![]() |
| Paroko Angelo Burgeo. |
Jeshi la Polisi mkoani hapa, linawashikilia watu watano watuhumiwa wa ujambazi wanaohusishwa na tukio la kuvamia na kuwashambulia kwa silaha za moto, mapanga na nondo mapadri wawili, Angelo Burgeo (60) na msaidizi wake, Herman Myalla (36) wa Kanisa Katoliki Parokia ya Isimani, wilayani Iringa.
Aidha, jeshi hilo limesisitiza kuendelea kuwasaka watuhumiwa wengine wanaodaiwa kukimbia baada ya kuwavamia watumishi hao wa Mungu, kuwajeruhi na kuwapora mali na fedha taslimu.
Hayo yalithibitishwa jana na Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda aliyesema ushirikiano wa polisi na wanakijiji ndio uliowezesha kukamatwa kwa watuhumiwa wanne jana asubuhi, huku mwingine akinaswa nyakati za jioni. Wote wanashikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi mjini Iringa.
“Ni kweli tumewakamata watu wanne, mmoja ni mama wa watuhumiwa wawili…tumekamata bunduki moja imetengezwa kienyeji na baruti gramu 100 na goroli 37. Ufuatiliaji wa polisi na wakazi wa Kata ya Isimani baada ya tukio ndio uliofanikisha kukamatwa kwao…
“Kuna wengine wamekimbia, lakini tunaendelea kuwasaka mpaka tuhakikishe tunawatia mbaroni,” alisema Kamanda Kamuhanda.
Waliokamatwa wametajwa kuwa ni pamoja na Joseph Ngwale (30), Erasto Ngwale (38), Gaitan Kitwange na Anitha Mwinuka ambaye ni mama mzazi wa watuhumiwa wawili, wote wakazi wa Isimani.
Habari zaidi kutoka kwa mmoja wa wananchi wa kijiji hicho aliyeshiriki katika msako huo zinasema kuwa, walianza kuwasaka watuhumiwa hao baada ya kufanya upekuzi katika nyumba ya Joseph Ngwale na kuikuta silaha aina ya gobore inayodhaniwa ilitumika katika ujambazi huo.
Naye Diwani wa Kata ya Kihorogota, Costantino Kihwele alisema baada ya kuwepo kwa tetesi za Ngwale kuhusika katika ujambazi huo, walifanya upekuzi katika nyumba yake na kukuta silaha hiyo.
Alisema baada ya kuwasaka watuhumiwa na kuwanasa, waliwapeleka kituo cha Polisi cha Iringa mjini wanakoendelea kushikiliwa.
Wakati hao wakishikiliwa, jopo la madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa limefanikiwa kumfanyia upasuaji Padri Angelo Burgeo na kumtoa vipande vitatu vya risasi katika ubavu wake wa kushoto.
Padri Burgeo alipigwa risasi na majambazi juzi usiku majira ya saa 4.45 katika tukio ambalo msaidizi wake, Padri Herman Myalla alijeruhiwa vibaya kichwani baada ya kupigwa na mapanga na nondo.
Kaimu wa Mganga Mkuu wa Mkoa Dk. Faustine Gwanchele alisema baada ya kumfanyia upasuaji na kutoa risasi hizo tatu hali ya Padri Burgeo inaendelea vizuri.
“Jana tulimfanyia upasuaji Padri. Angelo tukaweza kutoa risasi tatu sehemu ya ubavuni ambazo zilikuwa zimekwama. Hali zao zinaendelea kuimarika huku tukifanya jitihada za kuwahudumia,” alisema Dk. Gwanchele.
Katika hatua nyingine Dk. Faustine alisema kuwa mlinzi wa Kanisa la Kihesa Bathlomew Nzigilwa aliyejeruhiwa na watu hao bado hali yake ni mbaya japokuwa ameanza kuonesha dalili za kufumbua macho. Siku ya tukio, pamoja na kumjeruhi majambazi hao walivunja kanisa na kuiba mali kadhaa ikiwa pamoja na fedha taslimu sh 500,000.
“Mlinzi wa Kanisa la Kihesa aliyejeruhiwa na kuletwa hapa hospitalini bado hali yake ni mbaya na tumegundua kuwa alivunjika mfupa wa kichwani kwa hiyo tunaendelea kufanya utaratibu wa kuutoa,” alisema.
Na kwa upande wa Padri Myala, Dk Gwanchele alisema hali yake inazidi kuimarika na jana alinza kupata nguvu iliyomwezesha kukumbuka kilichotokea na kuongea kidogo.
Katika tukio la Isimani, mmoja wa majirani na Parokia inayoongozwa na Padri Burgeo, Ephraim Mpogole juzi aliwaambia wanahabari kwamba majambazi saba walivamia makazi ya viongozi wa Parokia hiyo.
"Walivunja mlango wa kuingilia sehemu anayoishi Padri Myalla wakampiga mapanga na nondo kabla ya kumwamuru atoe fedha na kumtaka awapeleke kwa Padri Burgeo," alisema.
Naye Padri Burgeo akizungumza kwa shida hospitali hapo alisema wakati majambazi hao waliokuwa wameficha sura kwa vitambaa vyeusi wakichukua Sh milioni 1.3 kutoka kwa Padri Myalla, kwake walichukua zaidi ya Sh milioni 2.5 na simu mbili za mkononi.
Padri huyo raia wa Italia ambaye ameishi nchini kwa miaka 34 akifanya kazi ya Mungu kupitia Kanisa hilo, alisema mmoja wa majambazi hao alitaka kumwua kwa risasi baada ya jitihada zake za kutaka kukimbia kutozaa matunda.
"Walipoingia na kutaka niwape fedha na mali zingine nilizonazo nilitaka kukimbia, wakati nikifanya hivyo nilipigwa nondo kichwani na baadaye risasi na wakati nikitapatapa kwa maumivu nikawaonesha sehemu niliyokuwa nimehifadhi fedha, wakachukua na kutokomea," alisema.
Akizungumzia matukio ya viongozi wa madhehebu hayo ya dini kuvamiwa na kujeruhiwa, Bruda Augustino Kagine aliitaka Serikali na hasa Jeshi la Polisi kuimarisha ulinzi.
Alisema kabla ya majambazi kuvamia Parokia ya Kihesa, walivamia na kumjeruhi Paroko wa Parokia ya Nyololo wilayani Mufindi kabla ya kutokea kwa tukio hilo katika Parokia ya Isimani.
"Tumeanza kuishi kwa hofu, kwa sababu hatujui baada ya viongozi wetu hawa ni nani ndani ya Kanisa letu atafuata," alisema.

No comments:
Post a Comment