Saturday, December 1, 2012

CHEKA TARATIBU...

Jamaa mmoja alikuwa kwenye matembezi na Malaika ndipo akaanza kutoa dukuduku lake la moyoni, "Najua wewe ni Malaika, lakini unanisikitisha mno!" Malaika akamjibu, "Nakusikitisha nini?" Jamaa akasema, "Kila ninapopita kwenye njia mbaya wewe unanitelekeza, lakini nikifika njia nzuri kama hii unajitokeza pembeni yangu." Malaika akacheeeka na kumjibu, "Unapokuwa kwenye njia mbaya huwa nakubeba na kivuli unachokiona ni changu. Ila unapokuwa pazuri nakuacha utembee mwenyewe sina sababu ya kukubeba!" Duh...

No comments: