![]() |
| KUSHOTO: Raymond Hewlett. KULIA: Madeleine McCann. |
Polisi wanachunguza upya endapo kama marehemu Raymond Hewlett, mtu anayejihusisha kufanya mapenzi na watoto alihusika kwa namna yoyote katika kupotea kwa Madeline McCann.
Mpotovu huyo mwenye miaka 64 alikuwa akiishi umbali ya saa moja kwa gari kutoka alipokuwa akiishi binti huyo aliyetoweka mjini Algarve Mei 2007 wakati akiwa mapumzikoni na wazazi wake.
Wapelelezi wa Scotland Yard sasa wanadaiwa kutaka kuongea na wapenzi ambako mtesaji watoto alikuwa na urafiki nao wakati wakiwa katika mapumziko na mtu aliyedaiwa kuwaeleza matapeli walimfuata wakitaka kuwanunua watoto wake.
Alan na Cindy Thompson wakazi wa Nottingham, walikuja kubaini baada ya mapumziko yao nchini Ureno historia hiyo ya askari huyo wa zamani waliporejea nyumbani, na kutoa taarifa pale walipotambua amekuwa akiishi kwenye tela la gari karibu kabisa na sehemu ambapo mtoto huyo wa miaka mitatu alitoweka, liliripoti gazeti la Daily Mirror.
Mpotovu huyo, ambaye alifariki kutokana na saratani ya koo mwaka 2010, aliwaeleza wapenzi hao kwamba alikataa kuuza watoto wake sita kwa
'watalii matapeli'.
Pia alijigamba mbele yao kufanya 'safari nzuri ya kibiashara' na familia yake nchini Morocco kufanya mauzo, lakini hakuweza kufafanua kiini hasa cha safari yake.
Idadi kubwa ya watu iliwasiliana na mamlaka husika kueleza kwamba walimwona binti huyo akitembea huko Afrika Kaskazini baada ya kuwa ametoweka.
Lakini Hewlett, ambaye alikuwa akiishi na mkewe na watoto sita katika tela la gari wakati Madeleine alipotoweka, alikataa kujibu maswali ya Thompson pale walipomfuata mwaka 2009.
Pale alipokabiliwa ana kwa ana na wapelelezi Dave Edgar na Arthur Cowley, wakifanya kazi kwa niaba ya wazazi wa Madeleine Kate na Gerry McCann, alikataa kujibu maswali yao kwa kutoa kisingizio, iliripotiwa.
Madeleine alitoweka siku kadhaa kabla ya kutimiza miaka minne kutoka katika nyumba ya wazazi wake iliyoko Algarve resort of Praia da Luz wakati wazazi wake, Kate na Gerry, wakipata chakula cha usiku na marafiki kwenye mgahawa ulioko jirani.
Ubainishaji huo wenye mashaka wa Hewlett umekuja baada ya mtu mwingine kusema kwamba alizungumza nao kuhusu madai ya mpotovu huyo kwamba matapeli walimfuata kuhusu kununua watoto.
Askari wa zamani wa jeshi la ulinzi, Peter Verran mwenye miaka 46, ambaye alikutana na Hewlett katika kambi ya Mmorocco kati ya Juni na Novemba 2007, alisema mhalifu huyo alimweleza kwamba matapeli walimlipa kwa ajili ya watoto aliowauza kwa watu wanaojihusisha kufanya mapenzi na watoto.
Mwaka 2012, Hewlett 'alikiri' kufahamu kilichokuwa kikiendelea kwa binti huyo mdogo kwenye kitanda chake cha mauti, ilidaiwa.
Raymond Hewlett alimwandikia kijana wake wa kiume akikataa kushiriki katika utekaji nyara wa mtoto huyo wa miaka mitatu, lakini akadai anafahamu 'ameibwa' na genge la matapeli.
Hewlett hapo kabla alidai kumuona mtoto huyo aliyepotea mara mbili kabla hajatoweka mwaka 2007.
Lakini aliapa tu kufichua mahali alipokuwa usiku aliopotea endapo angelipwa maelfu ya Pauni za Uingereza.
Wapelelezi binafsi wa Kate na Gerry McCann walikataa ombi hilo.
Wapelelezi walisema watapitia takribani nambari za simu 100 ambazo zilipigwa sababu wapigaji walisema walikuwa mabingwa wa maono au walikuwa na ndoto kuhusu uchunguzi wa hali ya juu.
Policia Judiciaria walikataa kuthibitisha kama walishawahi kumhoji mtu huyo anayejihusisha kufanya mapenzi na watoto, gazeti hilo liliripoti.
Msemaji wa Polisi alilieleza gazeti la Daily Mirror: "Hatujajiandaa kujadili chochote kuhusu tukio hili."
Hewlett alifungwa mara kashaa nchini Uingereza kwa udhalilishaji wasichana wadogo kwa ngono, ikiwamo shambulio la mwaka 1978 ambapo alimwekea bunduki mlengwa wake kwa nyuma.
Juni 2009, kabla ya kifo chake, Polisi wa West Yorkshire walithibitisha maofisa wake walikuwa wakimchunguza Hewlett kuhusiana na udhalilishaji hadharani uliotokea mwaka 1975.

1 comment:
The primary factor is to have some sort to item to continue to keep that can be shared with other family members and/or shut friends.
People when visiting Tampa Bay often ask what they need to visit and what are
some must doing activates at that place. Tampa Bay Realty also takes care of features like a highly sophisticated infrastructure with a wide network of road, air, water and rail transportation.
Also visit my site ; tampa
Post a Comment