Watoto wakiwa wamekata tamaa kufuatia mauaji ya kimbari yaliyoikumba nchi yao ya Burundi mwaka 1993 na kusababisha vifo vya maelfu kwa maelfu ya watu. |
Viongozi wa dini nchini wamepigwa msasa kuhusu mauaji ya kimbari na kuelezwa kuwa Tanzania ikiwa ni nchi pekee katika Ukanda wa Maziwa Makuu ambayo haijatumbukia katika dimbwi la vita vya kikabila na kidini, wanalo jukumu la kulinda amani iliyopo na kuisambaratisha.
Msuluhishi wa kitaifa wa Burundi, Dk Mohamed Rukara alisema hayo jana wakati akitoa mada katika warsha ya viongozi wa dini iliyoandaliwa na Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Uhalifu wa Mauaji ya Kimbari, Uhalifu wa Kivita, Uhalifu dhidi ya Binadamu na aina zote za Ubaguzi.
Mada hiyo ilihusu hali ya sasa ya kiusalama katika Ukanda wa Maziwa Makuu katika warsha hiyo ya inayohusu nafasi ya dini katika kulinda na kudumisha amani ya nchi.
Dk Rukara aliwaeleza viongozi hao kuwa amani katika nchi za Maziwa Makuu inakabiliwa na matatizo mengi kiasi kwamba ni vigumu kuhakikisha watu wanaendelea kuwa na amani hata wakati ambao hakuna vita.
Msuluhishi huyo aliyewahi kuishi nchini katika miaka michache iliyopita, alisema Mungu ameibariki Tanzania akaizawadia tuzo la amani na usalama. "Ni lazima mlinde maani hii na kuweka mikakati madhubuti kwani kinga ni bora kuliko tiba,” alisema.
Katika mada yake, Dk Rukara alitaja vyanzo vilivyosababisha vita na mauaji ya kutisha katika nchi za Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuwa ni ubaguzi wa aina mbalimbali wa ukabila, dini na rangi.
Alisema licha ya kuwa njia zinatofautiana kati ya Burundi, Rwanda na Kongo DRC, lakini mambo hayo ndio chanzo cha mauaji ya kimbari katika nchi za Maziwa Makuu na bado yanaendelea kuyumbisha usalama na amani katika nchi zote za ukanda huo.
Naye Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Mathias Chikawe alisema Kamati hiyo, ni chombo cha kitaifa kilichoanzishwa chini ya nchi za Maziwa Makuu kwa lengo la kupambana na itikadi, sera na vitendo vyote vya kibaguzi na ukiukwaji wa haki za binadamu.
Alisema kamati hiyo iliyoanzishwa Februari mwaka huu, inaonesha dhamira ya Serikali ya kuendelea kulinda na kudumisha amani iliyopo nchini. Kamati hiyo inafanya kazi kwa ukaribu na Ofisi Maalumu ya Mshauri wa Umoja wa Mataifa juu ya kuzuia mauaji ya kimbari pamoja na Sekretarieti ya Umoja wa Nchi za Maziwa Makuu.
Chikawe aliwataka viongozi hao wa dini kutathmini vyanzo vya vurugu za hivi karibuni vyenye sura ya kidini vilivyotokea Mbagala na Zanzibar na kuabuni mbinu na namna bora ya kushughulikia vyanzo vya vurugu zenye sura ya kidini.
Pia aliwataka viongozi hao kujadili, kubuni na kupendekeza njia sahihi ya kuzuia, kupunguza na hata kuondoa kabisa uwezekano wa migogoro na tofauti za kidini zinazotaka kupandikizwa na watu wachache.
Chikawe pia aliwataka waazishe ushirikiano na mshikamano baina yao na wafuasi wa dini zote.
Kwa upande wao, viongozi hao wa dini walitaja mambo kadhaa yanayoweza kuchangia amani ya Tanzania kutoweka ambayo ni kukithiri kwa tabaka la masikini na matajiri pamoja na viongozi kuweka marafiki zao kama wasaidizi.
Pia walisema kuwa matukio ya hivi karibuni ya kuchoma makanisa yaliyotokea huko Mbagala na Zanzibar yamefanywa na makundi ya watu wanaotumia mwamvuli wa dini.
Wakichangia mada ya Dk Rukara, viongozi hao pia walionya kuwa viongozi wa dini wanastahili kuchunga ndimi zao katika mahubiri yao kwani baadhi yao wamekuwa wakitoa matamshi yanayohatarisha amani.
“Amani katika nchi zote za Maziwa Makuu imetoweka baada ya kuwepo kundi linaloona linaonewa na kuamua kuingia msituni,” alisema mshiriki aliyejitambulisha kwa jina la Shekhe Salim.
Shekhe Yusuph Kundecha alisema viongozi wa kisiasa wamekuwa chanzo cha kuingiza nchi kwenye machafuko na akaonya suala la uteuzi linalofanywa na viongozi kuwa wakati mwingine wanawaweka marafiki zao kwenye nafasi mbalimbali hali inayozua manung'uniko.
“Viongozi waepuke kuchagua marafiki wao kuwa wasaidizi wao kwani inaweza kuleta vurugu,” alisema Shekhe Kundecha na kuongeza kuwa chanzo kingine ni mamlaka za kiserikali kuchelewa kushughulikia malalamiko ya baadhi ya makundi au kuyapuuza.
Naye Fatuma Suleimani katika mchango wake, alisema chuki kati ya matajiri na masikini pia inachangia kuleta migogoro katika nchi. “Huyu ambaye ni masikini ni lazima ahoji huyo amevipataje?” alisema.
Fatuma pia aliwataka viongozi wa dini kuepuka kuwa matajiri kupindukia wakati waumini wao ni masikini wa kutupwa hali aliyoonya kuwa inaweza kuzusha manung'uniko na kusababisha migogoro isiyo ya lazima.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa, Felistas Joseph alisema lengo la kamati hiyo ni kujenga uelewa wa wananchi kuhusu madhara na namna ya kuzuia mauji ya kimbari na kupinga vitendo vinavyoashiria uvunjifu wa amani, ikiwamo kuzuia matamshi ya uchochezi na kunyamazia mambo hayo kwa vyombo husika.

4 comments:
We're just out of a recession barely, and sales prices are up 9% in just one year!! This is not a normal occurrence, and when one sees this type of pattern, you have to be aware that a correction is likely on the horizon. [url=http://www.2012canadagoosepascher.fr]Canada Goose[/url] For our younger guests, ages4 and under, Easter eggs full of surprises will be hiddenin The Big Red Barn. Jeeeeze.. Assistance with finding qualified contractors and pricing out the project is available upon request by the purchaser..
We provide temporary living environments for abandoned, abused, neglected, sick, or unwanted Rat Terriers (and RT mixes). [url=http://www.icanadagooseca.com]canada goose jacket[/url] The role model of smallish, talent-challenged young boys who had dreams of playing in the big leagues, Nellie himself overcame all manner of adversity to become one of the game most beloved and recognized players. [url=http://officialcanadagoosesoutlet.ca]canada goose for sale[/url]
[url=http://flyballbags.com]canada goose down jackets[/url] Dre LeBron James Beats by Dre Turbine steeler beats green Headphones studio solo beats Beats by dre purple orange beat headphones beats blue steeler beats Black studio beats orange beats beats blue solo pink steelers beats blue beatslightning solo solohd pink solo whiteblue studioblue beats solobluesolo hdchromeTurbinebeats by dre tourproschicago bullsblack on black beatsmonster beats by dre Beats by Dr. [url=http://www.onlinebeatsbydreoutlet.com]beats by dre online canada[/url]
I don't leave many comments, but i did a few searching and wound up here "MRUNDI AIONYA TANZANIA KUHUSU MAUAJI YALIYOIKUMBA BURUNDI...". And I actually do have a few questions for you if it's allright.
Could it bе ϳust mе or ԁoеѕ іt look like some of thе reѕponѕes appeаг like theу arе
wrіtten by brаin dеad folkѕ?
:-P And, if you аre ωгіting on additiοnal social
siteѕ, І woulԁ like to fоllοw аnything fresh yοu hаve
tо post. Woulԁ you list of еѵery one of all your ѕhаrеԁ ѕites like yοuг linκeԁin
pгofile, Fасеbook page οr twitteг feеd?
Hеre is my blоg ρoѕt: Fotografo de bodas
Hі, еvery time i used to chеcκ web
site pοsts here in the early hours in thе break of day,
fоr the гeaѕon thаt i like to find оut more and more.
Ηere іs my web-site; fotografos de bodas en europa
Ηі, i thіnκ that і saw уou
visited my web site so i came to “retuгn
the favοг”.I'm trying to find things to improve my web site!I suppose its ok to use some of your ideas!!
Also visit my web page; xenos wedding photographer
Post a Comment