![]() |
| Abu Qatada (kushoto) akitoka gerezani mapema jana. |
Mtuhumiwa wa ugaidi, Abu Qatada jana ameachiwa huru kutoka gerezani alikokuwa akishikiliwa ambapo Serikali ya Uingereza imesisitiza kukata rufani kupinga hatua hiyo.
Qatada alionekana mwenye furaha wakati akishuka kutoka kwenye gari lililomchukua kutoka gerezani na kuelekea moja kwa moja nyumbani kwake ambapo alilakiwa na mamia ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari.
Hapo awali alikuwa zameshinda rufani yake kupinga kurejeshwa kwao Jordan kukabiliana na mashitaka, ikiwa ni pigo kubwa kwa serikali ambayo imekuwa ikijaribu bila mafanikio kumtimua Uingereza kwa kipindi cha karne.
Mtu huyo ambaye wakati fulani alitambulishwa na Jaji kama mtu wa mkono wa kuume wa Osama Bin Laden katika Ulaya, amekuwa akipinga kurejeshwa kushitakiwa nchini Jordan, ambako alihukumiwa kwa makosa ya ugaidi bila kuwapo mahakamani mwaka 1999.
Mahakama ya Rufaa ya Uhamiaji ilizuia kurejeshwa kufuatia kutothibitishwa na Serikali kwamba hakuna ushahidi wa mateso ambao ungetumika dhidi yake katika Jordan.
Majaji wa Kamisheni Maalumu ya Rufani za Uhamiaji walisema Serikali ya Uingereza 'haijaturidhisha kwamba ...hakuna hatari' kwamba taarifa zilizopatikana katika mateso haziwezi kutumika kwenye kesi ughaibuni.
Qatada - ambaye wanasheria walisisitiza siku za nyuma kwamba hawezi kutendewa haki katika kesi nchini Jordan - aliruhusiwa kuishi Uingereza mwaka 1994, lakini Serikali kwa nguvu zote inataka kumrejesha kwao.
Waziri wa Mambo ya Ndani, Theresa May amehakikishiwa na Jordan kwamba hakuna ushahidi uliopatikana kuhusu mateso ambao ungetumika dhidi ya Qatada, ambaye kwa sasa yuko gerezani.
Wizara ya Mambo ya Ndani ilisema Serikali 'haikubaliani kabisa na hukumu hii', akiongeza kwamba itakata rufani kupinga uamuzi huo.
Msemaji alisema: "Tumepata uhakika si tu kuhusiana na atakavyochukuliwa Qatada mwenyewe, lakini kuhusu ubora wa taratibu za kisheria kwamba utakaokuwa ukifuatwa wakati wote wa kesi yake.
"Vilevile, hukumu hii ya leo (juzi) imegundua kwamba 'Idara ya Mahakama ya Jordan, wanapenda wenzao wa ngazi za juu, wanadhamiria kuhakikisha kwamba mrufani atapata, na kuonekana akipata, hukumu ya haki'. Hivyo tutahitaji nafasi kupinga uamuzi wa leo (juzi)."
Kamisheni Maalumu ya Rufani za Uhamiaji (SIAC) ilipewa ushahidi katika siku saba za kusikilizwa kesi hiyo mwezi uliopita na Profesa Beverley Milton-Edwards.
Amejifunza hali ya kisiasa ya Jordan kwa miaka 25 na alisema mwezi uliopita kwamba Qatada amebaki kuwa 'mtu mwenye utata' katika Jordan na hukumu ya haki haitarajiwi.
"Kwa mtazamo wangu siamini kuna ushahidi wowote wa uhakika kwamba mahakama ya usalama wa taifa imejihusisha kwa kiwango kikubwa kujibadili kuweza kujiamini aweze kupata hukumu ya haki," alisema.
Jaji wa Mahakama Justice Mitting alimuuliza Profesa Milton-Edwards kama hati ya makubaliano ya Jordan na Uingereza kuhakikisha kwamba Qatada atapewa hukumu ya haki inaweza kuvunjwa.
Profesa Milton-Edwards alisema, "Chini ya muundo wa kisiasa na mahakama, itakuwa vigumu kumpatia yeyote hukumu ya haki licha ya ahadi za kimataifa au uwazi mpana wa kesi kama hii."
Mapema mwaka huu alikataliwa kibali cha kuhamishia kesi hii katika mahakama ya Ulaya, lakini alishinda katika SIAC, mahakama ndogo ambayo inashughulikia urejeshwaji nyumbani na kesi za usalama wa taifa.
Qatada, ambaye anasemekana kuwa na msaada mkubwa kutoka kwa watu wenye siasa kali, alionekana kwenye ibada iliyoonekana kwenye video mbalimbali katika jengo la mmoja wa walipuaji wa Septemba 11.
Amepingana na kushinda kila jaribio kutoka kwa Serikali kwa karne iliyopita kutaka kumpandisha ndege kumrejesha kwao.
Desemba mwaka 2001, Qatada alikuwa mmoja wa watu wanaosakwa kwa udi na uvumba nchini Uingereza baada ya kuendelea kukimbia nyumba yake iliyoko Acton, magharibi mwa London na kuingia mafichoni.
Oktoba 2002, alikamatwa na polisi katika nyumba ya halmashauri huko kusini mwa London na kushikiliwa katika gereza lenye ulinzi mkali huko Belmarsh.
Usikose kusoma mfululizo wa matukio ya Qatada kesho.

No comments:
Post a Comment