![]() |
| Waziri Mkuu Mizengo Pinda. |
Vyombo vya Dola vinafanya uchunguzi kubaini watu waliochochea na kupotosha suala la gesi mkoani Mtwara, kabla ya kuamua ni hatua gani zichukuliwe.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, alisema jana kuwa lengo ni kubaini hasa waliopotosha jambo hilo, kiasi cha kusababisha vurugu zilizoleta hasara ya mamilioni ya fedha kwa Serikali na watu binafsi Mtwara na Masasi.
Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, katika vurugu hizo, Halmashauri ya Masasi pekee, ilipata hasara ya Sh bilioni 1.5 kutokana na uharibifu wa majengo, magari na mali nyingine zilizoteketezwa.
Dk Nchimbi alisema wakati wa uharibifu huo, Masasi mbali na majengo na magari kuchomwa moto kwa kutumia petroli, watu hao waliteka kituo cha mafuta na kuamuru kwamba wasipopewa mafuta watakilipua.
Alisema halmashauri ya Masasi inahitaji Sh milioni 791 kurejesha hali ya kawaida ya ofisi zilizoharibiwa, hususan kwa kuweka samani na mahitaji mengine.
Akijibu maswali ya waandishi aliokutana nao kuelezea yaliyojiri katika kikao kati yake na wananchi wa Mtwara, Waziri Mkuu Pinda alisema wanajaribu kuona ni nani na kwa nini watu hao walifanya hivyo na hatua gani zichukuliwe.
“Wakati mwingine siasa ni taabu, unapenda kufanya jambo kwa sababu linakuimarisha kwenye jimbo bila kujali madhara yake. Tunajaribu kuona ni nani, kwa nini na hatua gani zichukuliwe,” alisema Pinda.
Alipoulizwa iwapo Serikali ina mpango wa kufidia walioharibiwa mali zao katika vurugu hizo, Waziri Mkuu alisema: “Ni kweli kuna mali zimepotea, lakini Serikali pia imepoteza mali na watu wamepoteza maisha. Ukizungumzia fidia, lazima tukae chini kulitazama kwa makini.
“Unataka fidia kwa misingi gani, kwa nini. Maadam ni jambo linaweza kuzungumzika, kama itaonekana upo umuhimu wa kufanya hivyo. Kwa upande wa Serikali hakuna ujanja, lazima magari yanunuliwe, ofisi zijengwe,” alisema Pinda.
Waziri Mkuu ambaye alisisitiza kwamba ni kwa bahati mbaya vurugu hizo hazikupaswa kufika mahali hapo, alisema atatoa taarifa bungeni juu ya suluhu iliyopatikana katika mkutano wake.
Akizungumzia uamuzi wa Bunge kuunda Tume ya kwenda kuzungumza na wananchi wa Mtwara kabla ya kujadili suala hilo katika mkutano huu wa Bunge, Pinda ambaye ni kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni, alisema uamuzi alioufanya Spika Anne Makinda ni kwa nia njema.
“Bunge pia linataka kufahamu ni nini kimejitokeza. Nitajaribu kutoa taarifa kwenye Bunge nalo litaona kwa ujumla kama ipo nia ya kufanya hivyo (kuunda tume),” alisema.
Alisisitiza kuwa chanzo kilipoeleweka kwamba ni ukosefu wa elimu kwa watu wa kawaida, nyoyo za wana Mtwara zimeridhika.
Aliendelea kusisitiza: “Nilipowasikiliza ni bahati mbaya sana jambo halikupaswa kufika hapo. Elimu kwa wananchi wa kawaida juu ya gesi hasa kwa watu wa vijijini, wananchi watarajie manufaa gani, haikuwa imewafikia walio wengi.
“Inawezekana tulio juu tulikuwa tunaelewaelewa… nao walipododoswa walisema walikutana na makundi machache. Wabunge walikuwa wakijua kinachoendelea lakini haikufanyika kiasi cha kutosha. Kwa sababu ya kutoelewa ikatokea uchochezi wakapewa taarifa zisizo sahihi,” alielezea yaliyojiri kwenye mkutano wake.
Kwa upande wake, Waziri Nchimbi alisema wanaoshabikia uvunjifu wa amani, vyombo vya Dola vitatimiza wajibu wake bila kumwonea mtu aibu.
Hata hivyo, alisema hali ya usalama sasa imetengamaa na vyombo vya Dola vimeimarisha ulinzi.
Alionya juu ya mashambulizi yanayofanyika kwa Polisi katika vurugu mbalimbali na kuhadharisha kwamba itafika wakati watu watahofu kujiunga na Jeshi hilo kutokana na kuandamwa. Alionya pia utamaduni uliojengeka wa kuharibu na kuchoma mali za Serikali.
Uharibifu uliotokea Januari 25 Mtwara ni kuchomwa nyumba ya Diwani wa Kata ya Chikongola, Mohamed Chikopa, nyumba ya Waziri wa TAMISEMI, Hawa Ghasia ambayo ilikuwa ikiendelea kujengwa, iliharibiwa kwa kupigwa mawe vioo vya madirisha, milango na kuunguzwa baadhi ya sehemu.
Nyumba nyingine ni ya askari mwenye namba A/Inspekta Jumanne Malangahe katika maeneo ya Sabasaba ambayo iliharibiwa mita ya umeme.
Pia ofisi ya CCM kata ya Ufukoni ilichomwa moto pamoja na kuunguza nyaraka mbalimbali.
Dk Nchimbi alitaja mali nyingine ni gari la Polisi PT 1420 lililoshambuliwa kwa mawe na kuvunjwa kioo cha mbele na pembeni, Mahakama ya Mwanzo ya Mtwara mjini iliyoteketea pamoja na nyaraka mbalimbali.
Katika maeneo ya Magomeni, duka la Mohamed Ali Mchanyambe, ambaye ni Diwani wa Kata ya Ufukoni lilivunjwa na kuibiwa mali mbalimbali zenye thamani ya Sh milioni 30.
Eneo hilo la Magomeni, glosari ya askari E 8935 Koplo Philemon ilishambuliwa na kuibiwa vitu mbalimbali vyenye thamani ya Sh 895,500 pamoja na fedha taslimu Sh 250,000.
Pia alisema askari namba G 5456 Konstebo Shabani, alijeruhiwa kwa kupigwa jiwe kichwani karibu na jicho upande wa kulia na hali yake inaendelea vizuri.
Kwa upande wa wilayani Masasi, watu wanne waliuawa kwa kupigwa risasi wakati wanamshambulia askari kwa kumkata mapanga.
Waliouawa kuwa ni Bakari Hamisi (30) mkazi wa Masasi, Jofrey Simonje (16), na watu wengine wawili ambao hawajafahamika majina yao.
Katika uharibifu huo mkubwa, Dk Nchimbi alitaja magari matano ya Serikali yalichomwa moto likiwamo lenye namba SM 3840, SM 9060 Land Cruiser yote ya kubebea wagonjwa.
Pia gari namba SM 9721, aina ya Isuzu tiper, STK 8417 aina ya Toyota Prado, Land Rover na Toyota Maruti, mali ya Ofisa wa Takwimu. Pia magari 17 na pikipiki nne za watu binafsi.
Alisema nyumba ya Ofisa Elimu, gari la Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Kasembe (CCM) vilichomwa moto.
Aidha, alieleza kuwa Mahakama ya Mwanzo ya Lisekese, Ofisi ya CCM ya wilaya ya Masasi viliteketezwa kwa moto na nyumba binafsi ya askari F3S /Sajini Lusekelo ilivunjwa vioo.
Nyumba ya Askari E.4696 Koplo Hassani ilichomwa moto na askari D/Sajini Taji Osiah Kibona alijeruhiwa kichwani kwa kukatwa mapanga na amelazwa katika hospitali ya Ndanda na hali yake ni mbaya. Waziri Mkuu alisema amehamishiwa Muhimbili, Dar es Salaam.
Dk Nchimbi alisema askari WP 5576 Konstebo Eneck William, chumba chake kilivamiwa na kundi la watu na kuchukuliwa vitu vyote vya ndani, G238 Konstebo Lais Saigirani nyumba yake ilibomolewa yote.
Pia E4696 Koplo Hasani Lipemba nyumba yake ilichomwa moto na E234 Koplo Jonas Mweri nyumba yake ilibomolewa.
Uharibifu mwingine aliutaja kuwa ni pamoja na kuvunjwa na kuharibiwa kwa vifaa vilivyonunuliwa kwa ajili ya ukarabati wa Ofisi ya Fedha, vikiwa na madirisha ya aluminiamu na vioo pamoja na vigae vyote.
Aidha, lango kuu la kuingilia ofisi kuu ya halmashari, liliondolewa mabati ya uzio wa jengo jipya. Ndani ya jengo la halmashauri, waliunguza kompyuta tano za mezani, kompyuta mpakato nne, printa tano, skana na mashine moja ya kudurusu.
Waliunguza chumba cha kuhifadhi vitu vya thamani ya Idara ya Maliasili yenye silaha na bunduki moja pamoja na shehena ya mbao zilizokamatwa iliteketezwa kwa moto.

No comments:
Post a Comment