![]() |
| Kevin Durant (mwenye mpira). |
Kevin Durant ameingia tena kwenye mapambano dhidi ya madai ya kisheria yanayodai kwamba ameiba jina la utani "Durantula" kutoka kwa mwanamuziki wa miaka ya 1980 ... akibisha kwamba hakujibatiza mwenyewe jina hilo na wala halitumii kwa ajili ya kujipatia fedha.
Kama ilivyoripotiwa hapo awali, nyota huyo wa Oklahoma City Thunder alishitakiwa na mpiga gitaa Mark Durante, ambaye alidai alisajili kibiashara jina hilo na kulitumia kuuza bidhaa kwa kipindi kirefu kabla Durant kuingilia kati.
Lakini katika majibu yake dhidi ya tuhuma hizo -- katika nyaraka zilizowasilishwa mahakamani mapema mwezi huu katika Mahakama ya Illinois Federal -- Durant anadai vyombo vya habari na mashabiki wake wamekuwa wakimwita kwa jina hilo kwa wakati wote wa uchezaji. Durant anasema hajawahi kutumia jina hilo kwa ajili ya kuuzia bidhaa ... hivyo madai ya Durante hayana mashiko.
Kwa kuongezea, Durant anadai Durante (ambaye amewahi kucheza katika Public Enemy, The Aliens na The Next Big Thing) kwamba hakuna yeyote anayeweza kuwachanganya wawili hao.
Durant anataka madai hayo yatupiliwe mbali kabisa na anataka Durante kulipa gharama zake za kesi.
Jaji bado hajatoa uamuzi wa mwisho.

No comments:
Post a Comment