Sunday, November 25, 2012

MWIGIZAJI MKONGWE WA TAMTHILIA YA "DALLAS' AFARIKI DUNIA...

Mwigizaji Larry Hagman, anayefahamika zaidi kama J.R. Ewing kwenye filamu ya "Dallas" amefariki dunia akiwa na miaka 81.
Hagman alifariki Ijumaa katika hospitali ya Dallas majira ya Saa 10:20 jioni, kutokana na matatizo kufuatia mapambano yake ya hivi karibuni dhidi ya saratani, kwa mujibu wa ripoti mbalimbali.
Familia ya mwigizaji huyo ilitoa taarifa muda mfupi baadaye ikisema: "Alikuwa kazungukwa na wapendwa wake wakati akiaga dunia. Kilikuwa kifo chema, kama ambavyo alikuwa akitamani iwe."
Hagman pia alikuwa mhusika mkuu katika filamu ya "I Dream of Jeannie" lakini alikuwa maarufu mno kwa kucheza kama mhalifu J.R katika miaka ya 1980 kwenye tamthilia ya "Dallas" -- na hivi karibuni kufanya kibwagizo hicho hicho katika toleo la TNT ... ambacho kilizinduliwa mapema mwaka huu.
Hadi mauti yakimfika, Hagman alikuwa na watoto wawili tu.

No comments: