtafuta ikiwa ni pamoja na kuripoti Polisi lakini bila mafanikio.
“Binti huyu ninaishi naye lakini baba yake yuko Ruvu anafanya kazi huko, mama yake hayupo, nilipoona haonekani nilimtaarifu baba yake, Charles Daniel, ambaye alikuja na wote tukaanza kuzunguka mtaani kwa rafiki zake hadi Polisi bila mafanikio,” alisema.
Alisema kutokana na binti huyo kutoonekana kwa muda mrefu, baba yake alikwenda kwa waganga wa jadi na mmojawao kudai yuko maeneo hayo amefichwa kwenye mti, lakini hata mganga huyo alipofanya ‘mambo yake’ bado hakuonekana.

ALIYEONGOZA MATANGAZO YA PEPSI, FIRESTONE AUAWA NA PAPA...
Mshindi wa tuzo ya Mwongozaji filamu bora na Televisheni ameuawa kwa kushambuliwa na papa nje ya ufukwe wa New Zealand jana ... huku mamlaka zikienda na silaha za moto eneo la tukio na kujaribu kumkabili mnyama huyo.
Adam Strange, mwenye miaka 46 -- ambaye aliongoza matangazo yote ya biashara kimataifa kwa ajili ya kampuni kama Pepsi na Firestone -- alikuwa akiogelea kwenye ufukwe maarufu nchini New Zealand ndipo papa mweupe alipomvuta chini ya maji. Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo hilo, takribani papa wengine watatu walishiriki katika shambulio hilo.
Polisi wa eneo hilo walikwenda haraka eneo la tukio wakiwa ndani ya boti ndogo ... wakisaidiwa na helikopta. Polisi hao walifyatua risasi takribani mara 20 alipokuwa papa huyo, lakini walikuwa wamechelewa mno.
Papa mmoja aliripotiwa kuuawa katika shambulio hilo la bunduki ... na mwili wake -- wenye urefu wa futi 14 -- uliopolewa kwenye maji muda mfupi baadaye.
Na kwa Strange -- mamlaka zilifanikiwa kupata mwili wake baada ya shambulio hilo.
Strange hakuongoza matangazo ya biashara pekee -- pia alishinda Tuzo ya Filamu Bora Fupi katika Tamasha la Filamu la Berlin mwaka 2009.
Marehemu ameacha mke na mtoto mdogo mmoja.

Wednesday, February 27, 2013
BINTI ATEKWA, AFUNGIWA NDANI MIEZI MINNE NA KUTOLEWA MIMBA KIBAHA...
Si rahisi kuaminika, lakini imetokea wilayani Kibaha mkoani Pwani, ambako mwanafunzi wa kidato cha kwanza wa sekondari ya Pangani, akiwa na umri wa miaka 16 (jina linahifadhiwa), ametekwa nyara na vijana watatu na kufungiwa ndani kwa miezi minne.
Binti huyo, ambaye pia vijana hao walimtoa mimba wakitumia majani ya chai, katika eneo alilofichwa alijengewa mfano wa kaburi na kumlaza humo, huku juu yake wakiweka godoro na kutumia kama kitanda chao.
Akisimulia mkasa huo kwa mwandishi nyumbani kwao mjini hapa jana baada ya kufanikiwa kuwatoroka watekaji wake, binti huyo ambaye ni mkazi wa kijiji cha Kidimu wilayani hapa, alidai kutekwa na vijana hao Novemba 11, mwaka jana, saa tisa alasiri wakati akienda kanisani.
“Siku hiyo, babu ninayeishi naye alinihimiza nitangulie kanisani jioni, kwa kuwa alikuwa na shughuli anamalizia. Niliondoka mwenyewe, Kanisa letu liko mbali kidogo na nyumbani, njiani nilikutana na vijana hao watatu,” alisimulia binti huyo.
Alidai kuwa vijana hao walimsimamisha na kumsalimia, huku mmoja wao ambaye ni mkubwa, akimtaka waongozane hadi anakoishi (si mbali na eneo hilo) ili akamkabidhi mzigo wa mama yake mdogo (binti) ambaye anajulikana kwa jina la Martha.
“Kweli niliwaamini, kwa kuwa vijana wale nilikuwa nawaona mara kwa mara kijijini, ingawa mmoja wao alikuwa akijaribu kunipa vijizawadi nilikuwa nakataa, lakini siku waliponiambia wana mzigo wa mama mdogo sikuwa na sababu ya kukataa,” alisema.
Baada ya kufika eneo wanaloishi vijana hao aliowataja kwa majina ya Isaka, Faida na Jovian, walimkamata mkono na kumsukumia ndani, huku Faida ambaye alionekana kuwa mkubwa kuliko wenzake, akimwambia kuwa hayo ndiyo yatakuwa makazi yake kuanzia siku hiyo akiwa kama mkewe.
Mwandishi alishuhudia eneo la makazi ya vijana hao ambao waliwekwa hapo kama walinzi; nyumba ya chumba kimoja pembeni ndani ikiwa imepangwa matofali mfano wa kaburi, na juu yake kikipangwa miti kama chaga na godoro ambalo vijana hao walikuwa wakilipanga juu na kulala huku binti huyo akiwa uvunguni.
“Waliponikamata walitoa visu na kunitishia kuwa nikipiga kelele wataniua, wakanisukuma ndani na kuniingiza kwenye ‘kaburi’ hilo na kunilazimisha kulala huku juu wakiweka godoro, hata mtu akiingia ndani ya chumba hicho hawezi kujua kama mimi nimo,” alisema.
Alisema aliishi hivyo kwa muda huo wote, huku akila mlo mmoja kwa siku, kwani vijana hao, walikuwa wakiondoka nyumbani hapo alfajiri na kurejea saa saba usiku na kupika.
“Wakati mwingine wakirudi, Faida huwatoa wenzake nje na kubaki na mimi ndani, na kunilazimisha kuvua nguo na kunifanyia mchezo mchafu na kisha ananirudisha kwenye uvungu humo na wenzake kuingia kulala,” alisimulia.
Aidha, binti huyo, alidai kuwa kutokana na kuingiliwa kimwili mara kwa mara na kijana huyo, alipata ujauzito kwani alihisi baada ya kutapika na kupoteza siku zake, vijana wale walipogundua walihaha kutafuta dawa ya kutolea mimba, walichemsha majani ya chai na kumlazimisha kunywa.
“Baada ya kunywa chai hiyo nilikaa kwa saa tano hivi, nikaanza kupata maumivu makali tumboni na baadaye damu ilitoka kwa mabonge, wale vijana hawakunisaidia, zaidi ya kunitoa nguo zenye damu na kuchukua ule uchafu niliotoa na kuufukia nje,” alidai.
Aliendelea kudai kwamba kipindi chote hicho hakuwa na namna ya kutoroka, kwa kuwa waliweka mlinzi hadi aliposikia vijana hao wakigombania masuala mengine na mwenye eneo hilo ambaye aliwaitia polisi baada ya kutoelewana.
“Polisi walikuja pale, lakini nilishindwa kupiga kelele, kwa kuwa walinifungia kwenye chumba kile na Isaka ambaye alinishikia kisu wakati wenzake wamekimbia, polisi waliishia kuulizia walipoona wenyewe hawapo wakaondoka,” alieleza binti huyo.
Alidai kuwa Jumamosi iliyopita, vijana hao waliondoka kwenye chumba hicho alfajiri na mmoja wao akasahau kufunga mlango, ndipo akapata upenyo na kukimbilia porini ambako alikutana na msamaria mwema aliyemsaidia.
Binti huyo alidai kuwa mtu huyo mchoma mkaa alimsaidia kupitia porini hadi nyumbani kwao ili asikutane na vijana hao ambapo pia alimpigia simu babu yake na kwa kusaidiana na wakazi wa kijiji hicho na serikali za mitaa waliwasaka vijana hao na kuwakamata.
Babu wa binti huyo, Daudi Zakayo, alisema mjukuu wake huyo alipotea Novemba 3 na walifanya juhudi zote za kumtafuta ikiwa ni pamoja na kuripoti Polisi lakini bila mafanikio.
“Binti huyu ninaishi naye lakini baba yake yuko Ruvu anafanya kazi huko, mama yake hayupo, nilipoona haonekani nilimtaarifu baba yake, Charles Daniel, ambaye alikuja na wote tukaanza kuzunguka mtaani kwa rafiki zake hadi Polisi bila mafanikio,” alisema.
Alisema kutokana na binti huyo kutoonekana kwa muda mrefu, baba wa mtoto huyo alikwenda kwa waganga ambapo mmojawao alidai kuwa binti huyo yuko maeneo hayo amefichwa kwenye mti na mganga huyo kufanya mambo yake lakini hakuonekana.
“Nawashukuru wakazi wa eneo hili na Serikali ya Mtaa kwani baada ya kusikia mjukuu wangu amerudi walishirikiana nami na kumkamata kwanza Isaka, ambaye alikana kuhusika, lakini baada ya kucharazwa bakora, alitaja wenzake walipo, tuliwakamata na kuwapeleka kituo cha Polisi Tumbi,” alisema na kuongeza kuwa siku anamwona mjukuu wake, alimsahau kutokana na alivyochafuka na nywele zilivyomtimka.
Akizumgumzia tukio hilo kwa niaba ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Pwani, Ofisa Upelelezi wa Makosa ya Jinai wa Mkoa, Juma Yusuph, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kuwataja vijana wanaoshikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na utekaji huo kuwa ni Faida Kazigwa, Isaka Kazigwa na Jovian Oswald.
“Kwa sasa vijana hawa wako chini ya ulinzi wanahojiwa kuhusu tukio hilo na ikithibitika kuwa wana kesi ya kujibu watafikishwa mahakamani,” alisema.
Mwandishi alifika hadi shuleni kwa binti huyo ambapo mlezi wa kike wa wanafunzi shuleni hapo, Mwalimu Bahati Eliaza, alikiri kusikia kuwa binti huyo amekumbwa na mkasa huo na kusisitiza kuwa wanasubiri taarifa ya Polisi ili wajue hatua zaidi za kuchukua.
“Sheria zinasema wazi, mtoto asipofika shuleni kwa zaidi ya siku 90 lazima jina lake lipelekwe kwa Bodi ya Shule ambayo itamjadili, lakini Katibu Tawala wa Mkoa akiwasilisha taarifa za mtoto na sababu za kutofika kwake shuleni, ataendelea na masomo, vinginevyo jina lake hufutwa,” aliongeza Makamu Mkuu wa Shule hiyo, Peter Mihayo.

CHEKA TARATIBU...
Kibaka kaiba televisheni kwenye nyumba moja bila kujua kuna kichaa anaishi mle ndani. Baada ya kubeba ile televisheni na kuanza kutimua mbio, ghafla kibaka akashangaa anakimbizwa na mtu nyuma yake. Kila akiongeza spidi na yule mtu anaongeza, mwishowe akaamua kusimama na kuhoji kulikoni. Yule jamaa akajibu, "Duh, umesahau rimoti hii hapa!" Kasheshe...
WEZI WA MAJI DAR SASA WAFUNGA MOTA UVUNGUNI MWA KITANDA....
Mmoja wa wakazi wa Dar es Salaam akisubiria kupata huduma ya maji. |
Wizi uliokithiri wa maji umegundulika katika Jiji la Dar es Salaam baada ya kiasi kikubwa cha mota za kusukumia kimiminika hicho kukutwa zimefungwa ndani ya vyumba vya ‘wezi’ hao.
Hatua hiyo imetokana na operesheni maalumu iliyoendeshwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick akishirikiana na vyombo vya Dola kutokana na kilio cha muda mrefu cha wakazi wa Jiji hilo kutokana na ukosefu wa huduma hiyo katika maeneo mengi.
Operesheni hiyo iliyofanyika jana ikimshirikisha pia Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana katika maeneo ya Kagera, Tandale, Urafiki na Mkwajuni.
Mota zaidi ya 25 zilikamatwa sambamba na pampu ambapo katika nyumba moja kulikuwa na mota hizo katika vyumba vya kulala, huku kabati likitumika kuficha mlango wa kuingia bafuni sehemu ambayo mabomba mengine yamefungwa. Watuhumiwa wawili walikamatwa.
Katika eneo hilo la Tandale mtaa wa Mkunduge, nyumba moja ikiwa na kisima cha maji nje ilibainika ikiendelea na biashara ya maji kwa wananchi wa eneo hilo, huku mota zikiwa kwenye vyumba vya kulala zikinyonya maji.
Meta chache kutoka hapo kuna kisima halali cha maji ya Kampuni ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco) ambacho hakina maji kutokana na mota hizo kuyafyonza na kuuzia wananchi ndoo moja Sh 200 tofauti na bei halali ya Dawasco ya Sh 20.
Katika mtaa wa Kagera, nyumba ilikutwa na mota nane huku mabomba yakiwa yametawanywa katika baadhi ya nyumba za wananchi kutoa huduma hiyo huku mabomba ya Dawasco yakiwa yamekauka kutokana na mota hizo kutumika kufyonza maji kwenye mabomba hayo.
Aidha, katika eneo la Mkwajuni, mabomba ya inchi nane mali ya Dawasco yalitobolewa kwa ustadi mkubwa huku maji yakielekezwa upande wa wananchi kuwasambazia na kuuziwa kwa bei kubwa inayofanya wananchi kulalamika kila siku kutokana na huduma ya maji.
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kagera, Juma Jangilaga, alisema suala la mabomba ya maji ya Dawasco kukatwa na wezi ni tatizo la Kampuni hiyo kwani amekuwa akifuatilia na kuripoti hali hiyo lakini ufumbuzi haukupatikana.
Katika mtaa huo, takriban nyumba zaidi ya tano zinadaiwa kujiunganishia mabomba hayo kwa njia ya wizi huku wakiyatawanya kwa wengine kinyemela.
Akizungumzia operesheni hiyo, Sadiki alisema asilimia 30 ya maji yanayopotea kila siku kutokana na kuibwa Serikali kupoteza Sh bilioni mbili kila siku.
Kuhusu maeneo yaliyokamatwa na mota, aliiamuru Dawasco kukata huduma hiyo huku ikitafuta njia mbadala kuhakikishia wananchi wa maeneo hayo hawahangaiki kwa kukosa huduma.
Aliitaka Dawasco inunue maboza yatakayofikisha huduma ya maji kwa bei nafuu kwa wananchi ili kuwapunguzia ukali wa maisha.
Aliitaka pia kuingia mkataba na wauza maji wa maboza na kuwatambua kisha kuwasajili ili walipe kodi kwani ni wafanyabiashara kama wengine.
Alihimiza wafanyakazi Dawasco kujisafisha kwa kuwa kuiba maji na kuyaunganisha kwa wananchi inafanywa kwa utaalamu mkubwa, hivyo wajidhibiti.
Aligeukia wenyeviti wa serikali za mitaa akiwataka kutoa taarifa za wizi huo unaofanyika ili kwamba isijeeleweka, kuwa nao wanashiriki kuhujumu Serikali.
Mkurugenzi Mtendaji wa Dawasco, John Midala alisema wako kwenye mchakato wa kununua mita za maji kama za Luku kuanzia Aprili ambazo watumiaji watakuwa wakilipia kadri wanavyotumia.

Tuesday, February 26, 2013
MGOGORO WAOTA MIZIZI KANISA LA MORAVIAN...
Ujumbe wa Kanisa la Moravian Duniani (Unity Board), umesikitishwa kwa jinsi mgogoro katika Jimbo la Misheni Mashariki unavyoota mizizi siku hadi siku, badala ya kumalizika na umesema hali hiyo inalivuta Kanisa kwenye mavumbi, uchafu na ni aibu.
Mgogoro huo ulioibuka takribani mwaka mmoja sasa, ulianza baina ya viongozi baada ya baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu chini ya Makamu Mwenyekiti wa Jimbo hilo, Mchungaji Sauli Kajula kutangaza kumvua madaraka Mwenyekiti wa Jimbo, Mchungaji Clement Fumbo kwa madai ya ufisadi na kukiuka Katiba.
Ujumbe huo ulizitaka pande mbili zinazopingana, ambazo sasa zimegawa hata waumini, kumtazama Mungu aliyewaita katika utume, kufuata Katiba ya Kanisa na kumwomba kwa bidii ili suluhu ipatikane na Kanisa lirejee katika hali ya amani.
Mtendaji Mkuu wa Kanisa la Moravian duniani, Mchungaji Dk Jorgen Boytler alisema hayo juzi, Dar es Salaam, alipozungumza na waumini wa jimbo hilo kutoka sharika mbalimbali katika Usharika wa Tabata, kabla ya kupokea maoni yao ya jinsi ya kumaliza mgogoro huo. Alifuatana na Makamu Mwenyekiti wa Moravian duniani, Mchungaji Nosigwe Buya.
Akieleza namna uongozi wa Moravian duniani unavyosononeshwa na mgogoro huo, Dk Boytler alisema, “Ninawapa salamu kutoka uongozi wa Moravian duniani, wamenituma niwaeleze kuwa jambo hili si la Dar es Salaam pekee bali dunia nzima, Unity inasikitishwa kwa hali hii na inaomba mumtangulize Mungu mbele.
“Kanisa la Moravian lilianzishwa mwaka 1457, wapo watu waliopoteza maisha kwa kazi ngumu ya umisionari wakati ule na kazi yao inapaswa kuwa faida leo, lakini sasa ni kama Kanisa linavutwa kwenye mavumbi na uchafu, ndiyo maana tuko hapa kupokea maoni yenu ya namna ya kumaliza mgogoro huu,” aliongeza Boytler.
Kuhusu uvumi uliosambazwa kuwa barua ya ujumbe huo iliyotumwa Februari 6 ikizuia wachungaji 16 waliotangazwa kufukuzwa na Mchungaji Clement Mwaitebele wa Jimbo la Kusini ambalo ni mlezi wa Jimbo la Mashariki, haikuandikwa na Unity Board bali watu wanaomwunga mkono Fumbo, Dk Boytler alikiri mbele ya waumini hao kuwa ndiye aliyeandika barua hiyo.
Mchungaji Buya alisema kusudi lao kuja nchini ni moja; kupokea maoni ya waumini na kuyafikisha kwa uongozi wa juu wa Kanisa hilo duniani, ili kuchukua hatua, lakini alisisitiza kuwa suluhisho la mgogoro huo liko mikononi mwa waumini wa jimbo hilo.
“Jambo hili ni mwendelezo wa mikutano tuliyokaa mwishoni mwa mwaka jana na mapema mwaka huu, leo (juzi) ni siku ya mwisho kukusanya maoni yenu, hatujaleta dawa ya mgogoro, dawa mnayo ninyi ila wakati haya yanafanyika, tafadhali msipelekane Polisi wala mahakamani, mwekeni Mungu mbele,” alisema Buya.
Wakati mkutano huo ukiendelea Tabata, upande wa Mchungaji Kajula ulikuwa na kongamano la maombi ya amani kwa Taifa na mgogoro huo, katika Ushirika wa Temeke. Ingawa hawakutoa kauli yoyote lakini awali walishaeleza msimamo wa kutoutambua uongozi wa Mchungaji Fumbo.
Akisoma mapendekezo ya waumini kuhusu namna ya kumaliza mgogoro, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Jimbo hilo, Mchungaji Emmaus Mwamakula, aliuomba uongozi huo wa dunia kuchukua uamuzi mgumu katika suala hilo, kwa kuwa waumini wanateseka, wakiwemo baadhi ya wachungaji wanaonyimwa posho kwa kuwa upande wa Mchungaji Fumbo.
“Itakumbukwa, kwamba mgogoro ulianza baada ya baadhi ya wajumbe wa Halmashauri Kuu kuitisha Sinodi batili iliyotangaza kumpindua Mchungaji Fumbo, jambo lililopingwa na mabaraza na waumini wengi, hivi sasa baadhi yao wanaishi kwa vitisho na baadhi ya sharika tumesitisha kupeleka fedha kwenye Sanduku la Umoja,” alisema Mwamakula.
Aliiomba Unity iharakishe kutafuta ufumbuzi wa suala hilo ikiwa ni pamoja na kuharakisha kulifanya kuwa jimbo kamili kwa kuwa zaidi ya sharika 15 kati ya 28 za jimbo na vituo vitano na waumini wengi wako upande wao na hawana imani na malezi ya Jimbo la Kusini kwa kuwa lina maslahi katika mgogoro huo.
Wakati tukienda mitamboni, taarifa kutoka London, Uingereza zilisema Kadinali Keith O'Brien, ambaye ni kiongozi wa juu wa Kanisa Katoliki nchini humo,ametangaza kujizulu uaskofu mkuu kutokana na tuhuma za tabia mbaya na kusema hatashiriki mchakato wa kuchagua mrithi wa Papa Benedict XVI.
Kadinali huyo alisema jana kwamba hatahudhuria mkutano huo wa mchakato, kwa sababu hataki vyombo vya habari vijielekeze zaidi kwake katika kipindi hicho muhimu mjini Roma, Italia.
Wataalamu walisema uamuzi huo wa kutohudhuria mchakato huo haukutarajiwa; kwa sababu haijapata kutokea huko nyuma Kadinali asishiriki kwa sababu ya kashfa binafsi, kwa mujibu wa mwanahistoria wa Vatican, Ambrogio Piazzoni, ambaye ni Makamu Msimamizi wa Maktaba ya Vatican.
Vatican ilithibitisha jana, kwamba O’Brien amejiuzulu uaskofu wa Mtakatifu Andrea na Edinburgh. Inakubalika chini ya sheria za kidini kutokana na umri wa O’Brien ambaye Machi 17 atafikisha miaka 75-ambao ni wa kawaida kustaafu uaskofu.
Alisema hana afya mbaya na kwamba alitangaza kujizulu Novemba mwaka jana. Taarifa ya Kanisa ilisema Papa alikubali kujiuzulu huko Februari 18.
“Nikirudi nyuma katika miaka yangu ya utumishi: Kwa mema ambayo niliweza kufanya, namshukuru Mungu. Kwa upungufu uliotokea, naomba radhi kwa wote niliowakosea,” alisema O’Brien. Papa Benedict XVI anatarajia kung’atuka rasmi Februari 28.
JAJI MWANAMKE AFANYA MAPENZI NA MFUNGWA MAHAKAMANI...
![]() |
Jaji Lisa Traylor-Wolff |
Jaji wa Indiana mwenye miaka 52 anakabiliwa na mashitaka ya kutumia vibaya taaluma yake baada ya kudaiwa kufanya mapenzi na mfungwa ambaye ana umri nusu yake katika chumba cha mahojiano wakati mfungwa huyo akiwa bado kifungoni.
Lisa Traylor-Wolff anafanya kazi ya muda maalumu kama Jaji wa daraja la juu katika mahakama mbili za kaskazini kwa Indiana. Pia anafanya kazi kama wakili wa utetezi.
Tume ya Sifa za Idara ya Mahakama imesema alianza 'mahusiano ya kimwili na mteja wake mfungwa huyo mwenye miaka 26' ambaye alikuwa akimwakilisha katika kesi binafsi.
Mahusiano hayo yalidaiwa kuendelea baada ya kuwa amehukumiwa kifungo gerezani. Lisa alimwakilisha mfungwa huyo wakati alipokata rufani kupinga hukumu hiyo, kwa mujibu wa gazeti la Indianapolis Star.
Tume hiyo ilibaini kwamba alikuwa na 'mahusiano yasiyokubalika' na kijana huyo ndani ya chumba cha kukutania mwanasheria na mteja katika Jengo la Marekebisho la Miami huko Peru, Indiana.
Lisa hakuomba mkataba mpya wa ujaji wake kwa mwaka 2013.
Ana siku 20 kujibu tuhuma hizo na baada ya hapo, kesi hiyo itafikishwa kwenye Mahakama Kuu ya Indiana.
Hapo kabla alifanya kazi kama Jaji wa Mahakama ya Juu katika Mahakama ya Pulaski na alikuwa mkuu wa Chama cha Majaji katika mahakama yake.
Lisa hakujibu chochote kuhusu madai hayo.
Awali alituhumiwa kuvunja sheria nne zinazohusu taaluma yake, ikiwamo miiko inayokata mwanasheria kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mteja wake, kuzuia mwanasheria kumwakilisha mteja endapo kuna ushahidi dhahiri kwamba uwakilishi huo unasukumwa na utashi binafsi wa mwanasheria.
Pia anatuhumiwa kwa kudharau uhuru wa uaminifu na uadilifu kama jaji.
Endapo Lisa atapatikana na hatia, Mahakama Kuu ya jimbo hilo inaweza kumfungia kuendesha ofisi ya mashitaka katika jimbo hilo - kwa muda hadi kufikia kifungo cha maisha.
Haijafahamika endapo Chama cha Majaji cha Indiana pia kinachunguza kesi hiyo.
Lisa ambaye alihitimu katika Chuo Kikuu cha Sheria cha Valparaiso mwaka 1986 - mwaka ambao anayedaiwa kuwa mpenzi wake huyo alizaliwa.

Jamaa mmoja katoroka kazini wakati bosi wake hayupo ofisini. Kufika nyumbani kwake kakuta bosi amelala na mkewe kitandani, akanyata na kutoka nje mbio kurejea kazini. Alipofika akaanza kumsimulia rafiki yake: "Duh, nimemkuta bosi kalala na mke wangu nyumbani, ila nashukuru hajaniona. Nikanyata na kutimua mbio maana angejua kama nimetoroka kazini ingekuwa balaa!" Mh...
Monday, February 25, 2013
MZEE WA KANISA KKKT AHUKUMIWA KIFUNGO...
![]() |
Askofu Mkuu Dk Alex Malasusa. |
Mzee wa Baraza la Wazee wa Mtaa wa Kanani wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati Arusha, Usharika wa Ngaramtoni, Daudi Loinyeye (56) amefungwa kifungo cha nje cha miezi sita.
Amefungwa kwa kosa la kutishia kumuua kwa maneno Mwinjilisti wa usharika huo, Christopher Daniel (36).
Mwinjilishi Daniel alimfungulia Loinyeye mashitaka Julai 12 mwaka jana katika Mahakama ya Mwanzo ya Emaoi iliyoko wilayani Arumeru katika Mkoa wa Arusha.
Juni 30 mwaka jana, mzee huyo wa kanisa alikamatwa wakati akiwa katika kikao cha hesabu za harambee.
Akisoma hukumu Ijumaa iliyopita katika mahakama hiyo, Hakimu Denis Shayo, alisema mahakama imebaini kuwa mshitakiwa alikuwa na chuki kubwa na mlalamikaji (Daniel) kwa madai ya kutumia vibaya fedha za harambee zaidi ya Sh milioni 20, zilizochangwa Machi 11 mwaka jana na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo.
“Chuki hiyo imetokana na ubadhirifu wa fedha za harambee zaidi ya shilingi milioni 24 ambazo zilipatikana wakati wa harambee ya ujenzi wa kanisa la usharika huo,” alisema Hakimu
Alisema mahakama imesikiliza ushahidi wa pande zote na imeridhika na ushahidi wa mazingira na kuona kuwa kulikuwa na chuki kati ya mshitakiwa na mlalamikaji, hivyo imemtia hatiani mshitakiwa kuwa alitenda kosa hilo.
Hakimu Shayo alisema pamoja na shahidi wa pili wa mlalamikaji, Elphans Mereji (46) kukana kutofahamu njama za kupanga kumuua mwinjilisti Daniel, lakini alikana hivyo baada ya kubaini kuwa njama hizo zilijulikana.
Alisema shahidi wa kwanza wa upande wa mlalamikaji Christopher Ngungati (54) aliieleza mahakama kwamba Mereji alikwenda nyumbani kwake na kumweleza kwamba kipo kikundi cha watu, wakiongozwa na Loinyeye kimeandaa majambazi kwa lengo la kutaka kumuua Mwinjilisti Daniel na ameahidiwa kupewa Sh 300,000 kwa kazi hiyo.
Hakimu Shayo alisema mashahidi wa upande wa mshitakiwa, Emilina Stephen (36), Loning’o Loshinongi (45) na Dora Seuri (3), wote waliieleza mahakama kuwa kesi iliyofunguliwa mahakamani hapo ilikuwa ya chuki.
Kwa mujibu wa Hakimu, mashahidi hao walisema kwamba mshitakiwa alifunguliwa kesi hiyo na mwinjilisti kwa lengo la kupunguza makali ya mzee huyo wa baraza, kuacha kumfuata na kutakiwa kutoa hesabu za harambee ya sh milioni 24.
Hakimu alisema pamoja na kusema hivyo mahakamani hapo, mashahidi hao walishindwa kutoa ushahidi wao kama mwinjilisti huyo anadaiwa fedha hizo.
Kutokana na hali hiyo, mahakama iliridhika na kuona kwamba kulikuwa na ushahidi wa mazingira na kuamua kumtia hatiani mshitakiwa kwa kifungo cha nje cha miezi sita na ndani ya kifungo hicho mtuhumiwa ametakiwa kutotenda kosa lolote.
Hata hivyo, Loinyeye amepinga hukumu hiyo na kusema sababu zilizotolewa na hakimu kwamba mashahidi wake hawakutoa vielelezo vya ushahidi wa ubadhirifu dhidi ya mwinjilisti haina msingi.
Loinyeye alisema kesi iliyofunguliwa mahakamani hapo ni ya kutishia kuua kwa maneno dhidi yake na siyo ubadhirifu wa fedha za harambee na mashahidi walitoa ushahidi ni kwani nini kesi hiyo ilifunguliwa katika mahakama hiyo na wengine kukana kupanga njama hizo.
''Ninakata rufaa katika Mahakama ya Wilaya kupinga hukumu hiyo kwani haki yangu imechakachuliwa,'' alisema Loinyeye .
Mgogoro wa KKKT Usharika wa Ngaramtoni, Jimbo la Arusha Magharibi huo uliotokana na ubadhirifu wa fedha, uliwahi kuripotiwa na gazeti hili, ambapo Mkuu wa Jimbo, Mchungaji Godwini Lekashu alituhumiwa kutumia vibaya fedha hizo za harambee.
Hata hivyo, Lekashu aliripotiwa kukana shutuma hizo na kusema yeye siyo mmoja wa watuhumiwa. Mkuu wa KKKT, Askofu Dk Alex Malasusa aliunda Kamati ya maaskofu sita kutoka nje ya Dayosisi ya Kaskazini Kati Arusha, kuchunguza chanzo cha migogoro ili kupata undani wa tatizo na hatimaye kufikia hatua ya kuumaliza.
Hata hivyo migogoro ndani ya Dayosisi hiyo iliibuka mara baada ya Mchungaji Kiongozi, Philemon Mollel wa Usharika wa Ngateu, Jimbo la Arusha Magharibi kufukuzwa kazi na kusimamishwa kufanya shughuli za kichungaji katika kanisa hilo, kwa madai yasiyovumilika ndani ya kanisa.
Baada ya uongozi wa Dayosisi kuchukua hatua hiyo, washarika wa usharika wa Ngateu walipinga madai hayo, wakidai mchungaji huyo alichukuliwa hatua hiyo, kutokana na ukweli juu ya ubadhilifu uliofanywa na baadhi ya viongozi wa Dayosisi katika Hoteli ya Corridor Springs.

BI HARUSI AANGUKA DIRISHANI NA KUFA WAKATI WA FUNGATE...
![]() |
KUSHOTO: Abbie Emmett. KULIA: Sean Emmett. |
Bi harusi mwenye miaka 27 kutoka Uingereza anaaminika kuanguka na kufa kutoka kwenye chumba cha hoteli wakati akiwa kwenye fungate mjini Dubai.
Abbie Emmett alifariki siku chache tu baada ya kuwasili katika Umoja wa Falme za Kiarabu akiwa na mumewe Sean, mwenye miaka 43, baba wa watoto watatu aliyetengana na mkewe, baada ya harusi yao iliyofanyika Afrika Kusini.
Polisi mjini Dubai walikuwa wakichunguza kilichotokea baada ya Abbie, ambaye ni binti wa kasisi, aliripotiwa kuwa ameanguka kutoka dirishani kwenye hoteli hiyo Jumanne iliyopita.
Alikuwa akichangia ghorofa mjini Addlestone, Surrey, na mwendesha pikipiki wa kulipwa wa mbio za Grand Prix, Sean, na alisemekana kuwa amefunga naye ndoa takribani wiki mbili zilizopita mjini Cape Town.
Jirani yao Nicole Turvey mwenye miaka 27, alilieleza gazeti la Sunday Mirror: "Najihisi mnyonge. Ni msichana mdogo sana, umri sawa na wangu. Inasikitisha kwa kila mmoja. Hakika alikuwa akihitaji kupata watoto."
Rafiki mwingine, ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema 'hakuweza kuamini' kilichotokea na kumsifia Abbie kama 'mtu mwenye upendo'.
Msemaji wa mambo ya Nje alieleza: "Tumepokea taarifa ya kifo cha raia wa Uingereza mjini Dubai mnamo Februari 19.
Tunatoa msaada wa kibalozi kwa familia katika wakati huu mgumu."
Sean kwa sasa amestaafu mbio hizo lakini bado ni mkufunzi binafsi na amekuwa mshindi wa mbio 19 za pikipiki na pia kushiriki zaidi ya mashindano 50 ya MotoGP katika kipindi chake.

Ama kweli mjini shule! Binti mmoja alikuwa akitaka kumuingiza mjini bwanake mmoja. Akatuma meseji hivi: "Baby ninataka kununua jeans moja nzuri lakini tatizo nimesahau pochi nyumbani." Baada ya dakika kadhaa meseji ikaingia kwenye simu ya binti: "Umepokea Shilingi 600 kutoka kwa Jofu. Binti akatuma meseji tena: "Jamani Baby, sasa hii 600 ya nini wakati jeans inauzwa 50,000!" Jamaa akajibu meseji: "Shilingi 300 nauli ya kwenda kufuata pochi nyumbani na Shilingi 300 nyingine ni nauli ya kurudi kununua jeans!" Duh, kasheshe...
ZANZIBAR YAWATOA HOFU WATALII KUHUSU MAUAJI...
![]() |
Baadhi ya majengo ya kitalii katika mji wa Zanzibar. |
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imewahakikishia watalii usalama kwa kuweka ulinzi katika vyanzo vikuu vya utalii.
Waziri wa Habari, Utangazaji, Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk alisema pamoja na matukio ya hivi karibuni ya mauaji, visiwa hivyo viko salama.
Alitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari kutokana na matukio ya hivi karibuni ya mauaji ya Padri wa Kanisa Katoliki la Minara Miwili, lililopo Mji Mkongwe Zanzibar, Evarist Mushi (56).
Kuuawa kwa padri huyo kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana wakati akienda kuendesha misa ya Jumapili, kuliibua hisia kali kupitia vyombo vya nchini na vya kimataifa.
Akifafanua katika taarifa yake, Mbarouk alisema serikali imekutana na wawekezaji na wamiliki wa hoteli za kitalii na kuahidi kuweka ulinzi katika maeneo hayo.
“Hali ya utalii na usalama wa wageni wanaozuru Zanzibar ni salama...tumekutana na wawekezaji na wamiliki wa hoteli za kitalii kwa kuwaahidi kuwapatia ulinzi kadri inavyowezekana,” alisema.
Alisema ulinzi umeimarishwa katika maeneo ya vyanzo vikuu vya utalii, ikiwemo Kanisa la Anglikana la Mkunazi, ambalo zamani lilikuwa soko kuu la watumwa waliokuwa wakitoka sehemu mbali mbali za Afrika ya Mashariki na kuuzwa hapo.
Mkuu wa Idara ya Mapokezi ya Watalii katika Kanisa hilo, John Mwakanjuki alisema wamekuwa wakipokea askari polisi wanaokuja kwa zamu kuanzia asubuhi, jioni hadi usiku kulinda eneo hilo.
“Tunashukuru sana hapa ulinzi umeimarishwa kutoka jeshi la polisi na hii imetusaidia sana katika usalama wa kanisa na watalii wanaozuru hapa,” alisema Mwakanjuki.
Kanisa la Mkunazi ambalo ni la kihistoria, lilijengwa mwaka 1893. Ni moja ya makanisa ya mwanzo katika Afrika ya Mashariki. Kiwanja cha ujenzi wa kanisa hilo, kilitolewa na mtawala wa wakati huo, Sultani wa Oman.
Takwimu zinasema kanisa hilo kwa mwaka hupokea zaidi ya watalii 60,000 wanaozuru hapo na kujipatia historia ya kale na kutembelea mapango ya chini kwa chini, yaliyokuwa yakitumiwa kusafirisha watumwa kutoka baharini.
Aidha doria ya polisi imeonekana ikifanyika Kaskazini mwa kisiwa cha Zanzibar, ambako kuna hoteli nyingi za kitalii, ikiwemo Kiwengwa, Pwani Mchangani na Nungwi.
Mmoja ya wasambazaji wa vyakula ikiwemo samaki katika hoteli za kitalii saba zilizopo eneo la Kiwengwa, Chura Abdalla alisema hali ya utalii bado ni imara, licha ya kujitokeza kwa matukio yanayoashiria uvunjifu wa amani.
Chura anayetoa huduma katika hoteli kubwa za kitalii zilizopo Kiwengwa, ikiwemo ya Mapenzi na Sea Cliff , alisema mwaka jana hali ya utalii iliyumba, kutokana na kujitokeza kwa matukio ya fujo yaliyosababishwa na wafuasi wa kundi la Uamsho.
“Vurugu na fujo za uamsho za mwaka jana zilizorotesha maendeleo ya sekta ya utalii ambapo baadhi ya mahoteli yaliahirisha kupokea watalii kutoka nje ya nchi,” alisema Chura.
Awali akizungumza na waandishi wa habari, Waziri wa Habari, Mbarouk alisema kwa sasa Kamisheni ya Utalii Zanzibar ipo katika mikakati ya kuimarisha masoko ya utalii katika nchi za Asia, ikiwemo China, Japan na Korea zenye idadi kubwa ya watu.
Mwaka jana, Zanzibar inatajwa kwamba ilipokea watalii 175,000. Imewekwa mikakati ifikapo mwaka 2020 wapokee watalii 500,000.
Sekta ya Utalii Zanzibar ni tegemeo katika kuchangia pato la taifa kwa asilimia 27 huku ikitoa ajira kwa zaidi ya wananchi 25,000 katika maeneo mbalimbali.
Zanzibar hutegemea kupokea watalii wengi kutoka Italia, Uingereza, Hispania pamoja na nchi za Scandinavia.
Akizungumza katika harambee ya kuchangia Kanisa la Living Water Centre lililoko Kawe, Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe aliwaeleza waumini jana kwamba pamoja na vurugu za kidini zilizotokea, Tanzania ni nchi ya amani na mfano kwa Afrika.
Dk Mwakyembe alitaka Wakristo na Waislamu kuendelea kuhubiri amani. Aliwaonya vijana kutokubali kutumiwa kuigawa nchi. Aliwataka waendelee kumuenzi Baba wa Taifa, Julius Nyerere kwa vitendo kwa kuimarisha amani.
Kwa upande wake, kiongozi wa kanisa hilo, Mtume na Nabii Cosmas Ndegi alitaka viongozi wa dini wakemee na kusimamia kwa vitendo kauli wanazotoa. Alisema, “tumekuwa wazungumzaji mno, haitoshi tusimamie kwa vitendo na tusimamie serikali na siyo kukaa kimya.”

MWALIMU ALIYEMDHALILISHA MTOTO AKABILIWA NA KIFUNGO JELA...
![]() |
Aaron Ledean. |
Mwalimu wa zamani anakabiliwa na kifungo jela baada ya kufanya vitendo vya kujirudia vya udhalilishaji dhidi ya mvulana mwenye umri mdogo.
Baraza la wazee kwa kauli moja lilimtia hatiani Aaron Ledean kwa matukio matatu ya udhalilishaji dhidi ya mvulana chini ya miaka 20 katika miaka ya 1990.
Mwalimu huyo wa zamani wa sayansi tayari alishatiwa hatiani kwa makosa ya kunakili picha takribani 4,000 zinazodhalilisha mtoto.
Wazee wa baraza wameelezwa jinsi mwathirika huyo wa udhalilishaji - ambaye hawezi kutajwa kwa sababu za kisheria, sasa mtu mzima - alivyohisi 'vitendo vya furaha' wakati akiendelea kupondeka kwa nguvu katika bashasha, kwa shoga asiyejificha Ledean.
Alisema ilikuwa ni wakati mgumu katika maisha yake walipokuwa wakioneshana mapenzi kila mmoja.
Walikwenda kwenye mabaa katika 'siku yao ya kwanza' mjini Middlesbrough na kujihusisha na vitendo vya kimahaba walipokwenda kwenye sinema na wawili hao waliandaa ziara nyumbani kwa Ledean.
Kijana 'aliharibikiwa' pale Ledean baadaye alipovunja mahusiano hayo.
Miaka baadaye, kijana huyo alimkabili Ledean na kusema haikuwa muafaka kwa yeye kuwa katika nafasi ya kuwajibika moja kwa moja kwa watoto.
Ledean alikuwa mwalimu katika shule ya Teesside kwa miaka kadhaa. Mdai alisema matukio hayo yamekuwa akilini mwake kwa zaidi ya miaka na amekuwa huku akiamini kilichokuwa kimetokea hakikuwa sahihi.
Alifanyiwa ushauri nasaha na kuripoti suala hilo kwa polisi mwaka 2010. Ledean hakusemema chochote kuhusiana na madai hayo ya vitendo vya ngono au hatari iliyopo.
Alisema alifikiria madhara lakini sio mvuto wa kimapenzi kwa kijana huyo na kusisitiza walikuwa ni marafiki tu.
Alisema anajutia sana kumkana kijana huyo, baada ya kijana huyo bila kutarajiwa kwenda nyumbani kwake akiwa na bunda la maua waridi.
Ledean mwenye miaka 40, amekana mashitaka matatu ya udhalilishaji katika kesi kwenye mahakama ya Teesside.
Lakini mwendesha mashitaka Shaun Dodds alidai kwamba Ledean alionesha hakuonesha kuvutiwa kimapenzi na wavulana wadogo.
Jaji Walford alimweleza Ledean, mkazi wa Crook, County Dyrham, kwamba jela haiepukiki, na kumsweka rumande hadi Machi 18.

WALIMU KUCHUNGUZWA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE...
![]() |
Dk Shukuru Kawambwa. |
Wakati Waziri Mkuu akiwa ametangaza kuunda tume ya kuchunguza matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne, imeelezwa kwamba kutafanyika uchunguzi kila shule, kwa kuangalia walimu wa masomo, ambayo wanafunzi wamefaulu na wamefeli.
Taarifa hiyo ilitolewa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa kwenye mahafali ya kwanza ya kidato cha sita ya Shule ya Sekondari ya Ali Hassan Mwinyi Elite, Dar es Salaam yaliyofanyika juzi.
“Tunataka kuangalia shule moja baada ya nyingine kwa kuangalia walimu wa masomo hayo ambayo wanafunzi wao wamefeli na wale waliofaulu katika somo husika, pia tunataka kuangalia ni kwa nini masomo ya Sayansi wamefaulu kuliko Civics na Historia,” alisema Dk Kawambwa.
Alisema pamoja na walimu na wazazi kuwa na nafasi katika kuepuka matokeo mabaya, serikali imeona ni vyema itafute mzizi wa tatizo kwa kufuatilia upande wa walimu.
Alitoa mfano, “nilikutana na kiongozi wa Malaysia aliniambia kuwa tatizo lililotukuta, hata wao liliwakuta.”
Kwa mujibu wa Kawambwa, kiongozi huyo alimwambia Serikali ya nchi hiyo ilichokifanya, ilikuwa ni kuwafanyisha mtihani walimu wote.
Alisema serikali hiyo ilifikia muafaka na chama cha walimu, wakaona waliofeli watengewe darasa lao.
Ingawa Dk Kawambwa hakufafanua zaidi kama pia Serikali inataka ifuate mkondo wa Malaysia wa kuwafanyisha walimu mtihani, alisisitiza kwamba jambo la msingi ni kuangalia kiini cha tatizo.
Alisema, “kwa mfano tukiangalia somo la Jiografia, kila shule tutamwangalia mwalimu wake ambaye wanafunzi wake wamefeli na wale ambao wanafunzi wake wamefaulu.”
“Pamoja na wanasiasa wa bei nafuu kutaka nijiuzulu, hawajui nje ya uwaziri nina maisha mengine, naweza kurudi kulima mihogo… Jambo la msingi ni kuangalia kiini cha tatizo hili,” alisema.
Alisisitiza kiwango cha ufaulu na kuongezeka kwa waliofeli, kimekuwepo kwa kipindi cha miaka mitatu tangu mwaka 2010 katika shule za serikali, binafsi na seminari.
Alitoa mfano wa kushuka kwa ufaulu kwa shule binafsi, kwamba mwaka 2010 waliopata daraja la kwanza ni watahiniwa 4,276, sawa wa asimilia 4.8 na kwamba mwaka uliofuata, idadi ilishuka na kufika 1,614 sawa na asilimia 2.8.
Aidha matokeo mwaka 2012, yanaonesha ufaulu umeshuka tena, ambapo waliopata daraja la kwanza ni 1,032 sawa na asilimia 1.6.
Kwa upande wa shule za seminari, alisema mwaka 2010 wanafunzi 695 sawa na asilimia 14.3 walipata daraja la kwanza. Hata hivyo, idadi ilishuka mwaka uliofuata hadi 428 sawa na asilimia 7.9. Mwaka 2012 imeendelea kushuka hadi watahiniwa 197 sawa na asilimia 3.3.
Wakati tume iliyoundwa na Waziri Mkuu haijafahamika wajumbe wake, vile vile hazijawekwa hadidu rejea zitakazozingatiwa katika kazi yake itakayoanza wakati wowote kuanzia sasa.
Tume hiyo inajumuisha wadau kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tamongsco), taasisi za dini zinazotoa huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Asasi Zisizo za Serikali (Azise) zinazoshughulikia elimu.
Wajumbe wengine watatoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (Tahossa).
Akizungumza na mwandishi jana, Rais wa CWT, Gratian Mukoba alisema chama chake hakiko tayari kuwa sehemu ya tume hiyo, kwa kile wanachoamini kwamba matatizo yanayoikabili sekta ya elimu, yanajulikana.
“Hatuko tayari kuwa sehemu ya hiyo tume, tunasubiri watupe barua ili tuwajibu kuwa matatizo yaliyofanya wanafunzi kufeli, wanayajua,” alisema.
Mukoba aliongeza kuwa, “Serikali isipoteze muda na rasilimali ambazo inaweza kuzitumia maeneo mengine kwa sababu matatizo ya sekta ya elimu wanayajua. Tumeshawahi kufanya vikao na Waziri Mkuu, Rais na hata waziri wa elimu. Hii ni sawa na kumtafuta paka mweusi kwenye chumba cha giza.”
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia ambaye hivi karibuni alikuwa miongoni mwa waliotaka Rais aunde tume kuchunguza mfumo wa elimu, alisema tume iliyoundwa kuchunguza matokeo ni sawa na tone katika bahari.

Sunday, February 24, 2013
CHUO CHAFUNGWA KWA KULEA WATOTO WASIOJULIKANA...
![]() |
Stella Manyanya. |
Kuibuka kwa biashara ya binadamu kunakoendelea kuimarika duniani, kumemtia shaka Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya na kuonya taasisi zinazochukua watoto na kuwalea bila taarifa zao kufahamika.
Manyanya alitoa onyo hilo juzi kutokana na taarifa ya kuwapo kituo cha elimu na malezi ya Kiislamu cha Nourul Hudaa Islamic Center Muzdalifa (MICO) kilichoko mjini hapa licha ya kuwa hakipo kisheria, lakini hata orodha ya watoto wanaolelewa hapo haifahamiki.
Pia viongozi wanaoendesha kituo hicho hawafahamiki huku daftari linaloonesha watoto hao wanakotoka au taarifa za wazazi wao halipo.
Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Mkoa alilazimika kutengua uamuzi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Sumbawanga iliyoamuru kufungwa kituo cha MICO baada ya kushindwa kukidhi vigezo muhimu ikiwa ni pamoja na kutosajiliwa.
Manyanya alifikia uamuzi huo jana jioni baada ya watoto 190 na walimu wao wawili, Hamisi Matope na Ustaadh Idrisa Majundo kutoka kituo hicho kilichopo eneo la Nelson Mandela mjini hapa, kuandamana hadi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, ili waonane naye.
Akimweleza Mkuu wa Mkoa katika kikao cha dharura kilichofanyika katika jengo la Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuhudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa, Salum Chima, mmoja wa walimu wa kituo hicho Matope alidai walilazimika kuwapeleka watoto hao ili Mkuu wa Mkoa awape malazi, kwa kuwa kituo chao kimeamriwa kufungwa na Manispaa ya Sumbawanga.
“Tumeamriwa kufunga kituo chetu na watoto warudishwe kwao hadi kitakapokidhi hadhi ya kuwa chuo, sasa tumewaleta watoto hawa kwa Mkuu wa Mkoa, ili awape malazi hadi watakapoweza kurejeshwa kwao, kwa kuwa sasa hawana pa kulala,“ alisema Matope.
Watoto hao kwa mujibu wa Majundo baadhi yao ni yatima kutoka sehemu mbalimbali za Mkoa wa Rukwa na mikoa ya jirani ya Mbeya, Katavi na Kigoma, ambapo baadhi yao wanasoma shule za msingi na sekondari mjini hapa.
Wengi wao hawakuwa tayari kuzungumza na mwandishi wa habari hizi kwa kile walichodai kuwa wamekatazwa na walimu wao kusema lolote kuhusu malezi yao.
Hata hivyo, mtoto aliyejitambulisha kwa jina la Maka Salumu (15) wa Kigoma, alionesha ujasiri na kudai kuwa waliandamana ili kumshinikiza Mkuu wa Mkoa awape malazi na chakula, hadi watakaporejea kwao kwani kituo chao kimefungwa kwa amri ya Manispaa.
“Mtoto mdogo miongoni mwetu ana umri wa miaka saba, miye nililetwa kituoni na bibi yangu nikitoka Kigoma, sasa kimefungwa hatuna pa kulala, hivyo tumekuja hapa ikiwezekana tulale hapa hapa ofisini kwa Mkuu wa Mkoa, hadi tutakaporejeshwa kwetu,“ alisema Salumu.
Katibu Tawala wa Mkoa, Chima alifafanua sababu za kufungwa kwa kituo hicho.
Alisema watoto katika kituo hicho walikuwa wakikabiliwa na kadhia mbalimbali zikiwamo za kulala chini sakafuni huku sakafu hiyo ikiwa na imelowa maji hata kwa waliokuwa wagonjwa, kushinda na njaa.
Licha ya kuwa kituo hicho hakijasajiliwa lakini watoto hao walikuwa hawana sehemu ya kupikia, huku majengo ya kituo hicho yakiwa chakavu na yasiyofaa kabisa kwa matumizi ya binadamu, kwani hata vyumba vya kulala watoto hao sakafu zina mashimo.
“Miye binafsi nilishafika kituoni hapo, pamoja na matatizo hayo pia hakijasajiliwa, hivyo hakipo kisheria na hata utunzaji kumbukumbu zake si mzuri kwani hakina hata daftari la orodha ya watoto hao sambamba na kuwa hata idadi yao haijulikani pia viongozi wanaongoza kituo hicho hawafahamiki kabisa,“ alisema Chima.
Ndipo Manyanya licha ya kuwashukuru kufanya maandamano ya amani, pia aliagiza wapewe miezi miwili zaidi ili waboreshe upungufu uliojitokeza.
Pia alimwagiza Chima afanye ukaguzi wa mara kwa mara katika kituo hicho, ili kuhakikisha kama upungufu uliojitokeza umerekebishwa na kuboreshwa pia wapewe wataalamu watakaowasaidia kuhakikisha kinasajiliwa kisheria.
“Lazima idadi na majina na wanakotoka ifahamike, si sahihi kulea watoto ambao hawafahamiki wazazi wao wako wapi lazima na watoto wenyewe wafahamishe walipo wazazi wao,“ alisisitiza.

TUME YAUNDWA KUCHUNGUZA KUFELI KIDATO CHA NNE...
![]() |
Mkurugenzi wa NECTA, Dk Joyce Ndalichako akionesha moja ya karatasi za mtihani wa mmoja wa watahiniwa. |
Serikali hatimaye imeonesha usikivu kwa kukubali maoni ya wadau mbalimbali wa elimu nchini na kuunda Tume Maalumu itakayochunguza matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne.
Matokeo hayo yaliyotangazwa Februari 18 na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa, yalionesha watahiniwa asilimia 60 kufeli mtihani huo uliofanywa Oktoba mwaka jana, na kuzua maswali kwa wadau.
Baada ya wadau hao wakiwamo viongozi wa vyama vya siasa na Serikali kupendekeza kuchukuliwa hatua kuhusiana na matokeo hayo mabaya kupata kutokea katika historia ya elimu nchini, Serikali imeridhia na kuitikia mwito huo.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Peniel Lyimo katika taarifa yake jana, alisema Tume hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kazi wakati wowote wiki ijayo, inajumuisha wadau kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (TAMONGSCO), taasisi za dini zinazotoa huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Asasi Zisizo za Serikali (AZISE) zinazoshughulikia elimu.
Wadau wengine watatoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA).
Aliwaomba wadau wa elimu, wazazi, walezi na wananchi kwa ujumla wao watoe ushirikiano kwa Tume ili iweze kufanya kazi yake kwa ufanisi.
Hata hivyo, Lyimo katika taarifa yake fupi, hakutaja majina ya watakaounda Tume hiyo wala muda itakayopewa kukamilisha kazi yake.
Akitangaza matokeo, Dk Kawambwa alisema zaidi ya nusu ya wanafunzi waliofanya mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne, wamepata daraja sifuri na kufafanua, kwamba kati ya wanafunzi 397, 136 waliofanya mtihani huo, 240,903, ndio waliopata daraja sifuri.
Alisema waliopata daraja la kwanza ni 1,641, la pili 6,453 na la tatu 15,426 na kuongeza kuwa wanafunzi 24 ambao matokeo yao yalifutwa kwa kuandika matusi kwenye masomo mbalimbali wakionesha utovu wa nidhamu wa hali ya juu na kwamba Serikali haitavumilia.
“Tunaangalia hatua za kisheria za kuchukua dhidi yao. Na kwa wale waliofanya udanganyifu wanaweza kufanya mtihani tena baada ya mwaka mmoja,” alisema.
Akizungumzia tathmini ya mtihani huo, Kawambwa alisema shule zilizofanya vizuri ni zenye mahitaji ya msingi, ikiwamo walimu wa kutosha, miundombinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
“Ukiangalia zilizofanya vibaya, ni zenye changamoto ya kukosa walimu hususan wa Sayansi
na Hisabati, kutokuwapo kwa maabara za shule na upungufu mkubwa wa vitabu vya kiada na ziada na kuwa na uwiano wa kitabu kimoja kwa wanafunzi 10,” alisema.
Baada ya kutangaza matokeo hayo, chama cha NCCR-Mageuzi kupitia Mwenyekiti wake, James Mbatia, kilimwomba Rais Jakaya Kikwete aunde Tume itakayojumuisha wataalamu waliobobea katika elimu ili kupata suluhu ya kuendelea kushuka kwa elimu, kwa kuwa limekuwa janga la kitaifa.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa naye alipendekeza iundwe Tume kuchunguza hali hiyo ya idadi kubwa ya wanafunzi kufeli mtihani huo.
“Matokeo ya Kidato cha Nne yamenisikitisha sana maana asilimia 60 ya wanafunzi kupata sifuri ni jambo la hatari. Napenda kumsihi Rais Kikwete, amefanikiwa katika sekta nyingine kama barabara… aunde tume kuchunguza sababu za wanafunzi kufeli, lakini kubwa kuliko zote tume hiyo ije na mapendekezo ya namna bora ya kuboresha mfumo wetu wa elimu,” alisema Lowassa.
Alisisitiza kuwa hoja ya kutaka Serikali iunde tume kuboresha mfumo wa elimu, alipata kuitoa mara kadhaa kwani anaamini katika kaulimbiu ya ‘Elimu Kabla, Kilimo Kwanza’.
“Kila Mtanzania anasema lake, wengine wanasema ni hujuma, wengine wanadai kuna mgomo baridi wa elimu, malalamiko na sababu ni nyingi na njia pekee ya kujua ukweli ni kupitia tume,” alipendekeza Lowassa.
Wakati hayo yakiendelea, Serikali kupitia kwa Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo imesema inaangalia utaratibu wa watahiniwa waliopata daraja sifuri kurudia mtihani mwaka huu kwa gharama zake.
Aidha, ikasema matokeo hayo mabaya yamesababishwa na mambo makuu manane; kubwa likiwa ni wanafunzi kupita bila kuchujwa katika mtihani wa Kidato cha Pili walioufanya miaka miwili
iliyopita.
Ingawa hata hadidu za rejea kwa tume hiyo hazikutajwa jana, pengine zikisubiri izinduliwe rasmi, ni dhahiri pamoja na mambo mengine, itachunguza pia chanzo cha watahiniwa badala ya kujibu maswali, wamekuwa wakiandika matusi na kuchora vibonzo.
Pia itaweza kuchunguza utendaji kazi wa walimu na kuhusiana na migomo, lakini hasa kutafuta suluhu ya nini kifanyike kuhakikisha wanafundisha katika mazingira mazuri, huku wanafunzi nao wakijibidiisha katika masomo yao.
Suala la uwiano wa walimu na wanafunzi, pamoja na vifaa vya kufundishia na kujifunzia na maabara, huenda nalo likawamo hususan katika shule za sekondari ambazo nazo zimezua mvutano miongoni mwa wadau kuhusu hoja ya kujengwa bila maandalizi ya kutosha.

Jamaa mmoja kapita sehemu isiyoruhusiwa kwenye kambi moja ya jeshi. Fasta akapewa adhabu ya kupakia matofali 1,000 kwenye lori lililokuwa jirani. Baada ya kupakia matofali 900, jamaa akakumbuka mkuu wa ile kambi walisoma naye. Akampigia simu na mambo yalikuwa hivi. JAMAA: Haloo mkuu, vijana wako wamenipa adhabu ya kupakia matofali kwenye lori. MKUU: Aah, hao wajinga sana, hawajui kama tumesoma wote? Sasa hebu yashushe halafu uje ofisini! Duh, balaa...
ZANZIBAR SI SHWARI! IMAMU AUAWA KWA MAPANGA...
![]() |
Msikiti wa Mwakaje, Zanzibar. |
Imamu wa Msikiti wa Mwakaje, Ali Khamis Ali (60) amepigwa mapanga hadi kufa na watu wanaodhaniwa kuwa wezi alipokwenda shambani mwake kukagua mazao yake Kitope mkoa wa Kaskazini Unguja.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kaskazini Unguja, Ahmada Abdalla alithibitisha kutokea mauaji hayo na kusema juzi mchana alikwenda shambani kwake na kukuta watu wakiiba nazi katika shamba hilo ambapo walimvamia na kumpiga mapanga.
“Ni kweli marehemu alivamiwa na watu wanaoaminika kuwa wezi shambani ambako kumekuwa na wizi wa mazao uliokithiri,” alisema.
Marehemu alizikwa jana na waumini wa dini ya kiislamu katika Msikiti wa Mwakaje, ambapo Jeshi la Polisi lilisema limeanza msako dhidi wahusika waliofanya uhalifu huo.
Mapema Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema Jeshi lake limetangaza dau nono la Sh milioni 10 kwa watu watakaotoa taarifa zitakazowezesha kukamatwa kwa watu waliomuua Padri Evarist Mushi wiki iliyopita.
“Jeshi la Polisi linatangaza dau la Sh milioni 10 kwa watu watakaotoa taarifa na hatimaye kukamatwa kwa wahalifu waliomuua Padri Mushi,” alisema Mussa.
Akifafanua, alisema hadi sasa Polisi imekamata watu kadhaa wakifanyiwa mahojiano kuhusu taarifa za kifo cha Padri Mushi.
“Tumekamata watu kadhaa tukiwafanyia mahojiano zaidi kuhusu tukio la mauaji ya Padri Mushi lakini hatujamfikisha mtu yeyote mahakamani hadi sasa,” alisema Mussa.
Haya ni mashambulizi ya nne kutokea tangu mwaka jana dhidi ya viongozi wa dini, ambapo katika tukio la kwanza, Shehe Fadhil Suleiman Soraga alimwagiwa tindikali akiwa mazoezini karibu na nyumbani kwake Magomeni saa za asubuhi.
Shambulizi lingine ni dhidi ya Padri Ambrose Mkenda ambaye alipigwa mapanga shingoni nyumbani kwake Tomondo, Unguja.

Saturday, February 23, 2013
KIBAKA AINGIA MLANGO WA JIRANI AKIDHANI KWA RIHANNA...
Mtu mmoja amekamatwa nje ya nyumba ya mwimbaji Rihanna iliyoko Southern California katika Pacific Palisades ... baada ya majirani kumuona mtu akiangaza angaza na kumkamata juzi usiku, imefahamika.
Vyanzo vya kisheria vimeeleza ... mtuhumiwa huyo aliwaeleza polisi mtu mmoja alimtumia baruapepe akimwelekeza jinsi ya kuingia kwenye nyumba hiyo ... hivyo alikwenda kwenye jengo hilo na kufuata maelekezo hayo.
Imeelezwa maelekezo hayo yalifanya kazi ... sababu mtu huyo aliweza kuingia ndani ya nyumba hiyo ... ambako alidaiwa kupeleleza kwa muda kabla ya majirani kugundua kilichokuwa kikiendelea.
Vyanzo vimeeleza ... majirani walikwenda kwenye nyumba hiyo na kumkabili mtu huyo -- na hatimaye kumshikilia baada ya kujiridhisha kwamba haishi pale. Polisi waliitwa eneo la tukio na kumchukua mtu huyo chini ya ulinzi.
Mtu huyo kwa sasa anachunguzwa kwa ujambazi.
Polisi wamesema mtu huyo hakuwahi kuingia kwenye nyumba ya Rihanna ... lakini, badala yake aliingia mlango mwingine akiamini kwamba ilikuwa ni nyumba ya Rihanna.
Alikamatwa nje ya jengo hilo ... na si nyumbani kwa Rihanna.

MKONGWE WA UTENGENEZAJI KATUNI AFARIKI DUNIA AKIWA NA MIAKA 91...
Bob Godfrey, mtengenezaji katuni mkongwe aliyefanikisha katuni bora za watoto za Roobarb & Custard na Henry's Cat, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91, familia yake imethibitisha jana.
Mzaliwa huyo wa Australia, ambaye amefurahia kazi yake kwa karne tano, ameshinda tuzo tatu za Baftas kwa kazi yake na pia Tuzo ya Oscar kutokana na filamu yake fupi ya Great, ambayo iliangazia maisha ya mhandisi Isambard Kingdom Brunel.
Katuni za paka na mbwa za Roobarb zilihadithiwa na Richard Briers, ambaye alifariki Jumapili iliyopita akiwa na miaka 79, na zilipata umaarufu mkubwa mno kwa mada zake zilizokamata na uhuishaji wake.
Godfrey alianza maisha yake ya kazi kama mchoraji kabla ya kujiunga na studio ya ubunifu na kuingia kwenye utengenezaji katuni. Kazi yake ya mwisho ilikuwa Millennium: Muziki kwa ajili ya Channel 4 mwaka 1999.
Mtengenezaji katuni huyo, ambaye alipata elimu yake mashariki mwa Londoni, alibainisha mwaka 2001 kwamba alikuwa na jutio moja, akisema: "Nilipendelea kuwa nimefanya makala moja kamili lakini siwezi kuonekana kujirefusha mwenyewe kwa urefu huo.
"Pale unapotazama filamu zangu, zinaonekana kuwa mfululizo wa matangazo ya biashara ya sekunde 30 kwa pamoja," alilieleza gazeti la The Guardian.
"Mimi ni mtu wa umbali mfupi nitake au nisitake."
Mwanzilishi wa Studio ya Aardman Animations, Peter Lord alisema kwenye mtandao wa Twitter: "Mpendwa mzee Bob Godfrey hatunaye tena."

WANANDOA WATUMIA MAJI YA TANKI LENYE MWILI WA MTU HOTELINI...
![]() |
KUSHOTO: Michael na Sabina. KULIA: Mafundi wakichunguza matanki hayo. |
Wanandoa wa Uingereza walioko mapumzikoni mjini Los Angeles wameeleza jinsi walivyokunywa, kuoga na kupiga mswaki meno yao kwa kutumia maji kutoka katika tanki lililoko katika paa la hoteli - ambamo mwili wa mwanamke ulikuwa umezama kwa wiki tatu.
Ni hadi pale mwili ulioharibika wa mwanafunzi wa chuo kikuu mwenye miaka 21, Elisa Lam ulipogunduliwa wiki hii ndipo walipobaini kwanini maji ya hoteli hiyo yalikuwa na ladha ya 'ajabu'.
Sabina Baugh, mwenye miaka 27, alikaa siku nane na mumewe Michael, ambaye pia ana miaka 27, kwenye Hoteli ya Cecil iliyoko Los Angeles.
Eneo hilo lina matukio mengi ya uhalifu katika jiji, hivyo kuliko kutoka usiku na kwenda kusaka chupa ya maji ya kunywa, walikunywa kutoka kwenye bomba.
Juzi Sabina, mwalimu wa piano, alisema: "Maji hayo yalikuwa na ladha ya ajabu na inayokera. Hatukuwahi kamwe kufikiria kitu kama hicho. Tulifikiri ilikuwa ndivyo yalivyo."
Michael, mpiga gitaa na mwalimu wa muziki, aliongeza: "Pale tulipobaini, tulijihisi kuumwa tumbo, hali mbaya mno. Hatuko sawa kisaikolojia. Ni kitu cha elimu nafsia. Kama unakifikiria, sio kizuri."
Wanandoa hao pia walisema maji katika hoteli hiyo inayotoza Pauni 52 kwa usiku mmoja, na kupewa hadhi ya nyota mbili katika mtandao wa TripAdvisor, yalikuwa yakichuruzika kutoka kwenye bomba. Wageni wengine waliripoti mafuriko.
Wanandoa hao wanaotokea Plymouth, sasa wanakaa katika sehemu nyingine ya mji na mamlaka hizo zinachunguza maji hayo katika eneo hilo kwa uchafu.
Polisi walithibitisha juzi kwamba mwili huo ulikuwa wa Elisa Lam, mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha British Columbia nchini Canada, ambaye alikuwa akisafiri kwenda Santa Cruz kaskazini mwa California ndipo alipotoweka mwanzoni mwa mwezi na kuipa wasiwasi familia yake.
Polisi hawafahamu jinsi gani Elisa alivyokufa au jinsi alivyoishia kwenye tanki katika paa la hoteli, ambayo inalindwa na milango madhubuti na kengele za dharura.
Hoteli hiyo ilijengwa mwaka 1920 lakini ilikarabatiwa miaka kadhaa iliyopita wakati fulani ilikuwa makazi mara kwa mara ya muuaji Richard Ramirez - aliyejipa jina la utani the Night Stalker - na Jack Unterweger aliyehusika na vifo vya makahaba tisa barani Ulaya na Marekani.
Polisi wamesema kumekuwa na ripoti za kuendelea kwa uhalifu katika hoteli hiyo.
Mwili wake uligunduliwa kwenye moja ya matanki makubwa ya maji baada ya wafanyakazi wa matengenezo walipopanda juu kuchunguza taarifa za kuwapo kwa presha ndogo ya maji, msemaji wa polisi wa Los Angeles alisema.
Bernard Diaz, mwenye miaka 89, ambaye ameishi hapo kwa miaka 32, alilieleza gazeti la Los Angeles Times kwamba alisikia kelele 'kubwa' katika ghorofa yake juu usiku ambao Elisa alitoweka.
Alisema ghorofa hilo lilikumbwa na matatizo ya mafuriko ya maji usiku huo.

Wataalamu katika hospitali moja ya vichaa waliamua kufanya jaribio ili kubaini wagonjwa wao ambao wameanza kupata nafuu. Wakachora picha ya embe ukutani na kuwataka vichaa wote wainuke na kwenda kula embe lile. Wote wakainuka kwa fujo na kuelekea ukutani isipokuwa mmoja tu ambaye aliendelea kujibanza kwenye kona ya chumba kile. Mtaalamu mmoja akiwa na imani kwamba yule kapona akamfuata kujua sababu za kutoinuka. Kichaa kwa kujiamini akamjibu, "Aah, mie nangojea kokwa!" Kasheshe...
Friday, February 22, 2013
WALIOFELI KIDATO CHA NNE KUPEWA NAFASI YA KURUDIA MTIHANI...
![]() |
Philipo Mulugo. |
Serikali imesema inaangalia utaratibu wa watahiniwa 240,903 wa kidato cha nne waliopata daraja sifuri katika matokeo yaliyotangazwa hivi karibuni, kurudia mtihani mwaka huu kwa gharama zake.
Aidha, imesema matokeo mabaya ya mwaka huu yamesababishwa na mambo makuu manane, kubwa likiwa ni wanafunzi waliopita bila kuchujwa katika mtihani wa kidato cha pili walioufanya miaka miwili iliyopita.
Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo alisema hayo jana alipozungumza na gazeti hili kuhusu hatua zitakazochukuliwa na Serikali kutokana na idadi kubwa (asilimia 60.6) ya watahiniwa wa kidato cha nne kufeli mtihani wa Taifa kwa daraja sifuri na hatima yao ya kujiuzulu.
Akifafanua, Mulugo alisema, “suala la kujiuzulu lipo nje ya mipaka yangu ya kazi kwa kuwa halihusishi wizara moja wala Serikali pekee. Lakini kuhusu hatua zitakazochukuliwa kwa waliopata sifuri, Serikali inafikiria warudie mtihani mwaka huu”.
Ingawa alisema wazo hilo halijapitishwa, lakini hivi sasa linajadiliwa kuona namna ya kuwasaidia watahiniwa zaidi ya 240,000 waliopata alama hiyo, kurudia mtihani wa Taifa kwa gharama za Serikali. Watahiniwa waliosajiliwa walikuwa 480,036.
“Katika kuchambua hilo, tumeangalia namna ya kuwalipia ada ya mtihani ambayo mwaka jana walilipa Sh 35,000 kila mwanafunzi, likipita hilo la kurudia mtihani, Serikali italipia ada hiyo na wataufanya kama watahiniwa binafsi,” alibainisha Mulugo.
Kuhusu matokeo mabaya, Mulugo alisema sababu kubwa ni kutokuwapo mchujo kwa watahiniwa waliopata chini ya asilimia 30 wakati walipofanya mtihani wa kidato cha pili na hali hiyo inaweza kujitokeza hata kwa watahiniwa wa kidato cha nne mwaka huu.
“Hawa ni waliofanya mtihani wakati mfumo wa kuwachuja walipokuwa kidato cha pili ulikuwa umeondolewa, walipita wote, iwe alipata F au A, na walipita kwa miaka miwili, hivyo hata mwaka huu athari zinaweza kutokea, ila watakaoingia kidato cha nne mwakani, walichujwa na sifuri zilikuwa zaidi ya 136,000, hivyo tofauti inaweza kuwapo,” alifafanua.
Hata hivyo, alisema matokeo hayo mabaya hayatarekebishwa kwa namna yoyote, ili kuongeza idadi ya watakaoingia kidato cha tano mwaka huu, bali watahiniwa 23,500 waliopata daraja la kwanza hadi la tatu ndio watakaoendelea. Alisema watakaochukuliwa Ualimu ni wa daraja la nne ya alama 26 na 27 huku wenye alama 28 wakiachwa bila kuchukuliwa mwaka huu.
Akielezea shinikizo la kuwataka yeye, Waziri Dk Shukuru Kawambwa na Katibu Mkuu wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Joyce Ndalichako wajiuzulu, Mulugo alisema suala hilo liko nje ya mipaka yake ya kazi kwa kuwa linahusisha Wizara zaidi ya moja.
“Si sahihi kulizungumza hilo la kujiuzulu, kwa kuwa liko nje ya mipaka yangu ya kazi, si suala la Wizara ya Elimu pekee, ni mtambuka na linashughulikiwa na wizara zaidi ya moja, hata hivyo hatua tayari zinachukuliwa kutafuta kwanza kiini cha tatizo na mpaka sasa tumegundua mambo manane.
Akiyataja, Mulugo alisema ni pamoja na jamii kutosaidia wanafunzi kufikia malengo, wanafunzi wenyewe, mitandao ya kijamii nje ya masuala ya elimu, wazazi, Sayansi na Teknolojia na Serikali katika mipango na sera, mwingiliano wa uwajibikaji kitaasisi (wizara zaidi ya moja, ikiwamo Tamisemi iliyo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu).
Kuhusu madai ya mtihani mgumu uliokuwa na mbinu za kitaalamu zaidi, Mulugo alisema hakuna mtihani mwepesi duniani na kuongeza, kwamba uwajibikaji wa wanafunzi katika elimu umefifia kutokana na uhuru mkubwa walionao kupitia mitandao ya jamii na vyombo vya habari, huku akidai baadhi wanaiga kwa kasi mabaya wanayoyaona humo na kuyahamishia katika mitihani.
Pia alieleza namna mtihani unavyotungwa na kubainisha, kuwa Necta huandika barua kwa Ofisa Elimu wa Mkoa akiomba walimu makini walio kazini, watunge maswali ya mwongozo wa mtihani na maswali hayo hupelekwa katika Baraza na huko walimu baadhi kuyapitia tena.
“Baada ya hapo walimu angalau wawili au watatu kutoka kila mkoa huweka kambi ya siku si chini ya 10 kuhakiki na kupitia maswali hayo, kisha Necta huunda kamati ndogo inayapitia miongoni mwao maswali yanakuwa mtihani na si nje ya hapo. Utaona anayetunga mtihani ni mwalimu anayemfahamu mwanafunzi,” alisema Mulugo.
Katika kusahihisha, kwa mujibu wa Mulugo, walimu makini kutoka kila mkoa huchukuliwa kwa uwakilishi na kupangiwa vituo vya kusahihisha mtihani, na walimu wa somo moja hukaa kituo kimoja tofauti na wa somo lingine na mwalimu mmoja husahihisha swali moja na kumpa mwenzake.
“Haiwezekani kumpendelea mtu, unakuta mtihani wa hesabu uko Kilimanjaro, Kiingereza uko Dar es Salaam, labda wa Kiswahili unasahihishwa Mbeya, sasa walimu wote wanakujua ama wakupendelee au kukuonea?” Alisema na kusisitiza kuwa matokeo ya mwaka huu yalitokana na udhibiti wa wizi wa mitihani uliofanywa na Serikali na utaendelea miaka yote.
Aliitaka jamii kushirikiana kuwawezesha wanafunzi kufikia malengo ya elimu kwa kudhibiti katika matumizi ya simu, mitandao ya jamii na wizi wa mitihani na kuongeza kuwa suala la elimu linapaswa kuwa la wote, huku Serikali ikiwa ni mtunga sera na msimamizi.
Yamekuwapo malalamiko mengi kutoka kwa wananchi wa kada mbalimbali kuhusu kufeli kwa kiasi kikubwa wanafunzi waliomaliza kidato cha nne mwaka jana.

Subscribe to:
Posts (Atom)