![]() |
| Ndege ya British Airways akitua kwa dharura mjini Lyon, Ufaransa. |
Ndege ya British Airways ililazimika kutua kwa dharura kufuatia wanawake wawili wa rika la kati kuanzisha vurugu ndani ya ndege hiyo ikiwa angani.
Wawili hao wenye umri wa miaka 50 na 43 walifanya timbwili hilo mbele ya watoto, huku wakigoma kurejea kwenye viti vyao na kujaribu kulazimisha kuingia kwenye chumba cha marubani baada ya kuwa wameonekana wakinywa Malibu moja kwa moja kwenye chupa.
Abiria mmoja alidai walifikia hatua ya kutishia kuisaka na kuiua familia ya mhudumu mmoja wa ndege ya shirika hilo inayofanya safari zake kati ya Uwanja wa Ndege wa Gatwick na Tunisia.
Kisha ilidaiwa walijificha katika choo cha ndege aina ya Boeing 737-400 ikiwa umbali wa futi 30,000 kwa ajili ya kuvuta sigara.
Rubani wa ndege hiyo alibadili uelekeo na kuipeleka ndege hiyo mjini Lyon, ambako polisi wa Ufaransa waliwakamata wanawake hao na kuwasweka rumande kwa usiku mmoja kabla ya kuwapandisha ndege ya kurudi walikotoka.
Abiria huyo aliliambia gazeti la The Sun: "Waliamua kwamba wanakwenda kuonana na rubani na watembea kuelekea chumba cha marubani. "Ilikuwa ikiogopesha mno."
Wanawake hao sasa wanaweza kufungiwa maisha kusafiri kwa ndege za British Airways.
Msemaji wa Shirika la British Airways alisema: "Safari ya ndege BA2664 Jumatatu kutoka Gatwick kwenda Tunis ilibadilishwa kwa dharura kwenda Lyon kufuatia tabia endelevu ya kuhatarisha amani kutoka kwa abiria wawili wa kike.
"Wateja wetu na wafanyakazi waliokuwa wakiruka na ndege hiyo wanastahili usalama na kufurahia huduma ya ndege zatu. Hatuendekezi tabia yoyote inayohatarisha amani angani katika ndege zetu."

No comments:
Post a Comment