Rais Jakaya Kikwete. |
Rais Jakaya Kikwete ameiagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, kuweka mwongozo na kupunguza bei ya viwanja ili wananchi wamudu kumiliki ardhi.
Pia amekemea tabia ya halmashauri nchini, kugeuza viwanja kuwa chanzo cha mapato badala ya kutoa kama huduma.
Alitoa kauli hiyo jana baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa nyumba za gharama nafuu Kibada, wilayani Temeke katika Mkoa wa Dar es Salaam na kuzindua rasmi miradi 14 ya ujenzi wa nyumba nafuu, inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
Amesema halmashauri zimegeuza viwanja kuwa vitega uchumi kwa kuuza kwa bei ya juu, ambayo mwananchi wa kawaida hawezi kumudu na kusababisha ugumu kwa wananchi kumiliki viwanja na mashamba.
“Hata uamuzi wa wanasiasa ni tatizo, utakuta madiwani wanaamua kupanga viwanja kwa bei ya juu, lakini kwa kufanya hivyo madiwani mnafanya jambo la hovyo, uamuzi lazima uzingatie maslahi ya wananchi,” alisema Rais Kikwete.
Akitolea mfano Kibaha, Kikwete alisema; “kule Kibaha, halmashauri zinanunua eneo kwa wananchi kwa shilingi milioni sita na bila hata kuboresha wanauza kwa shilingi milioni 300 au 600… watu wa kawaida hawawezi kununua. Wizara hakikisheni mnaweka mwongozo na kupunguza bei ya viwanja, si kwa shirika pekee, bali hata kwa watu wa kawaida.”
Rais Kikwete pia alisema pamoja na kupitisha sheria mbili za kumwezesha mwananchi kupata mkopo wa nyumba, haridhishwi na idadi ya benki na riba ya juu inayotolewa.
Ameitaka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Wizara ya Fedha na Benki Kuu kuangalia namna ya kupunguza riba hiyo.
“Riba ya asilimia 18 ni kubwa, sasa isipopungua watu watajenga mahali walipo, mtu wa mahakamani atachukua rushwa, hospitalini atauza dawa na kudai rushwa kwa wagonjwa, Tanesco (Shirika la Umeme) vishoka wataongezeka,” alihadharisha.
Aliwataka NHC kuchangamkia fursa hiyo, kwa kuanzisha taasisi ya fedha watakayoitumia kukopa wenyewe na kuwakopesha wananchi kwa riba nafuu, jambo litakaloongoza mabenki mengine kupunguza riba ya mikopo.
Kuhusu ombi la NHC la kutaka kuondolewa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika nyumba zisizozidi Sh milioni 100, Rais Kikwete alisema suala la kuondoa kodi haliwezekani, lakini kinachoweza kufanyika ni kupunguza riba hiyo.
“Kuondolewa kodi haiwezekani, maana hii ni kodi halali, ila kupunguza nitawasaidia kuzungumza nao, lakini itakuwa baadaye kwenye bajeti ijayo. Hatuwezi kuingilia bajeti ya sasa maana itavuruga utendaji wa Serikali,” alisema.
Awali, Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Nehemia Mchechu aliiomba Serikali kuondoa VAT kwenye nyumba na vifaa vya ujenzi ili bei ya nyumba iwe nafuu.
Alisema kutokana na changamoto ya gharama ya ardhi, kodi katika nyumba na vifaa vya ujenzi na ujenzi wa miundombinu, shirika hilo limelazimika kuuza nyumba ya bei nafuu ya vyumba viwili kwa Sh milioni 38.9 kabla ya VAT na ile ya vyumba vitatu kwa Sh milioni 44.
Mchechu alitaja changamoto nyingine, kuwa ni upatikanaji wa ardhi na mamlaka za miji kuchelewesha utoaji wa vibali vya ujenzi. Aliiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kutoa ruzuku kwa shirika hilo.
Mradi wa nyumba za bei nafuu wa Kibada, unatarajia kujenga nyumba 292 kwa awamu mbili na unatarajia kukamilika Mei mwakani.

No comments:
Post a Comment