![]() |
| Profesa Sospeter Muhongo. |
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, ameeleza kushangazwa kwake na maandamano ya kuzuia gesi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam na kufafanua kuwa gesi nyingi haiko katika mkoa huo.
Akizungumza jana ofisini kwake Dar es Salaam, Profesa Muhongo alisema gesi inayopatikana Mtwara ni asilimia 14 tu ya gesi yote iliyogundulika nchi kavu na baharini (futi za ujazo trilioni 32).
Mbali na Mtwara, alifafanua kuwa Lindi ina asilimia saba na Pwani asilimia moja huku asilimia 78 iliyobaki ikipatikana kwenye kina kirefu baharini.
“Gesi nyingi inapatikana kwenye mipaka ya nchi na si mipaka ya Mtwara, na pia inapatikana kwenye miamba yenye umri mkubwa ambako mipaka ya Afrika, Tanzania wala Mtwara haikuwapo,” alisema.
Akielezea sababu za kusafirisha gesi kwenda Dar es Salaam, Profesa Muhongo alisema ni kutokana na asilimia 80 ya shughuli za uchumi nchini zinazochangia pato la Taifa kufanyika Dar es Salaam.
Alisema sababu za kiuchumi na kupunguza gharama, ndizo zilizoifikisha Serikali kuamua kusafirisha gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.
Alisema upelekaji gesi Dar es Salaam utaisaidia Serikali ambayo inatumia takribani dola milioni 1.7 kwa siku kuzalisha umeme kwa mafuta na hivyo kuokoa dola bilioni 1 (Sh trilioni 1.6) kwa mwaka ikiwa miundombinu ya gesi itakamilika miezi 18 ijayo.
Alisema kwa sasa uniti moja ya umeme inayofuliwa kwa mafuta ni kati ya senti za Marekani 30 hadi 40 wakati bei ya uniti moja ya umeme unaotengenezwa na gesi ni senti za Marekani sita hadi nane, ambazo huenda zikapungua kutokana na matumizi.
“Pia Serikali inaweza kuokoa dola milioni 202 kwa mwaka endapo jiji la Dar es Salaam litatumia gesi asili badala ya mafuta katika magari, taasisi na majumbani.
“Fedha zitakazookolewa zitatoa mchango mkubwa kwenye uchumi wa Taifa letu kwa manufaa ya Watanzania wote wakiwamo walioandamana na walioratibu maandamano ya Mtwara Mjini,” alisema Profesa Muhongo.
Profesa Muhongo alisema sababu nyingine ni miundombinu mikubwa ya usafirishaji na usambazaji umeme kwenda mikoa mingine ambayo iko mbali na Dar es Salaam na kujenga miundombinu hiyo sehemu nyingine ni ghali kuliko kujenga bomba.
Alisema kuna utafiti wa gesi na mafuta unaoendelea Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Manyara, Kigoma, Mbeya, Njombe, Rukwa, Katavi, Morogoro na Tabora na katika mipaka ya Tanzania na Kenya na Msumbiji.
“Sitarajii kama watu wa mikoa hii nao wataandamana kama walivyofanya wa Mtwara, kwa kutaka kupewa upendeleo wakati rasilimali ni za Watanzania wote,” alihadharisha.
Alisema kwa sasa Mtwara haina shughuli za kiuchumi za kutumia gesi hiyo peke yao na kuwa tangu kuanza kutumika kwa gesi ya Mnazi Bay Desemba 2006, Lindi na Mtwara kunazalishwa umeme wa megawati 18 na unaotumika ni megawati 12 kwa siku.
Aidha, Profesa Muhongo alisema Serikali imezingatia maendeleo ya maeneo husika na kuwa katika miundombinu ya kusafirishia gesi inayojengwa, imewekewa matoleo ya kuchukulia gesi muda wowote itakapohitajika katika matumizi ya viwanda na majumbani.
Alisema Serikali imetenga eneo katika pwani ya mikoa ya Kusini kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vikiwamo vya mbolea na saruji, ikiwa ni pamoja na kiwanda cha kusindika gesi ambavyo vitasaidia ajira kwa watu wa eneo hilo.
Akizungumzia ushirikishwaji wa wananchi, Profesa Muhongo alisema Serikali imeshirikisha wadau wote kabla ya kuanza mchakato wa ujenzi wa miundombinu hiyo.

No comments:
Post a Comment