Saturday, December 1, 2012

AUA MKE WAKE NA KUMLAZIMISHA MWANAE ANYWE DAMU...

Karunya Limbitu.
Mwanaume mmoja amewaacha wengi midomo wazi baada ya kumuua mkewe na kula sehemu ya viungo vyake, lakini naye akaishia kushambuliwa na kuuawa na kundi la watu wenye hasira usiku wa kuamkia Jumatano wiki hii katika kijiji cha Wendiga, Kieni Magharibi.
Inaelezwa kuwa, mwanaume huyo, Morris Gituma Mutegi (23) baada ya kumuua mkewe alikula moyo, ini, sehemu ya uso na pia kunyonya ubongo, huku akimlazimisha mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka miwili na nusu kunywa damu ya mama yake.
Mutegi, ambaye ni mkulima inadaiwa aligombana na mkewe Caroline Gatwiri (22) muda wa saa tano usiku. Mfanyakazi wao wa ndani, Anne Wangeci alishuhudia Mutegi akifukuzana na mkewe, lakini kelele za kutaka kunusuru hatari yoyote hazikusaidia, kwani wakati majirani wanafika katika nyumba hiyo, tayari Gatwiri alikuwa ameshafanya mauaji kwa kutumia upanga na mkuki.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Nyeri, Karunya Limbitu alisema Gituma na mkewe wanatoka katika kijiji cha Kandungu kilichopo Gitije Meru Kusini.
Maofisa wa polisi waliokuwa eneo la tukio walisema kichwa cha  Gatwiri kilikuwa kimetenganishwa na mwili na kupondwa na jiwe. Kipande cha fuvu na mfupa wa taya vilikuwa bado eneo la tukio hadi asubuhi, lakini baadaye polisi waliviondoa.
Solomon Mwangi, ambaye ni mtoto wa kiume wa Wangeci, alisema Mutegi alimuua mkewe mita chache kutoka nyumbani kwa mama yake kabla ya kuuburuza mwili katika nyumba yake na kisha kuukatakata.
“Amemuua mke wake karibu na nyumba ya mama yangu , muda wa usiku. Kisha aliingia nyumbani kwake kumchukua mtoto wake na kumlazimisha kunywa damu ya mama yake, lakini wakati akiuburuza mwili ndani ya nyumba yake tulifanikiwa kumpokonya mtoto. Alikuwa amejihami kwa upanga na mkuki na hivyo tuliogopa kumkaribia,” alisema Mwangi.
Polisi walisema Mutegi alikula viungo vya mkewe ikiwa ni pamoja na moyo, ini, uso na ubongo.
Kwa mujibu wa Mwangi hatimaye majirani waliokuwa karibu 200 walifanikiwa kumkamata Mutegi, kisha kumfunga katika nguzo ya ukuta kwa kutumia kamba na kisha kumpa kipigo.
“Tulimfungua kwa kutumia kamba, lakini alikuwa mkali kama mynama,” alisema Mwangi.
Mkewe aliwasili jioni akitokea Meru, ambapo  Mutegi alikwenda kumpokea mjini Mweiga kilometa chache kutoka nyumbani kwao.
Alimpeleka mtoto wake kwenda kumsalimia mwajiri wake, akimwambia Wangeci kuwa mkewe alikuwa amepumzika baada ya safari ndefu.
Hadi Alhamisi asubuhi, mtoto huyo alikuwa ametapakaa damu ya mama yake usoni na aliachwa chini ya uangalizi wa Wangeci, lakini polisi wa kituo cha Mweiga kilitoa taarifa baadaye kikieleza kuwa, baadaye watamkabidhi kwa maofisa wa ustawi wa jamii Nyeri.
Mwajiri wake alimwelezea Mutegi kuwa hajawahi kugombana na mtu yoyote tangu aajiriwe kuchunga ng’ombe mwezi Machi mwaka huu.
“Hakuwahi kusikika akimfokea mtu, hata mtoto. Alimleta hata mtoto wake aje kunisalimia baada ya kumpokea mkewe aliyetokea Mweiga na kila kitu kilionekana sawa muda huo,” alisema Wangeci.
Kutokana na tukio hilo, wengi wa majirani wamekuwa wakiizunguka nyumba kwa kutoamini kilicho kilichotokea.

No comments: