Sunday, November 18, 2012

BINTI JASIRI AELEZA ALIVYOBAKWA NA BABA YAKE MZAZI...

Robert Hawksworth (kushoto) na Emily.
Msichana jasiri jana alielezea jinsi baba yake alivyombaka katika tukio ya kusikitisha wakati alipokwenda kumtembelea baba huyo wakati wa mapumziko ya mwishoni mwa wiki.
Robert Hawksworth mwenye miaka 54 alimnywesha mvinyo binti yake Emily ambaye wakati huo alikuwa na miaka 17 katika nyumba yake huko Derbyshire kabla ya kumlaza kitandani na kisha kuanza kumbaka.
Binti huyo alikuwa akidhalilishwa kijinsia na Robert tangu akiwa na miaka 14, lakini alibaki kimya hadi tukio hilo la ubakaji mwaka jana, pale aliporipoti tukio hilo kwa polisi.
Binti huyo mwenye miaka 18, ambaye wazazi wake walitengana wakati akiwa na miaka saba, sasa ameibuka kudai haki yake kwa kuongelea kijasiri kuhusu mateso yake ili kusaidia watoto wenzake wanaopitia katika kama hiyo.
"Nilipoamka asubuhi nilijihisi mgonjwa na nilihisi kuna kitu kimefanyika," alisema Emily, ambaye alikuwa bikira hadi wakati wa tukio hilo la kutisha. "Nilihisi nimeshambuliwa.
"Nilikaa kitandani siku nzima na Jumapili aliendelea kunilazimisha niende naye mjini na kunipa vidonge ninywe.
"Nilikataa kuvipokea sababu sikutaka kuamini kilichotokea.
"Nilikuwa nina chuki naye na sikutaka nianzishe majibizano.
"Nilipokwenda nyumbani Jumapili usiku, sikupanga kumweleza chochote mama lakini mara tu nilipofika nikaanza kububujikwa na machozi.
"Alifahamu kuna kitu kimenitokea hivyo nikamweleza. Alichanganyikiwa na kupiga simu polisi."
Jumatano Robert, ambaye amekanusha kubaka na kudhalilisha kijinsia, alifungwa kwa miaka minane baada ya kesi katika Mahakama Kuu ya Debry.
Emily alisema mwanzoni hakuripoti kilichotokea sababu alijawa na hofu..
"Nilikuwa mdogo wakati huo," alisema. "Sikufahamu jinsi ya kulishughulikia suala hilo."
Robert mkazi wa Findern huko Derbyshire, alikana kumbaka binti yake wakati alipokamatwa, na kumlazimisha atoe ushahidi katika kesi yake.
Akimhukumu kifungo, Jaji John Burgess alimweleza Robert: "Alikuja kukutembelea kama ambavyo alikuwa akifanya mara kwa mara mwishoni mwa wiki.
"Wakati wa tukio la hiyo Ijumaa jioni wewe na yeye mlikuwa mmekunywa mvinyo na kinywaji, pombe uliyoandaa wewe.
"Alilewa sana na alikuwa mgonjwa mno. Ulimbeba na kumlaza kitandani.
"Usiku huo ulikuja chumbani kwake, ukamvua nguo zake za ndani na kumwingilia kimwili.
"Alikuwa ni bikira hadi wakati unamfanyia unyama huu. Huu ulikuwa ni uvunjaji mkubwa wa imani na ukatili kwa binti asiyeweza kulindwa."
Robert alitengana na mama wa Emily mwaka 2001 baada ya kumwingiza katika mahusiano ya 'lugha chafu za kupindukia', mahakama ilielezwa.
Jana mama wa Emily, Karen Atalay mwenye miaka 53 alielezea mateso ya binti yake kama ya 'kutisha na kusikitisha'.
Alisema: "Nilijihisi mwenye hati mno. Nilihisi lilikuwa kosa langu.
"Ndoa yangu na Robert ilitawaliwa na lugha za matusi lakini nilikuwa naogopa mno kumweleza yeyote chochote.
"Nilijipa moyo kwamba mwishowe tuna suluhisho.
"Tukajikuta wote inakuwa ngumu mno kuishi maisha ya kawaida."
Emily, ambaye amechoma picha zote na zawadi alizoletewa na Robert, amebadili jina lake la pili katika harakati za kufuta kabisa uwezekano wa kuhusishwa na baba yake.

No comments: