Godbless Lema. |
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kujiweka tayari kutumia njia yoyote, kwa kile kinachodai kumkomboa Mtanzania kutoka manyanyaso ya Serikali ya CCM, ikibidi kuingia msituni kama ilivyo kwa Kundi la M23 ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
Kauli hiyo ilitolewa jana mjini hapa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Chadema, Godbless Lema, wakati akizindua operesheni maalumu ya siku sita katika Jimbo la Bunda wilayani Bunda katika Mkoa wa Mara, kwa lengo la kukiimarisha chama hicho iitwayo “Ondoa Wassira na CCM Bunda”.
“Nawaambieni, Chadema hatutakoma kudai ukombozi wa Watanzania, ambao wananyanyaswa kila leo na Serikali ya CCM. Kama tutashindwa kwa njia ya demokrasia, basi tutaingia msituni kama walivyo M23 ili kuhakikisha tunamkomboa Mtanzania,” alisema Lema.
Akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyikia katika eneo la Stendi ya Zamani, Lema alisema ukombozi wa mtu hauji hivi hivi mpaka kuwepo nguvu au shinikizo kutoka nje ya Serikali iliyoko madarakani.
Kutokana na mazingira hayo, Lema alisema Chadema iko tayari kutumia njia yoyote ile ili kuhakikisha Serikali ya CCM inawaachia huru Watanzania, ambao imewanyonya kwa muda mrefu.
Akitumia mifano ya Rais wa Kwanza wa Afrika Kusini, Nelson Mandela na mpigania uhuru wa zamani wa nchi hiyo, marehemu Steve Biko, Lema alisema wanaharakati hao kwa pamoja, hawakukubali kila aina ya mapendekezo mbalimbali waliyokuwa wakiahidiwa na makaburu ili wasogeze mbele na harakati zao za kupigania uhuru wa nchi hiyo.
Alisema wapigania uhuru hao, walikataa mapendekezo hayo na kusimama kidete kuhakikisha Waafrika wanakombolewa.
Lema alisema ingawa Biko alikuja kufa baadaye huku Mandela akifungwa jela miaka 27, lakini hatimaye Uhuru wa Afrika Kusini ulipatikana na sasa wanaharakati hao wameandika historia ya pekee katika taifa hilo.
Alisema jambo hilo, linapaswa kuigwa na wafuasi na wanachama wa Chadema katika kudai uhuru wa Mtanzania.
Hivyo, Lema ambaye alijitambulisha kama Mbunge wa Arusha Mjini aliyeko katika fungate, aliwataka vijana kutoogopa kuingia mwituni kudai uhuru wa Watanzania, wanaoonewa na Serikali aliyoiita katili ya CCM.
Aliwashawishi vijana hao kuwa ni fahari kijana kufa akidai uhuru wa wengi, maana ataacha historia kuliko kufa kama kibudu bila kuacha historia yoyote kwa taifa lake.
“Nimekuja kuwatia shime vijana. Msiogope kuingia msituni kudai uhuru wa Watanzania. Msiogope hata kama kamanda mmoja atapigwa risasi na kufa, tutamzika na kuendelea na mapambano mbele”, alisisitiza Lema.
Kwa mujibu wa Lema, Serikali ya CCM haina huruma hata kidogo kwa Watanzania, maana watu wake wachache wamejilimbikizia mali na kuwaacha watu wengi wakiishi maisha duni yasiyoelezeka yasiyo na uwezekano wa kupata huduma muhimu za kijamii, kama vile maji, elimu, afya, barabara na mazingira kwa urahisi, jambo alilosema halivumiliwi na Chadema.
Kauli hiyo ya Lema inafanana kwa maudhui na kauli aliyowahi kukaririwa akiitoa Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari (Chadema), ya kutaka itangazwe Jamhuri mpya katika mikoa ya Kaskazini.
Naibu Kamishna wa Polisi, (DCP) Isaya Mngulu, alinukuliwa akisema Nassari na wenzake walisema “kama polisi hawatawakamata watu waliohusika na mauaji ya Mwenyekiti wa Chadema Tawi la Usa River, wilayani Arumeru, Msafiri Mbwambo, basi watajitangazia uhuru wa eneo la Meru pamoja na mikoa ya Kaskazini kwa kushirikiana na baadhi ya mikoa ya Kanda ya Ziwa.”
Alisema alitamka kwamba wanampiga marufuku Rais na Waziri Mkuu kutembelea Mkoa wa Arusha.
Kutokana na kauli hiyo, Nassari alijikuta matatani na Polisi ambapo alijisalimisha mwenyewe Polisi akiwa na wakili wake, Albert Msando, ambako alihojiwa kwa zaidi ya saa nne kuhusu tuhuma za kutoa maneno yanayodaiwa kuwa ya uchochezi.
Alipopata dhamana, Nassari alisema Polisi walitaka kujua maana ya maneno aliyoyatoa kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika jijini Arusha. Akifafanua, Nassari alisema lengo kubwa la kauli yake ni kuweka mabadiliko ya kihamasa katika mikoa hiyo ili wengine waone wivu wa kimaendeleo kwa mikoa ya Kaskazini, ambayo imeonesha mabadiliko makubwa.
“Mimi ni mtu mdogo tu, sina nguvu hizo za kutangaza uhuru wa sehemu yoyote ya nchi,” alisema.

No comments:
Post a Comment