Watu waliofika kushuhudia sakata hilo la misukule katika Mtaa wa National Housing, mjini Bukoba. |
Watu 22 wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo Bukoba, kwa kosa la kufanya fujo na kuhatarisha amani ya jamii na maisha ya Mwalimu Bernadetha Katabarwa wa Shule ya Msingi Kashai, waliyemtuhumu kukutwa na misukule.
Inadaiwa watu hao, walifanya fujo usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano nyumbani kwa Katabarwa katika Mtaa wa National Housing wakitaka kuteketeza nyumba ya mwalimu huyo kwa madai alichukua watoto msukule.
Fujo hizo zilisababisha Polisi mkoani Kagera kuingilia kati kwa kufyatua mabomu ya machozi ili kuwatawanya mamia ya watu waliokuwa wamezingira nyumba baada ya kuhamasishwa na taarifa hizo kutoka katika redio moja ya kijamii ya Bukoba.
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo, Richard Ngole alisema jana kwa simu kuwa Polisi inaendelea na ulinzi katika eneo hilo kwa kuwa bado watu wanataka kumdhuru mwalimu huyo na tayari watu 22 walifikishwa mahakamani jana.
“Watuhumiwa 22 wamepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Mwanzo kujibu kosa la kufanya fujo, baada ya kusomewa mashitaka, 12 walipata dhamana na 10 walikosa, kesi imeahirishwa hadi Desemba 24 mwaka huu, tunaendelea kuwasihi wananchi waheshimu utu na sheria,” alisema Ngole.
Hata hivyo katika hatua nyingine, Ngole alisema wanaendelea kufanya uchunguzi na upelelezi wa kina ndani ya familia hiyo baada ya kubaini kuwa, kuna tatizo la kiimani ndani yao hadi kusababisha uvumi huo kuleta madhara kwa jamii.
Awali katika tukio hilo, baada ya uvumi kusambaa kupitia redio hiyo kuwa mwalimu huyo amekutwa na misukule ambayo ni watoto wa ndugu yake, watu walifurika eneo la tukio na fujo zao zilisababisha polisi kufunga mtaa na kuweka ulinzi usiku kucha na mchana kutwa.
Inadaiwa Katabarwa alitembelewa na mdogo wake Benedikta Bukene akiwa na watoto wake wawili akitokea kwenye msiba wa mumewe kijijini Bushagara, wilayani Muleba huku nyuma ndugu wa marehemu mumewe wakatoa taarifa Polisi kuwa watoto wamepelekwa kwenye ushirikina Bukoba.
Ngole alisema polisi wa Kamachumu, Muleba waliongozana na ndugu wa marehemu hadi shuleni kwa Mwalimu Katabarwa mjini Bukoba kuwachukua watoto hao Gloria na Denis Bukene waliokuwa na mama yao na baada ya watoto kuchukuliwa, ghasia ziliibuka.
Katika fujo hizo, Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Zipora Pangani ni miongoni mwa watu waliorushiwa mawe na wananchi alipofika kuwatuliza na kuzungumza nao katika eneo la tukio juzi.

No comments:
Post a Comment