Hospitali ambako mtoto huyo alizaliwa akiwa mwenye afya njema. |
Mtoto mchanga amefariki kwa kukosa pumzi baada ya kuminywa akiwa amelala kitandani katikati ya wazazi wake waliokuwa wamelewa pombe.
Wakunga walishamwonya mama huyo - ambaye hakutajwa jina - kuhusu hatari ya kulala kando ya mtoto wake - lakini amekiri kudharau ushauri wao mara kwa mara.
Maelezo ya kina kuhusu mkasa huo uliwekwa bayana katika ripoti iliyokabidhiwa Halmashauri ya Jiji la Coventry.
Mtoto huyo - ambaye ametajwa tu kama Mtoto W - alizaliwa akiwa mwenye afya njema Mei, 2011.
Hatahivyo, mama huyo alipuuza ushauri wa 'ulalaji salama' aliopewa kabla ya kuruhusiwa kutoka hospitali na mara kwa mara alilala na mtoto akimuweka kati yake na mpenzi wake.
Julai mwaka jana aliamka na kugundua mtoto wake hapumui na hivyo kuita gari la wagonjwa, lakini madaktari hawakuweza kuokoa maisha ya mtoto huyo.
Maofisa wa polisi wameanza uchunguzi kamili wakati wazazi hao wakiwa katika huduma za jamii.
Mtoto huyo hakuwekwa katika uangalizi mzuri lakini wafanyakazi waliamua kufanya uchunguzi zaidi wa familia.
Wiki iliyopita bodi ya ulinzi salama wa mtoto ya jiji hilo ilichapisha katika ripoti yake, ambayo ilibainisha kwamba janga hilo lisingeweza kuepukika.
Lakini wakuu wa afya wamesema hili halikuwa janga lisiloepukika na wanawaonya wazazi dhidi ya kuwalaza watoto wao kitandani kando yao.
Katika Coventry yote na Warwickshire watoto 27 wameshakufa kwenye vitanda vya wazazi wao tangu mwaka 2008.
Carmel McCalmont, mkuu wa huduma ya ukunga katika Hospitali ya Chuo Kikuu, Walsgrave, alisema wanawake wote wajawazito na wazazi wapya wamekuwa wakishauriwa dhidi ya ulalaji wa pamoja.
Hatahivyo, alisema baadhi ya wazazi wameendelea kufanya hivyo, pengine sababu walikuwa wamechoka au wamekuwa wakipewa ushauri mbovu na ndugu zao.
"Haijalishi wazazi wamechoka kiasi gani hawatakiwi kushawishiwa kuwaleta watoto wao kitandani kulala nao pamoja."
Lakini licha ya hatari hizo, baadhi ya mashirika ya kujitolea yameendelea kushawishi faida za kulala pamoja na watoto, kama vile kuweka urahisi wa mama kuwanyonyesha watoto wao.

No comments:
Post a Comment