![]() |
| Baadhi ya makaburi ya wanafunzi shuleni hapo. |
Wanasayansi wamegundua ushahidi wa vifo 98 na makaburi zaidi kuliko walivyofikiri kabla katika Shule ya kurekebisha wavulana ya Florida, ambako inadaiwa wanafunzi walipigwa vibaya, kubakwa na kuuawa.
Watafiti kutoka Chuo Kikuu cha South Florida huko Tampa wamekuta mashimo ya makaburi takribani 50 kwenye Shule ya Wavulana ya Dozier huko Marianna, mjini Florida ikiwa ni 19 zaidi ya yale yaliyotambuliwa na Idara ya Utii wa Sheria ya Florida katika uchunguzi wa mwaka 2010.
Kwa jumla, wanasayansi wanaamini kwa uchache watoto 96 wenye umri kuanzia miaka 6 hadi 18, na watu wazima wawili wamekufa kati ya mwaka 1911 na 1973 kwenye shule hiyo yenye sifa mbaya, mazishi mengi kati ya hayo yakiwa hayako kwenye nyaraka.
Ripoti iliyotolewa juzi imeelezea madai ya udanganyifu uliofanywa na shule hiyo, ambayo ilizinduliwa mwaka 1900.
Ilifungwa Juni mwaka 2011 na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu baada ya kuwepo utata wa miaka mingi kuhusu kuzagaa udhalilishaji wa kimwili na kingono.
Ugunduzi huo wa kutisha na matarajio ya kuwepo makubwa zaidi mbeleni - umeibua maswali kwa shule hiyo ambayo kwa sasa imefungwa, wafanyakazi wake na serikali.
Chunguzi zilizopita na mashitaka yaliyofunguliwa na 'Wavulana wa Ikulu' - waliitwa hivyo sababu sehemu kubwa ya udhalilishaji ulifanyika kwenye jengo lenye vyumba 11 lililofahamika kama Ikulu.
Kundi la wanafunzi wa zamani lilishitaki serikali mwaka 2010, lakini kesi yao ilitupwa kutokana na mipaka ya amri ya serikali kupita wake wa mwisho. Wanafunzi wengine waliandika vitabu kuhusu uzoefu wao.
Kufuatia madai hayo, watafiti katika Chuo Kikuu cha South Florida huko Tampa walitumia rada za chini kwa chini na sampuli za udongo na sasa wanaamini kuna miili mingi zaidi iliyozikwa pale kuliko ilivyoripotiwa hapo kabla.
Eneo hilo kubwa la makaburi liko katika upande wa kaskazini wa eneo la shule, ambako wavulana Wamarekani-Weusi walizikwa.
Ni katika eneo hili ambako makaburi 31 yamewekewa alama ya misalaba ya rangi nyeupe, lakini watafiti wanaamini hayahusiani na maeneo halisi ya maziko.
"Tunatazamia kukuta takribani mashimo ya makaburi 25 hadi 30," alisema Christian Wells, profesa msaidizi wa elimu ya binadamu ambaye aliongoza kazi hiyo kwenye eneo hilo. "Lakini kwa sasa tumegundua kwa uchache 50."
Rekodi binafsi za Dozier zinaonesha kwamba zaidi ya watoto 50 walizikwa katika viwanja hivyo, huku miili mingine zaidi ya 30 ilipelekwa kwingineko kwa ajili ya kuzikwa. Lakini shule hiyo ilishindwa kuweka kumbukumbu za maeneo ya maziko kwa watoto wengine 22 ambao watafiti wamegundua walikufa kwenye eneo hilo, gazeti la Miami Herald liliripoti.
Baadhi ya watoto hao - na watu wazima wawili walikufa katika mlipuko wa moto na homa ya mafua mwanzoni wa miaka ya 1900 wakati wengine waliripotiwa kusumbuliwa na matatizo ya kiafya au kiwewe.
Januari, watafiti hao watarejea katika eneo hilo la shule, ambako watoto weupe walikuwa wakiishi. Walisema wanatarajia kugundua makaburi zaidi hapa, pamoja na wavulana ambao pia walibaguliwa katika kifo.
Watoto Wamarekani-Weusi katika shule hiyo walikuwa mara tatu zaidi ya wavulana weupe wanaodhaniwa kuzikwa kwenye maeneo ambayo hayakuelezwa, ripoti hiyo imegundua.
Wavulana saba wanaaminika kufa kufuatia majaribio yao ya kutaka kutoroka, kwa mujibu wa ripoti hiyo.
Kati ya watoto ambao walisahaulika alikuwa mvulana mweupe aliyetajwa kuwa ni Thomas Curry, ambaye alikufa kutokana na kurukwa akili. Rekodi zimedai alikufa mbali na eneo la shule baada ya kuwa ametoroka.
Rekodi za shule hiyo zinadai kwamba wavulana waliotoroka wanaonekana kufa katika ghasia, wakiwamo wawili ambao walikufa kutokana na kujeruhiwa kwa risasi kifuani au kichwani.
Wanafunzi wa zamani wa Shule ya Dozier, sasa wana umri wa miaka 60 au zaini wamesimulia hadithi hizo za kutisha jinsi walivyokuwa wakipigwa kama wavulana, katika miaka ya 1940, 1950 na 1960.
Ovell Smith Krell, sasa ana miaka 83, alisema kwamba kaka yake, Owen Smith, alipelekwa Shule ya Dozier kwa Wavulana majira ya bamvua mwaka 1940, baada ya kuwa ametoroka nyumbani na baaye kuiba na kuvunja gari.
Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa mwaka 2009 na Ovell, familia hiyo haikuweza tena kuwasiliana na Owen. Alisema kwamba mama yake aliiandikia shule kutaka kujua aliko kijana wake, lakini aliambiwa kuwa Owen ametoroka.
Kisha shule hiyo ikasema alikamatwa na kushikiliwa na idara ya uliwali. Pale baba yao alipodai kijana wake, alielezwa kwamba alikuwa amerejeshwa tena Dozier.
Haifahamiki kipi tena kilichompata Owen. Ovell alisema kwamba aliongea na mwanafunzi wa zamani ambaye alisema kwamba Owen alipelekwa kwenye kile kilichofahamika kama Ikulu, sehemu ambako wavulana walikuwa wakitiwa adabu katika eneo la shule hiyo.
Aliandika: "Walipomtoa nje, walikuwa wamembeba. Mvulana huyo alisema walisikia kelele zake za maumivu na kwamba alipelekwa hospitalini."
Shule hiyo ilisema kwamba kuna uwezekano mkubwa alikufa kutokana na nimonia na walikuwa chini ya nyumba hiyo akijaribu kupata joto. Hatahivyo, daktari na mwanasheria wanaoishi katika nyumba hiyo walimweleza Ovell kwamba hawakuwahi kusikia au kuhisi harufu yoyote.
Ovell aliieleza CNN kwamba anatumaini ya kumpatia kaka yake maziko anayostahili. "Nitamchukua na kumweka chini pamoja na mama na baba yangu kwenye kaburi lao," alielezea. "Natarajia kupata nafasi hiyo."

No comments:
Post a Comment