![]() |
| Marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki' |
Msanii mahiri katika tasnia ya filamu nchini, Juma Kilowoko ‘Sajuki’ aliyefariki dunia jana, anatarajiwa kuzikwa keshokutwa kwenye makaburi ya Kisutu, Dar es Salaam.
Sajuki alifariki dunia jana asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ambako alilazwa baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Akizungumzia jana msiba huo, Mwenyekiti wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF), Simon Mwakifwamba, alisema shirikisho limekubaliana na familia kumzika kesho kutwa ili kutoa fursa kwa wanandugu walioko nje ya Dar es Salaam kuwasili.
Alisema mbali na kuwa msanii, lakini pia Sajuki ana taswira ya utaifa, hivyo ni vema kwa wanajamii, wadau wa filamu na watu wengine pia wakashiriki msiba huo.
Akizungumzia mchango wa Sajuki katika filamu, Mwakifwamba alisema amekuwa ni zaidi ya msanii kwa kuwa alitoa mchango mkubwa katika kuinua tasnia hiyo nchini.
Alisema Sajuki alikuwa pia mwanaharakati wa kupigania sanaa nzima kiujumla kwa kuwa alikuwa pia muasisi wa chama cha watayarishaji filamu nchini.
Mwakifwamba alisema Sajuki alikuwa mpigania haki mzuri za wasanii kwa kuhamasisha vita dhidi ya wezi wa kazi zao pamoja na kupigania maslahi ya wasanii kwa ujumla.
Sajuki ameacha pigo kubwa katika filamu kwa kuwa alikuwa na upekee katika kuendeleza tasnia hiyo na alisema wasanii wote kwa pamoja wanaungana katika kipindi hiki kigumu.
Akizungumzia hatua ambazo mpaka sasa TAFF imechukua katika kusaidia msiba huo alisema kuwa imeunda kamati sita; za chakula, fedha, usafiri na mapokezi, habari, maziko na itifaki.
Msemaji wa familia, Cosmas Chidumule, alieleza kushitushwa kwake na msiba huo hasa ikizingatiwa kuwa ndugu yao alikuwa ameshaanza kupona.
Alisema kifo cha Sajuki si tu ni pigo kwa tasnia ya filamu, bali pia kwa wanandugu kwa kuwa walimpenda kwa ucheshi wake na ukarimu katika familia.
Kaka wa marehemu, Salum, alisema dakika chache kabla ya kufariki dunia, Sajuki alimwita mkewe na kumwimbia wimbo wenye ujumbe wa upendo na kisha kumwomba akaurekodi studio na kwa pamoja walicheka.
Akizungumzia wasifu wa marehemu alisema alizaliwa Aprili 4, 1986 Bombambili, Songea mkoani Ruvuma na alianza elimu ya msingi mwaka 1994 na kumaliza 2000. Alijiunga na sekondari mwaka 2001 hadi 2005 kabla ya kujiunga na Chuo cha Sanaa Bagamoyo.
Ni mtoto wa nne kati ya watoto watano wa familia ya Mzee Kilowoko ambao ni Issa, Salum, Sajuki, Zawadi na Ziada.
Mbali na filamu ya Mboni Yangu na The Killer ambazo ni moja kati ya filamu nyingi ambazo Sajuki aliigiza, lakini pia alikuwa na filamu iitwayo Mwanasheria ambayo alikuwa ameanza kuiigiza tangu aliporejea nchini akitokea India kwa matibabu.
Maandalizi ya maziko yanafanyika nyumbani kwake Tabata, Bima na ameacha mtoto Farlihin na mjane Wastara ambaye pia ni msanii wa filamu.
***Taarifa tulizozipata baadaye zinaeleza kwamba msanii huyo atazikwa kesho Ijumaa katika makaburi hayo ya Kisutu, jijini Dar es Salaam. Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote!***

No comments:
Post a Comment