Kamanda Robert Boaz. |
Askari wawili wanaolinda Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA), wamedaiwa kumbaka mama mmoja hadi kumuondoa kizazi chake.
Taarifa hizo zimesababisha wananchi wa Kijiji cha Mbahe Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro kusitisha shughuli za utalii za Kinapa, kwa kufunga barabara inayoingia kwenye lango la hifadhi hiyo.
Habari kutoka eneo la tukio zimeeleza kuwa mama huyo (jina limehifadhiwa), alibakwa Alhamisi iliyopita saa 12 asubuhi ndani ya eneo la Kinapa wakati akikusanya kuni.
Taarifa kutoka Hospitali ya Kilema zimedai kuwa
mama huyo ameharibiwa vibaya sehemu za siri kwa kuchanika pamoja na kizazi kuharibiwa vibaya, hali iliyolazimu ashonwe sehemu hizo nyeti.
Kutokana na tukio hilo, wananchi zaidi ya 300 kutoka katika Kijiji cha Mbahe na vijiji jirani, walijikusanya na kufunga barabara ya Marangu Mtoni, inayokwenda kwenye lango la hifadhi hiyo saa sita mchana juzi. Kutokana na hali hiyo, watalii wanaoshuka na kuingia msituni, walilazimika kusitisha safari zao.
Polisi kutoka kituo kidogo cha Himo na Moshi mjini waliwasili eneo la tukio saa saba mchana na kuanza kufyatua mabomu ya machozi, kuwatawanya wananchi hao waliokuwa wametumia magogo makubwa na mawe, maarufu kama fatuma, kufunga barabara.
Baadhi ya wananchi hao waliwashambulia kwa mawe askari hao huku wakiwa wamejificha kwenye migomba na mahindi, hali iliyosababisha kazi ya kuwatawanya kuwa gumu.
Diwani wa Kata ya Marangu Mashariki, Stanley Mrema alikiri kuwa hali sio nzuri katika eneo hilo, kutokana na wananchi kufunga barabara zaidi ya kilometa mbili.
“Hali huku sio nzuri hata kidogo, wananchi wamefunga barabara kwa mawe makubwa, hata watu kumi hawawezi kuyaondoa…hali imebadilika kwani polisi wanatumia mabomu ya machozi, lakini
wananchi wanajificha migombani na kuwarushia mawe,” alisema Mrema.
Mrema alisema kuwa shughuli za utalii, zimesimama, kutokana na vurugu hizo. Wageni waliotarajiwa kushuka mlimani na kusafiri kwa njia ya ndege saa saba, walishindwa kusafiri, kutokana na hali hiyo. Wengine waliotarajia kupanda mlima, walikwama eneo la Marangu Mtoni.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alikiri kubakwa kwa mama huyo, kulikosababisha wananchi kuandamana hadi kwenye lango la Kinapa kutoa kilio chao, kwa kile walichodai kuwa askari wa hifadhi hiyo ndio wahusika wa tukio hilo.
Boazi alisema kuwa taarifa zinaeleza kuwa mara baada ya mama huyo kubakwa, alirudi nyumbani na kuwaeleza ndugu zake, ambao walimpeleka katika Hospitali ya Kilema kwa ajili ya matibabu.
Alisema kuwa hadi sasa haijafahamika, kuwa waliombaka mama huyo ni askari wa Kinapa au ni watu wengine.
Alisema Polisi inaendelea na msako, kuwabaini wahusika kwani kitendo hicho ni cha kinyama.

No comments:
Post a Comment