Thursday, February 28, 2013

BOBBY BROWN AHUKUMIWA KIFUNGO JELA KWA ULEVI...

Bobby Brown amehukumiwa kifungo cha siku 55 jela kufuatia kukamatwa kwake hivi karibu akiendesha gari huku akiwa amelewa, imefahamika.
Bobby alikamatwa Oktoba mwaka jana baada ya polisi kumsimamisha mwimbaji huyo kutokana na uendeshaji wa hatari, na kunuka harufu ya pombe ndani ya gari yake.
Bobby alishitakiwa kwa makosa ya kuendesha huku akiwa amelewa na kutumia leseni iliyofungiwa wakati wa tukio hilo. (Leseni ya Bobby imefungiwa kufuatia makosa kama hayo siku za nyuma mwaka 2012. Bobby pia alishawahi kuhusika na kosa kama hilo mwaka 1996.)
Bobby hakutakiwa kujibu chochote jana. Alihukumiwa kifungo hicho jena pamoja na kuwekwa chini ya uangalizi maalumu kwa miaka minne. Pia ameamriwa kumaliza mpango wake wa miezi 18 wa tiba dhidi ya pombe. Hii ni mara ya tatu kwa Bobby kukamatwa kwa kuendesha gari huku akiwa amelewa.
Bobby ataanza kutumikia kifungo hicho ifikapo Machi 20, mwaka huu - na ameamriwa kuhudhuria mikutano ya 3 AA kwa wiki hadi wakati huo.

No comments: