![]() |
| Philip Mangula. |
Philip Mangula anatarajiwa kurejea tena katika ulingo wa kisiasa katika ngazi za juu za CCM baada ya kuteuliwa kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
Mangula aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM kwa miaka 10 ya utawala wa Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Mwenyekiti Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, sasa njia ni nyeupe kurejea katika safu ya juu ya uongozi wa CCM.
Juzi, Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) pamoja na NEC yenyewe, vilimpitisha mwanasiasa huyo mkongwe kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi utakaofanyika kesho na Mkutano Mkuu wa Taifa.
Jana, wakati Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete alipotangaza jina lake, ukumbi wa Kizota ulilipuka kwa shangwe, kuashiria kukubaliana na uteuzi wa kada huyo kutoka mkoani Njombe.
Awali, Katibu wa NEC wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, alitangaza uteuzi huo wa Mangula na Dk Ali Mohammed Shein kwa umakamu wa Zanzibar, kwa waandishi wa habari jana asubuhi Kizota.
Baadaye, Rais Kikwete katika hotuba yake ya ufunguzi aliwatangazia wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Nane kuhusu uteuzi huo na kushangiliwa.
Mangula alikuwa katika uongozi wa Rais Mkapa hadi alipoondoka madarakani kikatiba mwaka 2005 na katika uteuzi wa Sekretarieti ya kwanza ya Rais Kikwete, aliteuliwa Yusuf Makamba.
Makamba, naye alitemwa mwaka jana na kuteuliwa Wilson Mukama, ambaye duru za siasa hapa zinaeleza kuwa uwezekano wa kurudi ni mdogo.
Akizungumzia uteuzi wa Mangula, mwanasiasa mkongwe nchini, Paul Kimiti alisema kada huyo ni mtu mchapakazi, mwadilifu na anayeaminika.
“Huyu ni mtu mwadilifu. Ni zao la Mwalimu Nyerere, mtu asiyekuwa na tuhuma mbalimbali. Ni mtu msafi, mwadilifu, kiongozi anayeaminika,” alisema Kimiti.
Alisema kurejea kwa Mangula katika uongozi wa juu wa CCM kutakuwa msaada mkubwa kwa chama.
Akishinda kesho, Mangula atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya CCM na anatarajiwa kuwa atarejesha chama hicho ‘katika mstari’ baada ya siku za karibuni kunyooshewa vidole kwa kukosa maadili miongoni mwa wanachama wake.
Uteuzi wa Dk Shein ulitarajiwa hasa baada ya kuwa Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kuamua kuendelea kushika wadhifa huo hata baada ya kuondoka madarakani mwaka 2010.

No comments:
Post a Comment