![]() |
| Kamanda wa Polisi, Faustine Shilogile. |
Askari wa Opareshani Okoa Bonde la Kilombero, mkoani Morogoro waliokuwa kazini katika Kata ya Chita, Tarafa ya Mngeta, Wilaya ya Kilombero wamemuua mfugaji, Dasu Hima (25) kwa risasi ya makalioni, baada ya kuvamiwa na kikundi cha wafugali waliokuwa na sime na fimbo.
Wafugaji hao wanadaiwa kuwavamia askari hao katika Kijiji cha Udagaji na kuwalazimu askari hao kufyatua risasi 17 hewahi kujihami na mapigano kutoka kundi la vijana zaidi ya 10 la wafugaji hao.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilongile, akizungumza kwa simu jana kutokea Mjini Ifakara, wilayani Kilombero, alithibitisha kuuawa kwa mfugaji huo.
Alidai mfugaji huyo aliuawa Novemba 10, mwaka huu saa 11: 30 jioni katika Kijiji cha Udagaji, Kata ya Chita, Tarafa ya Mngeta, wilayani humo wakati askari wa vikosi vya mgambo walipokuwa wakilinda ng’ombe zaidi ya 300 waliovamia maeneo hayo.
Kamanda Shilongile alidai wakati askari sita kutoka vikosi hivyo wakilinda ng’ombe hao wakisubiri wahusika waje kulipa faini na kuwaondoa kuwapeleka sehemu walizotengewa nje ya wilaya, ghafla walivamiwa na vijana zaidi ya 10.
Vijana hao wanadaiwa kuwa na silaha za jadi ikiwemo fimbo na sime na baada ya kuwavamia askari, waliowashambulia wakitumia fimbo ngumu na sime.
Kutokana na shambulio hilo, Kamanda Shilongile alidai mmoja wa askari alilazimika kufyatua risasi 17 hewani ili kuwatisha vijana hao, lakini walitumia ujanja wa kuinama chini ya ng’ombe na mwingine kuibuka na kuvamia askari wenye namba E 7183, Koplo Charles kwa kumpinga na fimbo mkononi na begani na kusababisha aanguke chini.
Kwa mujibu wa madai ya Kamanda huyo, askari huyo akiwa ameanguka chini aliendelea kushikilia silaha yake na katika kujihami alifyatua risasi iliyompata Hima (25) aliyekuwa na silaha za jadi fimbo na sime, sehemu ya matakoni.
Pia mdogo wake Hima, Dafe Hima (22) anayedaiwa kuwepo kwenye uvamizi huo alijeruhiwa mguu wa kushoto, wakati vijana wengine walikimbia.
Alisema, vijana watatu na askari mmoja waliojeruhiwa walipatiwa matibabu katika zahanati moja iliyopo karibu na kijiji hicho, isipo kuwa majeruhi mmoja aliyepigwa risasi matakoni alifariki dunia kutokana na kumtokwa damu
nyingi akiwa njiani kufikishwa katika zahanati hiyo.
Kutokana na sakata hilo, Polisi inawashirikilia vijana wawili , Huhende Lulinga (26) mkazi wa Kitongoji cha Uga, Kijiji cha Udagaji na Dafe Hima ( 22) na kuwasaka wengine waliohusika na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

No comments:
Post a Comment