![]() |
| Ian McKellen |
Mwigizaji wa filamu za "Lord of the Rings" na "Hobbit", Ian McKellen ametangaza usiku wa kuamkia leo kwamba ana saratani ya kibofu.
McKellen ambaye ana miaka 73 sasa alilieleza gazeti la Daily Mirror amekuwa akisumbuliwa na saratani ya kibofu kwa miezi sita au saba iliyopita, lakini amesema si kwa kiasi cha kutishia maisha yake.
"Wakati inapokupata, unaifuatilia kwa ukaribu, na unatakiwa kuwa mwangalifu mno isiweze kusambaa. Lakini kama imejikita kwenye kibofu pekee, si tatizo kubwa."
Aliongeza, "Ninafanyiwa uchunguzi kila mara na imedhibitiwa, haisambai. Sijawahi kufanyiwa matibabu yoyote."

No comments:
Post a Comment